John Chiligati kupewa ukatibu Mkuu wa CCM?

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Jamani,

Nina mashaka huyu kutokuwepo kwenye baraza la mawaziri ... huenda akaula ukatibu mkuu wa CCM... kwa sababu kura zilizoelekea kutotosha za CCM ni dalili za Makamba kushindwa kazi.

Mimi nasubiri kuona yatakayojiri.
 
Nafasi yake ya uwaziri imechukuliwa na Lazaro Nyalandu, si unajua pia suala la kijiografia huzingatiwa kweney uteuzi wa mawaziri? Isitoshe alishawahi kunukuliwa akisema ameshindwa kuwa karibu na wapiga kura wake kutokana na majukumu mengi ya kichama. Huenda kweli akapewa ukatibu mkuu na Makamba ni muda wake wa kupumzika sasa. Naona hata Kikwete ameshaanza kumchoka. Statement yake (Makamba) ya kwamba mwanae asipoteuliwa kuwa waziri atashangaa naona ilimchukiza Kikwete na ameamua kumshangaza Makamba. Ngoja tusubiri tuone.
 
Ndugu zangu,
Kama mnavyofahamu, Mzee Chiligati ameachwa kwenye timu ya jk iliyotangazwa leo. Katika hali ya kawaida na kwa kutambua role ya babu huyu kwenye uhai wa chama chake, siyo rahisi kwamba Mzee huyu kaachwa solemba kwa sababu ya utendaji mbovu. Binafsi nahisi Mzee amekuwa reserved kwa ajili ya vyeo vya kichama mojawapo ikiwa ni kiti cha ukatibu mkuu wa ccm. Mzee makamba aliyetia fora kwa upayukaji na ulopokaji lazima atawekwa pembeni kwa sababu zilizo wazi.

Mnasemaje wakuu?
 
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…