John Heche atangaza rasmi kugombea jimbo la Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Heche atangaza rasmi kugombea jimbo la Tarime

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Aug 13, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  MWENYEKITI wa Baraza la Vijana (Bavicha) Taifa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Tarime mkoani Mara, mwaka 2015. Heche alisema kuwa, iwapo dhamira yake hiyo itapewa baraka na chama chake, kwa kupitisha jina lake, atahakikisha anapigania maendeleo makubwa ya wananchi wa Tarime, ikiwa ni pamoja na kuwanusuru na umasikini uliokithiri.

  Kada huyo aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika viwanja vya sokoni, Sirari, ambapo pamoja na mambo mengine, aliirushia kombora Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa imehindwa kutumia vizuri rasilimali za nchi kuleta maendeleo.


  Alisema, msukumo wa kutaka kugombea ubunge unatokana na uchungu alio nao wa kutaka kuweka chemichemi kubwa ya mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo, pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha wakazi wa Tarime na Watanzania wote. "Huu ni wakati wa ukombozi wa nchi hii. Maana Serikali hii ya CCM imeshindwa kabisa kuwasaidia wananchi wake!

  Rasilimali za kila aina, zipo hapa Tanzania, lakini zinawanufaisha watu wa nje ya nchi. "Kwa maana hiyo, mwaka 2015 kama Mungu ataniweka hai nitagombea ubunge Tarime. Kama chama changu kitanipitisha, nimejipanga vizuri kuhakikisha ninaleta mabadiliko ya kimaendeleo hapa," alisema Heche.


  Kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, mwenyekiti huyo alimshutumu Rais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kujenga uchumi wa ndani ya nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo, badala yake rasilimali hizo zinayanufaisha wageni.

  Alisema, licha ya kuwepo kwa madini ya almasi, dhahabu, makaa ya mawe, nyuklia, gesi na madini yanayotengeneza ndege na kompyuta, maziwa, bahari, mbuga za wanyama na milima mikubwa, watanznaia wanazidi kuteseka kwa umasikini wa kutupwa.

  "Tanzania ina kila aina ya madini, lakini umasikini ndiyo unazidi kuota mizizi na kuwatesa Watanzania. CHADEMA hatukubaliani na hali hii, tujiandaeni tuiondoe CCM kupitia sanduku la kura mwaka 2015," alisema Heche.

  Source: Tanzania Daima.


   
 2. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  atagombeaje ubunge 2015 wakati cdm kimebakiza miezi 10 kabla ya kukata roho
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  akili ndogo kuongoza akili kubwa ni mradi wa ccm liwalo na liwe ccm mnahaha hatuwaachii kamwe kama noma na iwe
   
 4. a

  andrews JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA ina network mpaka usalama wa taifa mkipanga saa 2 dakika kumi nyingi taarifa zote tunazo si mnaona mlimtuma shibuda kabla hajakaa tukajua sasa anahaha kamati kuu hatii mguu na mkeshe mkiwanga na nguvu za giza zinazodondosha mikutanoni viongozi wenu.
   
 5. m

  majebere JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Mbona mapema hivi? Tunangoja tuwasikie kina molemo wanamshambulia kama walivyo mshambulia Zitto. Hivi huyu Heche hakusikiliza maneno ya Mbowe?
   
 6. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,224
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Hivi Kamanda Mwita Mwikwabe na yeye sini wa huko huko Tarime au nachanganya ma-file?Mmh!Yetu macho tu ,kumbe posho wengi tunazipenda aisee!!
   
 7. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,441
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kusikia kama huyu, na wale wengine waliotangaza nia kwenye harambee ya M4C pale Serena kama nao wataitwa majina kama alivyoitwa Zitto.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kumbe kampeni zimeishaanza za kugombea ubunge na urais mbona Zitto Kabwe akisema anashambuliwa.
   
 9. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Dhana ya kusaidia mpaka uwe mjengon ni matapiko yasiyokuwa na tija...saidia hata kama haupo mjengoni...msaada wa kimawazo unatosha kuwakomboa hao unao waonea uchungu...
   
 10. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mbunge na mbunge msaidizi.
   
 11. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ama kweli nimeamini "muwikaji jogoo tu, akiwika bundi wanasema mchuro". Angekua Zitto Kabwe hapo watu wangemtungia hadi ngonjera za kumsema. Sasa kauli hii ia utofauti gani na ile ya Zitto?!
  Ifike hatua tujifunze kuwa fair.
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Urais na ubunge ni vitu viwili tofauti kabisa
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Utakufa wewe ukiache
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe. Na ninaamini Heche anafanya hivyo kwa sasa. Hata hivyo sio vibaya unapoona upungufu na unaweza kuupunguza basi ukaamua kuchukua hatua kwa kwenda mstari wa mbele!
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Ulimsikia Lema majuzi kwenye Star TV alisema anataka kumuachia Slaa, agombee ubunge Arusha halafu 2005 Slaa nae atamuachia Lema, halafu Slaa atagombea urais 2005 wanaachiana vijiti, hapo ndiyo hujue Chadema ina wenyewe hakuna chaguzi za kupitisha wagombea.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna watu wanaodhani ni wao tu ndio wamezaliwa wawe na madaraka? huu ni upuuzi mtupu, tumetoka kwenye uchaguzi mkuu juzi tu halafu leo bado kuna mtu anazungumzia uchaguzi wa 2015. Mpumbavu huyu.
   
 18. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Watu wamemuekea Heche maneno mdomoni, haya mmeyatoa wapi? katika mikutano yake yote anayoifanya hajatamka swala la kugombea, mfano mkutano wake 13-8 hapa muliba hajatamka hayo. CCM haya mnayatoa wapi?
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa hiyo unapingana na gazeti pendwa la Tanzania Daima au umetumwa.
   
 20. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jimbo hili ni la yule aliyekuwa rais wa daruso mwita. Na wewe heche vp acha tamaa dogo. Mi namwamini mwita mwikwabe.
   
Loading...