iron finger
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 358
- 221
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA Mnyika Leo amewaaga wapiga kura wa jimbo la kibamba kutokana na ombi la mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwataka wana kibamba wamruhusu mbunge wao mtarajiwa aende mikoani kwa ajili ya kuongeza nguvu katika majimbo yote ya ukawa na pia kujazia kura za urais.
Ombi hilo la Mbowe lilikubaliwa kwa sauti kubwa ya ndio na maelfu ya wapiga kura wa kibamba huku wakisema kwamba jimboni hapo mh Mnyika hana haja ya kupiga kampeni kwani tayari ni mbunge anayesubiri kuapishwa.
Kuanzia kesho Mnyika atajiunga na kundi lingine la wabunge machachari kina Lissu, Mdee,Lema, Kafulila na wengineo katika kampeni kali ya kutafuta kura za ukawa majimbo yote Tanzania
Amzungumzia Dr. Slaa
Mnyika alimfananisha mchumba wa aliyekuwa mke wa katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa bi Josephine kuwa ni kama Delila aliyetumia ulaghai kumpotosha Samson.
Mnyika alisema kwamba adui wa Mabadiliko sio mtu toka ndani ya CCM ila ni mfumo wa CCM mzima na yeyote atakayesapoti mfumo wa CCM ni adui wa mabadiliko.