John Chiligati kupewa ukatibu Mkuu wa CCM?

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,696
781
Jamani,

Nina mashaka huyu kutokuwepo kwenye baraza la mawaziri ... huenda akaula ukatibu mkuu wa CCM... kwa sababu kura zilizoelekea kutotosha za CCM ni dalili za Makamba kushindwa kazi.

Mimi nasubiri kuona yatakayojiri.
 
rmashauri

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
3,011
448
Nafasi yake ya uwaziri imechukuliwa na Lazaro Nyalandu, si unajua pia suala la kijiografia huzingatiwa kweney uteuzi wa mawaziri? Isitoshe alishawahi kunukuliwa akisema ameshindwa kuwa karibu na wapiga kura wake kutokana na majukumu mengi ya kichama. Huenda kweli akapewa ukatibu mkuu na Makamba ni muda wake wa kupumzika sasa. Naona hata Kikwete ameshaanza kumchoka. Statement yake (Makamba) ya kwamba mwanae asipoteuliwa kuwa waziri atashangaa naona ilimchukiza Kikwete na ameamua kumshangaza Makamba. Ngoja tusubiri tuone.
 
Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
398
Ndugu zangu,
Kama mnavyofahamu, Mzee Chiligati ameachwa kwenye timu ya jk iliyotangazwa leo. Katika hali ya kawaida na kwa kutambua role ya babu huyu kwenye uhai wa chama chake, siyo rahisi kwamba Mzee huyu kaachwa solemba kwa sababu ya utendaji mbovu. Binafsi nahisi Mzee amekuwa reserved kwa ajili ya vyeo vya kichama mojawapo ikiwa ni kiti cha ukatibu mkuu wa ccm. Mzee makamba aliyetia fora kwa upayukaji na ulopokaji lazima atawekwa pembeni kwa sababu zilizo wazi.

Mnasemaje wakuu?
 
Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
78
Ndugu zangu,
Kama mnavyofahamu, Mzee Chiligati ameachwa kwenye timu ya jk iliyotangazwa leo. Katika hali ya kawaida na kwa kutambua role ya babu huyu kwenye uhai wa chama chake, siyo rahisi kwamba Mzee huyu kaachwa solemba kwa sababu ya utendaji mbovu. Binafsi nahisi Mzee amekuwa reserved kwa ajili ya vyeo vya kichama mojawapo ikiwa ni kiti cha ukatibu mkuu wa ccm. Mzee makamba aliyetia fora kwa upayukaji na ulopokaji lazima atawekwa pembeni kwa sababu zilizo wazi.:target::painkiller::drum:
bora makamba mara milioni kuliko kipofu chiligati! mfano mzuri ni mtizamo wake kuhusu chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati jk analihutubia bunge! kwa kifupi ni mtu asiyejua hata maana ya demokrasia ni nini? kwake mfumo wa chama kimoja ni ajenda ya kudumu akilini mwake!:angry: ni utendaji mbovu uliopelekea kuachwa kwake kama sivyo ni nini? kwisha habari yake!
 
Ndugu yangu hivi unaifahamu ccm??? Viongozi mnaowaona ni 'fyatu' wenyewe ndiyo wanawataka. Nani alitegemea kama makamba angekuwa katibu mkuu. Ebu fikiria ccm ina wanachama wangapi wenye elimu kubwa, weledi na uzoefu wa hali ya juu lakini bado aliyeonekana anafaa alikuwa ni mlopokaji makamba.

Kwa hiyo, wewe unamwona chiligati si lolote si chochote lakini kwa ccm huyo ni lulu. Tusubiri tuone itakavyokuwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom