TANZIA John Nyerere afariki dunia

R.I.P john, Poleni familia nzima na Mola awape subira katika wakati huu mgumu.
 
Mwana jf mwenzetu Andrew, poleni sana kwa msiba huu mkubwa na nadhani ndio wa kwanza kwa mtoto wa Mwalimu!.

Kusema ukweli baadhi ya wanafamilia wa Baba wa Taifa wako too low profile kiasi licha ya mimi kukulia jirani na Pale Msasani huku tukisoma darasa moja na Milton sikuwahi kusikia lolote kumhusu John zaidi ya kusikia alikuwa na cheo cha Capt. wa JWTZ na alikuwa ni fighter pilot wa Jet.

RIP Capt. John Magige Nyerere.

Pasco

Hapo kwenye Bold usahihi ni JOHN GUIDO NYERERE
magige ni EMIL
 
Kwa kumbukumbu zangu, John (sasa marehemu) na Andrew wote wawili walikuwa marubani wa ndege za kivita pale Ngerengere Kizuka air force na waliacha jeshi kabla ya vita ya Uganda. Naomba kusahihishwa.
 
John Nyerere,mtoto wa nne wa Mwalimu Julius Nyerere,amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.

Kwa Mama wa Taifa Maria, Andrew, Mada, Mako, Anna, Rose, chifu Wanzagi na wanafamilia wote, poleni sana kwa kuondokewa na mwanafamilia, tunawapenda na kuwaombea subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Rest in Eternal Peace John.
 
Poleni sana wafiwa na Mungu awape nguvu ya kustahimili ktk kipindi hiki kigumu kwenu.
 
Nilimuuliza Butiku kuhusu Yericko. Butiku akasema nipe namba yake ya simu,nitamtafuta. Nilimpa Butiku hiyo namba. Sijui jambo gani lilitokea. Lakini baadaye Yericko akasema kwamba yeye hayupo katika familia ya Nyerere. Anajiita Nyerere kwa ajili babu yake mhehe alikuwa anaitwa Nyerere.

Pole Kamanda,kipindi cha nyuma kidogo niliwahi kukuuliza kuhusu hili na hukunijubu,lakini naona umeleta jibu wakati huu ambao siyo wakati muhafaka,kwa mtazamo kama Yericko anapenda kujiita jina hilo naona tumpe nafasi afanye hivyo labda analilia kazi alizofanya baba yako,nakushauri usiendelee na mjadala dhaifu kama huu kwani hautusaidii tena hapa tulipofika,hata mimi kesho naweza kujiita Rosemary Nyerere ili tu kukumbuka kazi za baba yako!
 
Andrew Nyerere : Poleni sana familia ya Nyerere kwa msiba huu.
Kapteni John Nyerere atakumbukuwa sana na wana anga wa jeshi kutokana na umahiri wake wa kumudu ndege za kivita wakati wa ujana wake.

Samahani mkuu najua hii ni tanzia,hila kuna jamaa wakati anamnadi makongoro Nyerere alidai watoto wa vigogo w waligoma enda jeshini mwaka 1978-vita ya kagera hispokuwa makongoro peke yake...vipi tena na huyu mbona ni rubani alipigana vita gani?samahani
 
Back
Top Bottom