John Heche amtembelea Mabele Marando nyumbani kwake

John Heche amtembelea Mabele Marando nyumbani kwake

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,676
Reaction score
59,171
IMG-20251011-WA0012.jpg

Leo tarehe 11 Oktoba 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA John Heche amemtembelea nyumbani kwake aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Mabere Marando.

Ziara hii imebeba maana kubwa ya kuthamini mchango wa viongozi waliotangulia na kuendeleza mshikamano ndani ya chama.

Katika ziara hiyo, Heche aliambatana na Brenda Rupia ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Ntele Benjamin Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, pamoja na Aron Mashuve.
IMG-20251011-WA0011.jpg
 
Mzee Mabere Nyaucho Marando aandike kitabu kuhusu mapito yake yote.

Itasaidia sana kuelewe historia ya nchi yetu hii Tanzania .

TOKA MAKTABA :

15 April 2013

HAWA NDIYO MAGAIDI WA TANZANIA
kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa wa Machi 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Wilfred Lwakatare wa CHADEMA ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=SjZkNKkHAcs
Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani wakili mashuhuri Mh. Mabere Marando akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya CHADEMA jijini Dar es Salaam juu ya kikundi cha Magaidi kinachoua na kutesa watu nchini Tanzania... simu za David Msaki, Shah Ali, Swaumu, Mwigulu Nchemba, Ridhwani Kikwete, Emmanuel Nchimbi .. meseji zao .. kupangiwa nyumba ya kifahari ...

Jopo la mawakili Mabere Marando kama wakili mwandamizi , wakili Prof. Abdallah Safari, wakili Peter Kibatala, wakali Tundu Lissu watakuwemo katika jopo la kumtetea Lwakatare ambaye ni kurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ...
source : chadematv
 
View attachment 3487019

View attachment 3487018
Kumbe Heche anakazi maalumu huko! Nyumbu be informed!!
 
Nikimuangalia Mabere Marando naona kama kazeeka haraka.

Siku zinaenda aisee.
 
View attachment 3487019
Leo tarehe 11 Oktoba 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA John Heche amemtembelea nyumbani kwake aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Mabere Marando.

Ziara hii imebeba maana kubwa ya kuthamini mchango wa viongozi waliotangulia na kuendeleza mshikamano ndani ya chama.

Katika ziara hiyo, Heche aliambatana na Brenda Rupia ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Ntele Benjamin Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, pamoja na Aron Mashuve.
View attachment 3487018
Je amekumbuka kumbebea tone tone? Maana yeye na Lema walikusanya sana
 
TOKA MAKTABA :
Tuesday 23, April 2013

LWAKATARE, LUDOVICK JALADA LAO LAKABIDHIWA KWA DPP

Na Josephat Isango

WATEKAJI na watesaji wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka, na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, wanaendelea kuwa kitendawili baada ya Jeshi la Polisi kudai linaendelea na uchunguzi.

KIBANDA+2.JPG

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda na Madaktari Stephen Ulimboka

Wakata jeshi hilo likishindwa kuwatia mbaroni watesaji wa wanataaluma hao, limetamba kukamilisha uchunguzi wake kuhusu kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu, kwa waandishi wa habari jana, jalada hilo limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Licha ya matukio ya Ulimboka na Kibanda kutokea muda mrefu ikilinganishwa na lile la Lwakatare, Mungulu alishindwa kujibu maswali ya waandishi kuhusu suala ambalo linaonekana kupigwa danadana.

Dk. Ulimboka alitekwa na kuteswa vibaya kwa kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili na kung’olewa meno, kucha kisha kutelekezwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Juni 26, 2012.

Katika tukio linalofanana na hilo, Kibanda naye alivamiwa wakati akiingia nyumbani kwake na kupigwa kwa nondo kichwani, kutobolewa jicho la kushoto, kung’olewa kucha, meno mawili na kukatwa kidole.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na makao makuu limeunda timu za wataalamu kuchunguza matukio hayo lakini hadi leo zimekuwa zikipigwa danadana ya kuwakamata wahusika.

Katika mkutano wake na wanahabari, Mungulu aligusia matukio hayo kwa kifupi akisema uchunguzi bado unaendelea.

“Kuhusu kuvamiwa, kuteswa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk. Ulimboka, matukio yaliyotokea Zanzibar, uchunguzi bado unaendelea na uko katika hatua mbalimbali ambazo kwa sasa hakuna umuhimu wa kuziweka wazi kuepusha kuharibu upelelezi,” alisema.

Alipoulizwa ni kwa nini hawajamkamata mtuhumiwa mwingine zaidi ya yule aliyejisalimisha katika kitubio kanisani, Joshua Mulundi, Mungulu alikwepa akiwataka waandishi wasome nakala ya tamko la jeshi hilo.

Hata hivyo nakala hiyo iliyogawiwa haikusema chochote kuhusu tume hiyo kupata watuhumiwa wengine kwa kesi ya Dk.Ulimboka.

Tukio la Ulimboka ni kama jeshi la polisi limeinua mikono kwani Inspekta Mkuu wa Polisi (IGP), Said Mwema, aliwahi kusema mbele ya wakuu wenzake wa mataifa mbalimbali kuwa ni siri ya taifa.

Dk. Ulimboka mwenyewe baada ya matibabu yake nje ya nchi, hajawahi kuhojiwa na jeshi la polisi licha ya kukaririwa na vyombo vya habari akimtaja mtumishi moja aliyedai ni wa Ikulu akidai alihusika kumteka na kumtesa.

Wakati huo huo, Mungulu alisema kuwa upelelezi wa kumwagiwa tindikali kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha, katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga mkoani Tabora September 2011, upo katika hatua za mwisho.

Alisema ingawa watuhumiwa wawili tayari wamefikishwa mahakamani, endapo watapatikana wengine zaidi nao watafikishwa huko.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Mzee Mabere Nyaucho Marando aandike kitabu kuhusu mapito yake yote.

Itasaidia sana kuelewe historia ya nchi yetu hii Tanzania .

TOKA MAKTABA :

15 April 2013

HAWA NDIYO MAGAIDI WA TANZANIA
kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa wa Machi 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Wilfred Lwakatare wa CHADEMA ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=SjZkNKkHAcs
Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani wakili mashuhuri Mh. Mabere Marando akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya CHADEMA jijini Dar es Salaam juu ya kikundi cha Magaidi kinachoua na kutesa watu nchini Tanzania... simu za David Msaki, Shah Ali, Swaumu, Mwigulu Nchemba, Ridhwani Kikwete, Emmanuel Nchimbi .. meseji zao .. kupangiwa nyumba ya kifahari ...

Jopo la mawakili Mabere Marando kama wakili mwandamizi , wakili Prof. Abdallah Safari, wakili Peter Kibatala, wakali Tundu Lissu watakuwemo katika jopo la kumtetea Lwakatare ambaye ni kurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ...
source : chadematv

Magenge ya utekaji kumbe yalishamiri toka mwaka 2013 huko kwa watu wanaoikosoa serikali. Kikwete anatumia uwezo, uzoefu wake kumshauri Samia.
 
Back
Top Bottom