PreGE2025 John Mnyika: Mbowe hana nia ya kuhama Chama wala kugombea Urais

PreGE2025 John Mnyika: Mbowe hana nia ya kuhama Chama wala kugombea Urais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,144
Reaction score
56,411
Anaandika John Mnyika kwenye ukurasa wake wa X:

mnyika.png

Nimewasiliana na Mwenyekiti Mstaafu Freeman Mbowe amenieleza hana dhamira ya kugombea urais, ubunge au uongozi wa chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Natambua kuwa wachache waliojiondoa CHADEMA baadhi yao wamekuwa wakitumia jina lake kushawishi baadhi ya viongozi wa Chama na wenye nia ya kugombea kujiondoa kwenye Chama kwa madai kuwa anawaunga mkono na anajiandaa kugombea urais kupitia Chama kingine.

Natambua pia mfumo wa Serikali na CCM uko nyuma ya baadhi yao kwa nia za kukwamisha No Reforms No Election, kupasua Chadema na kuhalalisha udhalimu na uharamu unaoandaliwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Natambua kuwa mfumo huo huo ukihusisha mtu wa karibu na Rais Samia na mtumishi mmoja wa Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ORP Tanzania ndio uliohusika kufungua kesi ya Said Issa Mohamed aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar na wenzake ambayo wameomba pamoja na mambo mengine shughuli za kisiasa za Chadema zizuiwe wakati kesi ya msingi ikiendelea.

Kwa uzoefu wangu wa kuwa kwenye Sekretariati ya Chama kwa takribani miaka 21 mapito mengi ya Chadema ambayo tulifanikiwa kuyashinda. Hii vita dhidi ya Chadema naamini pia tutaishinda.

Tuelekeze nguvu kwenye mapambano ya No Reforms No Election Tumjue vizuri adui yetu, tuwajue vizuri washirika wetu. Tuepuke kushambuliana sisi kwa sisi mpaka iwepo sababu ya kweli na ya lazima yakufanya hivyo. Kwa umoja na nguvu ya pamoja, tutashinda.

Pia soma Pre GE2025 - John Mnyika, usimuamini sana Freeman Mbowe licha ya yeye kukanusha habari ya yeye kugombea uraisi kupitia chama kingine cha siasa
 
Nimewasiliana na Mwenyekiti Mstaafu @freemanmbowetz amenieleza hana dhamira ya kugombea urais, ubunge au uongozi wa chama chochote cha siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Natambua kuwa wachache waliojiondoa @ChademaTz baadhi yao wamekuwa wakitumia jina lake kushawishi baadhi ya viongozi wa Chama na wenye nia ya kugombea kujiondoa kwenye Chama kwa madai kuwa anawaunga mkono na anajiandaa kugombea urais kupitia Chama kingine.

Natambua pia mfumo wa Serikali na CCM uko nyuma ya baadhi yao kwa nia za kukwamisha #NoReformsNoElection, kupasua Chadema na kuhalalisha udhalimu na uharamu unaoandaliwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Natambua kuwa mfumo huo huo ukihusisha mtu wa karibu na Rais @SuluhuSamia na mtumishi mmoja wa Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa @orpptanzania ndio uliohusika kufungua kesi ya Said Issa Mohamed aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar na wenzake ambayo wameomba pamoja na mambo mengine shughuli za kisiasa za Chadema zizuiwe wakati kesi ya msingi ikiendelea.

Kwa uzoefu wangu wa kuwa kwenye Sekretariati ya Chama kwa takribani miaka 21 mapito mengi ya Chadema ambayo tulifanikiwa kuyashinda. Hii vita dhidi ya Chadema naamini pia tutaishinda.

Tuelekeze nguvu kwenye mapambano ya #NoReformsNoElection. Tumjue vizuri adui yetu, tuwajue vizuri washirika wetu. Tuepuke kushambuliana sisi kwa sisi mpaka iwepo sababu ya kweli na ya lazima yakufanya hivyo. Kwa umoja na nguvu ya pamoja, tutashinda.
Huyu jamaa wa nyika hamna kitu hapo, maana alitamba kutokusaini kati ya vyama 19 Cha kwake kikakataa kwa kauli yake, Sasa asubiri kuvishwa koti la lawama. Kwa kifupi, hakuona mbali.
 
Mnyika ajue wasaliti ni vyema kuondoka,

Viongozi ni wengi mno,

Wataibgia kwa maelfu wakipishana mlangoni na wasaliti.
 
Mnyika ameandika kwa wingi wa hofu tele, lakini si dhambi, kwa mh. Mbowe kwenda popote kwa muda fulani nasisitiza si dhambi, anaweza kwenda kusaidia vyama vingine! Ili angalau tupate chama kingine chenye nguvu, pili itakuwa kama political practical na challenge, tatu, kwanini mnyika amewahi kwa haraka sana kuipigia simu mbowe!, wajinga pigeni baragumu, huyu ni msaliti 😊😊😊
 
Back
Top Bottom