John Mnyika: waraka kwa Chenge kuhusu kodi ya kadi za simu

John Mnyika: waraka kwa Chenge kuhusu kodi ya kadi za simu

Ndugu wanaJF,
Hivi sasa kuna malalamiko mengi sana yanatolewa na wananchi wa kada mbalimbali kuhusu kodi ya kumiliki laini ya simu.Viongozi wanalaumiana wanateteana wananyoosheana vidole.Wabunge wanalalamika(sio wote) vyama vinalalmika na kutoa matamko.Ukweli ni kwamba kodi hii haifai na ni kukandamiza wananchi.Pamoja na hayo yote mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya bunge letu ameibuka na kusema kwamba walifanya utafiti wa kutosha na kwamba ushauri wao ni sahihi.Kwa chenge hii kodi ni halali na haimuumizi mwananchi.Lakini tuulize chenge ana credibility gani kutetea watanzania.
Binafsi nilishangazwa na bunge kumchagua chenge kuongoza kamati hii nyeti.Ni chenge huyuhuyu aliyeingia mikataba ya kuwanyonya watanzania alipokuwa mwanasheria mkuu.Yeye alikuwa ni sehemu ya wizi mkubwa uliofanyika wakati wananunua rada.Ni chenge ambaye ana account nje ya nchi na ina bilioni za hela.Hiyo peke yake inaonyesha chenge hana uchungu na watanzania ndio maana katuibia na kaweka hela nje ya nchi.
Tunapompa jukumu la kututetea katika suala zima la kupunguza mzigo kwa wananchi,sioni kama chenge anacredibility hiyo.Tayari ameshafanya usaliti na ndio maana bado anasisitiza hii kodi na fair kwa watanzania.Chenge anahisi kipato chake ni sawa na mama yangu kule kijijini ambaye mimi ndio nimemnunulia simu na vocha ninamwekea kwani yeye hana uwezo wa kufanya hivo.Katika mazingira hayo mama yangu atakuwa halipi kodi badala yake mimi namlipia and at the same time nalipia laini zangu tatu.
Tujiulize kwa nini nchi hii watu ambao wana skendo ndo tunawapa madaraka?Hivi juzi tu generali shimbo ameteuliwa kuwa balozi china na mwaka jana kulikuwa na habari za chinichini kwamba anamiliki mabilioni nje ya nchi.
Imefika wakati watanzania tufanye maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
 
Dogo badala ya porojo angeanza kushuguhlikia matatizo ya Ubungo kwanza.

Siku zinaisha!!!

Kwa hiyo we unaona hii ni porojo? Wewe ndo unaleta porojo! Hata mwezi haujapita mmemkosakosa kumlipua, kama anapiga porojo mnamfuata fuata wa nini? Hili la sim card tutabanana nao tu mbaka kieleweke.
 
Dogo badala ya porojo angeanza kushuguhlikia matatizo ya Ubungo kwanza.

Siku zinaisha!!!

Hivi wewe ni mtanzania kweli au kikaragosi fulani kutoka nchi isiyotutakia mema. Nazisoma posts zako nyingi na kwa kweli zinatia kichefuchefu yaani haujali wala huna uchungu na mambo yanavyoendelea. Umejaa ubinafsi na umbumbumbu uliokithiri na wala nafsi yako haikushitaki kweli. Hapa swala sio ushabiki wa siasa bali ni kupigania (kwa pamoja) hatma ya nchi yetu ambayo licha ya potential kubwa inapelekwa kuzimu na walafi wachache. usipobadilika siku ukifa hata shetani atakukataa maana umemzidi kwa roho mbaya. Shame on you ..sucker!
 
Dogo badala ya porojo angeanza kushuguhlikia matatizo ya Ubungo kwanza.

Siku zinaisha!!!

Si bora yeye ana miaka 3 tu madarakani, Wenye miaka 50 na ushee wapo na bado wanazurura mtaani bila kufanya cha kueleweka zaidi ya kuficha ripoti kila kukicha.
 
Hili suala ni mzigo kwa wananchi wa kipato duni.
Baadhi ya kodi hazina uhalisia kwenye maisha ya watanzania. Serikali iache kukopi na kupesti hizi kodi toka nchi za nje.
 
Naipenda sana hii ya kutoa namba za hawa Overpaid; Under performing MPs.., yaani sasa angalau wafanye kazi kidogo kwa kujibu maswali ya wananchi na sio kulalamika namba zetu za simu zimetolewa.., as if kazi yao sio wawakilishi wa wananchi na wanavuta pesa kwa kazi hio..

Nadhani next tupatiwe personal number ya JK ni mengi aliyoahidi wananchi wangependa kumuuliza
 
Wakti wa mijadala na mafisadi mbona ulikwisha kitambo Mnyika? Hatuwezi kuwa tunakaa mezani na viongozi wanafiki na vigeugeu toka CCM: Pindi tukitoka mezani na maazimio, wao wanayakiuka na kufanya walitakalo.

Way forward? Seriously, Mnyika, you know there is no such thing when dealing with THIS government.

Yatosha sasa. Tunaanza na Economic Boycott of the Mobile Communications Subsectors. Other subsectors will follow; Consumer Goods, Public Transport, Public Safety, Entertainment and Sports, you name it.

If it takes putting to task economic sanctions on this nation, setting it back 50 years, so be it!

Did I also mention we will boycott the power sector? Solar energy is abundant, so is wind.

Unaweza kumpeleka ng'ombe kisimani, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji!

Tumekamuliwa maziwa mpaka yamekuwa damu sasa. Inatosha!

First Boycott: Nationwide Mobile Phone Switch-off, kuanzia saa 6 usiku, 19-8-13 hadi saa 6 usiku, 20-8-13, ikiwa ni saa 24. HII NI KWA MITANDAO YOTE YA SIMU! YOTE!
 
Last edited by a moderator:
vipiki2 hakuna kusubiri mpaka 2015. Kwa sababu gani ya msingi? Vita dhidi ya ufisadi ni endelevu. Mwanzo wake haujulikani na mwisho wake pia.
 
Last edited by a moderator:
Dogo badala ya porojo angeanza kushuguhlikia matatizo ya Ubungo kwanza.

Siku zinaisha!!!

Ni kweli,Sijui na JK atamaliza lini kutekeleza ahadi zake kwa wananchi manake siku zinakwisha!!!! Ikiwemo ya Uwanja wa ndege wa kimataifa kila Mkoa...na Meli kubwa kuliko MV Bukoba..bila kusahau Maisha bora kwa kiiiiiila Mtanzania.....!!!!!!!!
 
Dogo badala ya porojo angeanza kushuguhlikia matatizo ya Ubungo kwanza.

Siku zinaisha!!!

hili swala la kodi ya simu ni sumu kubwa kwa CCM.
Yani mmeamua kuwaadhibu watanzania kwa kuwatoza kodi yenye kuwakandamiza kwa maslahi ya mafisadi.

NB:
Kama unataka kumjibu mnyika nakushauri uje na takwimu hapa, la sivyo utazidi kujichoresha wewe binafsi na unazidi kuitia aibu ccm hii inayokufa.
 
kp24072013.jpg

​
 
Back
Top Bottom