John Pombe Magufuli ni pandikizi la CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Pombe Magufuli ni pandikizi la CHADEMA?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Uswe, Mar 13, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Waziri John Pombe Maguli, tofauti kabisa na ilivo kawaida ya mawaziri wengine wa CCM, anaonekana ni mtu makini, anayezingatia utawala wa sheria, asiyechanganya siasa na kazi na mtu mwenye kujali maslahi ya umma kuliko maslahi ya mafisadi wachache

  .
  Inawezekana John Pombe Magufuli akawa ni pandikizi la chandema ndani ya ccm?
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sio pandikizi la Chadema ila ni mchapa kazi asiyependa kunufaisha wachache. Hongera sana Magufuli na Chadema ni chama ambacho kinazingatia maendeleo ya nchi
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 550
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwa mda mrefu sana mimi nimeamini kwamba Magufuli ni pandikizi la CDM. Hii imethibitika wiki iliyopita pale waziri mkuu alipompinga wazi wazi. Sababu hasa ya kumpinga mbele za watu ni kuonesha kwamba huyupo katika kundi lao. Nafurahi sana kuona CDM tayari imeshapata mapandikizi.
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,612
  Likes Received: 2,380
  Trophy Points: 280
  Nyote hamumfahamu vizuri Siwakuwa pandikizi chadema,kwani chadema wana historia naye kwa mgombea wa chato!!
   
 5. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Achen upuuz mtu akiwa against na RA basi ni pandikiz. pambaaaf
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Thanks again kuiinua CHADEMA,Yes Magufuli ni mwanachadema damu! na tunamtayarisha kuivunja CCM, utagundua kipindi cha kugombea urais 2015. (utopia)
   
 7. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 6,625
  Likes Received: 8,005
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani. Sawa sawa Uswe?
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,597
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  nina amini kabisa kuwa mh pombe ni mmoja wa awatu makini waliopo ndani ya ccm.
  la msingi ni walio ndani ya ccm kuwaondoa wote waliochafuka ili mfumo uwe kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Magufuli alikuwa mchapakazi hodari tangu enzi za mkapa wakati chadema bado haijaonekana kwenye ramani ya siasa za tanzania nakumbuka mkapa aliwahi kutamka waziwazi kwamba katika mawaziri wake wote magufuli alikuwa mchapa kazi hodari na akampa mlinzi wa kumlinda (bodyguard). Ina maana wakati ule magufuli alikuwa pandikizi la NCCR MAGEUZ!
   
 10. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukumbuke kuna vyama vya siasa na kuna wanasiasa, haimaanishi kuwa kwa sababu chama cha CCM kimeshikwa na wanasiasa MAFISADI basi miongoni mwa wanasiasa/wanachama wa CCM hakuna wachapakazi au watu safi. Ni MAGUFULI huyuhuyu alisimama kidete kuhusu kuuzwa kwa jumba za serikali na baadhi ya nyumba anatuhumiwa kuchakachua uuzaji wake watu wote walimshambulia hata wasio safi mfano. ROSTAM kupitia gazeti lake la RAI walibeba Bango sana kuhusu kashfa hiyo sababu si mwanamtandao wenzao. Leo karudi tena kwenye CHAT, CDM mnaanza kudai ni member wenu mmempandikiza CCM je alipochakachua kuhusu mijengo ya UMMA mbona hatukuwasikia kusema ni Pandikizi lenu ndani ya CCM?
  Tabia hii ya CDM kukimbilia majina makubwa (wanasiasa) inaanza kuwatafuna bila wao kuelewa oneni mlivyo mkumbatia MABERE MARANDO bingwa wa kutetea MAFISADI mahakamani ktk kesi wanazo shtakiwa kwa UFISADI wa Rasilimali za UMMA. Pia mmembeba SHIBUDA ambaye kwenye nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi mnaanza kumuona MZIGO. Sasa MAGUFULI anarudi kwenye kiwango chake mnadai PANDIKIZI lenu. Kweli siasa ni mchezo wa karata tatu.
  Tukumbuke CCM,CUF,CDM,NCCR,TLP,NLD,NRA,UMD,UPDP,JAHAZI ASILIA vyote ni vyama vya siasa ambavyo ndani yake kuna wanasiasa, wanasiasa hao wamo wasafi na wachafu, wazalendo na Mafisadi. Hivyo Tusizame katika kushabikia vyama kama vile vinaongozwa na MALAIKA tukummbuke vyama vyote vinaongozwa na wanasiasa hivyo ni jukumu letu kuwapima na kuamua nani anatufaa kuwa kiongozi wetu
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tamaa ya Fisi kusubiri mkono wa Binadamu udondoke ale nyama!
   
