John Kaduma!

Sawa sawa kabisa na ndani yake ilipatikana makala ya stanslaus katabalo ikihusu loliondo.akiita loliondo-gate.wapo wengi tu kuna emmanuely kibiki yo man.
 
Sawa sawa kabisa na ndani yake ilipatikana makala ya stanslaus katabalo ikihusu loliondo.akiita loliondo-gate.wapo wengi tu kuna emmanuely kibiki yo man.

Stan Katabalo namfananisha na Saed Kubenea. Naona aligombana na "wakubwa." Emmanuel Kibiki nilikuwa naona stori zake katika Jarida la Tabasamu pamoja na Bakari Masasi (Ras).
 
hivi hadithi ya panga la shaba alichora nani? marco tibasima wapi b.mkora, mmenikumbusha mbali sana

Panga la Shaba alichora John M. Kaduma. Bado naitafuta stori hiyo...

Marco Tibasima yupo... anapatikana hapa. Bi Mkora nina muda sijaiona... alikuwa anachora Robert Mwampembwa.
 
Mkuu asante kwa taarifa!
 
Umenikumbusha anga za wenyewe mkuu, hiyo nadhani alikuwa anachora fortunatus ndila.
Niliwahi kusikia ndila alifungwa kipindi fulani baada ya kushirikiana na mtoto wa kigogo flani wakamuibia huyo kigogo pesa ili waende marekani lakini baada ya kufanikiwa kuiba hiyo ela ndila akaamua baki hapa hapa tz, mwenzake akaondoka. Sijadhibitisha lakini nilisikia hiyo kitu.

Nadhani huyu ndo mchoraji wa ile hadithi ya "anga za wenyewe", mtanisaidia mnaokumbuka vizuri.
 
Mkuu elmagnifico hiyo skendo ya Ndilla sikuwahi kuipata, ngoja waje wadau wenye taarifa kamili watatusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Kazi nyingine ninazozikumbuka za huyu gwiji john m kaduma ni ile ya MZUNGU WA UNGA (pablo zungu) ilikuwa inazungumzia masuala ya madawa ya kulevya katika jarida la KIU,
hata hivyo jarida hilo lilifutwa muda mfupi kwa sababu zisizojulikana.
Majarida mengine yaliyotamba enzi hizo ni pamoja na AMBHA na KINGO (james gayo wa kenya).
 
Tuwa ndiye alinifanya niache kusoma hadithi za shigongo... Hussein Tuwa ni mkali, ila pia riwaya za msiba na willy gamba zilikuwa zinasisimua kweli.
Hivi ni nani aliyeandika riwaya ya azina iliyo laaniwa?
 

Mkuu fanya hima tupate vitu vya ukweli tulivyovimiss miaka kadhaa iliyopita,
nasubiria kwa hamu sana mkuu.
 
Namkumbuka sana huyu jamaa kaniburudisha sana nikiwa primary kipindi icho tukawa tunacopy michoro yake R.i.p kaduma
 

daah kaka ume nikumbusha hii kitu pablo zungu aisee!! ilikua kwenye jarida la Tabasamu toleo la kwanza na hadithi ikaanza!
r.i.p john kaduma he inspired me to be a good artist especially kwenye uchoraji maskini kipaji changu hakija nifikisha popote mfumo wa elimu ya bongo shida sana inaua vipaji sana,shuleni wame nitumia sana kuchora vitu mbali mbali.
 

Enzi ZA TABASAMU, BONGO Daah siku zinaenda kasi sana asee
 
Kwenye jarida la ambha kulikua na love story Tanganyika na unguja sio mchezo zama zinaenda
 

Mkuu vipi upon?
 

Mkuu umenikumbusha mbali sana kwa kweli. Mpaka machozi. Hivi pia gazeti LA Watu lilikuwaje? Michapo nakumbuka lilifungiwa na Dr. William Shija kipindi hicho akiwa Waziri wa Habari na Utangazaji nadhani kwenye 1991-92 hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…