PreGE2025 John Heche: Shughuli ziendelee bila kutumia rasilimali za chama

PreGE2025 John Heche: Shughuli ziendelee bila kutumia rasilimali za chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Heche anaelewa maana ya raslimali za chama ? Ni pamoja na human resource ya chama ambayo ni pamoja na viongozi sio magari na fedha tu
Hata yeye haruhusiwi sababu na yeye ni rasilimali ya chama
 
CHADEMA tunapenda tusomeke kuwa sisi ni wapigania haki na pia tunaheshimu misingi ya sheria na utawala bora hivyo tuna wajibu wa kuheshimu maamuzi ya mahakama katika misingi iliyo ya haki na kweli kamwe hatutasujudu kwenye mambo ya hila na ukandamizaji. Tuna kusudi la kuomba la kuomba mapitio upya yaani review ya hukumu hiyo ya tarehe 10, juni 2025 maana amri zilizotolewa hazina msingi wa haki.”

“Wakati jambo hili likiendelea kufanywa na wanasheria wetu tunawaelekeza wanachama amri zifuatazo. Amri ya zuio la kutokujishughulisha na shughuli za siasa imeelekezwa kwa Katibu Mkuu na bodi ya wadhamini hivyo viongozi wengine wote na wanachama tunawaelekeza kuendelea na shughuli za kisiasa kama kawaida bila kutumia rasilimali za chama. Hivi sasa chama kipo kwenye program ya kichama ya kuziba mapengo vikao hivi viendelee na kazi hii ikamilike kama ilivyopangwa”

Amesema John Heche akizungumza kupitia akaunti ya YouTube ya CHADEMA MEDIA TZ leo Juni 17, 2025.
Ametoa amri….
 
CHADEMA hairuhusiwikufanya siasa ikiwemo kutumia Raslimali watu

Heche hajui maana ya raslimali za Chama
 
Back
Top Bottom