 12. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,258
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Hizi sifa isijekuwa ni mitandao ya fitina za kuelekea 2015?
   
 13. U

  Uswe JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sasa mbona utendaji kazi wake unakinzana kabisa na msimamo wa CCM? unakumbuka ile issue ya samaki? unaona jinsi anavosimamia sheria huyu bwana? mi napata taabu kuamini huyu jamaa ni CCM
   
 14. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,832
  Likes Received: 2,109
  Trophy Points: 280
  hakuna alie msafi ndani ya SISIEM aaaaaaaaaaaaaghh.FULL STOP.
   
 15. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  What is Good is always Good, hakuna cha upandikizi hapo ni uchapakazi wake tu hata ndani ya CDM mnayotaja kuna wasio na uzalendo kama walivyo kwa CCM, kinachotakiwa ni wananchi kuwatambua na kuwamwaga wakati wa uchaguzi 2015 bila kujali itikadi. Kama mtu wa Chadema, CUF au NCCR hafai usimpe kura kwasababu unataka wapinzani waongoze au kwasababu mtu ni wa CCM chama chako ushakula posho na Tshirt na Kofia umebeba unapiga kura halafu unaanza kujutia. Tulia, tafakari chukua hatua.
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Inaonekana wewe ndie pandikizi la mafisadi na unajaribu kufanya kazi uliyotumwa hapa jamvini.

  Ciao,

  Tiba
   
 17. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uswe uswe uswe..........kwangu mimi binafsi sioni kama hizo sifa anazo magufuli peke yake na tujifunze sana siasa za tanzania na msione Raila Odinga ni njinga alipokuja hapa tz baada ya kushindwa uchaguzi,na kabla Jacob Zuma hajapata uraisi alikuja hapa pia kwa muda wa siku chache,leo hii Museven anajitapa kama a good product of tanzania,tusijifanye hatumjui Milton Obote alitokea wapi,Joachim Chisano na Samora Mashel hatuwakumbuki?Laurent Kabila na mwanae je hatujala nao mihogo ya kukaanga hapa tz?...orodha ni ndefu sana CCM huwa wanacheza na hii jamii yetu jinga kwa kututafutia mtu ambaye anakubalika sana lakini matokea yake ni haya ya kaka yetu JK yuleee anaondoka na uchumi wetu...tujifunze kujua tatizo siyo mtu ...tatizo hapa ni chama chenye wazuri wachache na wabaya wengi.

  kauli ya kingunge; wakati wote chama chetu kinanatafuta mgombea atakayekifanya chama kijinadi kupitia yeye...do we remember him what he said?


  usafi wa mwili si usafi wa roho hata mnikate kichwa.....because I was born so, do not expect I will leave it to you.
   
 18. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,571
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Ccm humchakachuaga kila mara , toka enzi za Nkapa hadi baby face Pinda
   
 19. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pombe Hafai Kuwa Hata Katibu Kata Kwani ni Muhasherati Kupindukia.
  [​IMG]
   
 20. milioni milioni

  milioni milioni JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2015
  Joined: Mar 25, 2013
  Messages: 1,656
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 280
  We nawe,
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...