John Cheyo: UKAWA kuweni wakweli

John Cheyo: UKAWA kuweni wakweli

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia (TCD), John Cheyo amewataka wanasiasa wenzake wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wanashinikiza Bunge Maalumu la Katiba (BMK)liahirishwe, wawe wakweli.

Amesema kuwa Bunge hilo, haliendeshwi kwa amri za watu walioko barabarani. Pia, Cheyo amesema Rais hana mamlaka ya kusimamisha Bunge hilo; kwani linaendelea kisheria na litakoma Oktoba 4, mwaka huu.

Amesisitiza kuwa katika majadiliano yaliyokuwa yanafanywa kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Rais Jakaya Kikwete, waliafikiana mambo hayo na sio vinginevyo.

"Kama wanabisha, tumwombe Rais aruhusu majadiliano hayo yaoneshwe kwenye Kipindi Maalumu ili kila mtu aonekane mambo aliyokuwa anayasema kwenye kikao hicho…waungwana na sio kwenda kupotosha watu," alisema Cheyo wakati anatoa mchango wake bungeni mjini hapa jana.

Cheyo aliliambia Bunge hilo, kuwa hakuna makubaliano mengine katika mazungumzo hayo, zaidi ya yale ambayo aliyasoma mbele ya waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, likiwemo suala la BMK kuendelea na kazi zake ili kukamilisha kazi zake hadi Oktoba 4 mwaka huu.

Akionesha kuchukizwa na kitendo cha viongozi wenzake wa vyama kumruka Cheyo kuwa walikubaliana Bunge lisitishwe, Cheyo alisema kama Ukawa hawafurahishwi na hatua ya BMK kuendelea shauri yao, kwani sheria ndiyo inalipa haki Bunge hilo.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa wajumbe waliobaki ndani, watawapatia Watanzania Katiba nzuri yenye kujali maslahi ya wananchi, kama wakulima, wavuvi na wafugaji.

"Hapa tutaandika Katiba ambayo itapendekezwa kwa wananchi, kama mtu yuko nje na anakerwa sisi kuwepo hapa ndani shauri yake…naamini kuwa humu kuna bongo barabara za watu watakaowakabidhi Watanzania Katiba nzuri inayopendekezwa na Bunge," alisema mwanasiasa huyo.

Cheyo alisisitiza kuwa Katiba inayotungwa ni ya maridhiano na kwamba sio kundi kung'ang'ania upande wao, badala yake akasema pande zinatakiwa kutafuta vitu ambavyo wanaweza kukubaliana navyo na vitu ambavyo vinaweza hata kuwekwa pembeni kwa sasa, wakubaliane kwamba baadaye vikashughulikiwa kwa mazingira ya wakati huo.

Alisema hilo amejifunza wakati wanazungumza na Rais Kikwete juu ya mchakato wa Katiba na uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema Rais amekuwa mfano mzuri wa kusikilizana, licha ya kuwa halazimishwi kufanya hivyo na mtu yeyote, badala yake alijishusha akakaa na viongozi wa TCD na wale wanaojiita Ukawa.

Alisema kikao cha kwanza kilidumu kwa saa 4 na kikao cha pili kilidumu kwa saa zaidi ya nne. Alisema miongoni mwa makubaliano yao ni BMK ipate Katiba inayopendekezwa kwa wananchi na wakakubaliana kuwa kwa hali halisi ya muda uliopo haiwezekani mchakato huo ukamalizika kwa Katiba hiyo kupigiwa kura ya maoni na wananchi.

Cheyo alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutoahirisha uchaguzi wa mwakani, ambao wote hawakutaka jambo hilo lijitokeze. "Rais mwenyewe alikataa kuwa tusimtwishe mzigo wa kuahirisha uchaguzi huo na akasisitiza kuwa utaratibu uliopo, uendelee kuwepo na ndio maana tukakubaliana kuwa Bunge limalize kazi yake," alisema.

Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa Bunge hilo, haliendeshwi kwa amri za mtu aliyeko barabarani, bali linaendeshwa kwa sheria na sheria iliyopo ni GN 254 ambayo inasema Bunge lisitishe shughuli zake Oktoba 4.

"Itoshe mimi kusema yale niliyotangaza kwenye vyombo vya habari ndio makubaliano yetu, hakuna makubaliano mengine, ukisema sikusaini mazungumzo… jamani sio lazima kusaini kila kipengele, bali makubaliano ni matokeo ya mazungumzo na ndicho nilichofanya," alisema mwanasiasa huyo.

Aliwataka wabunge wajiamini kuwa Katiba itakayotolewa na waandishi, ndio itakuwa Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kwenda kupigiwa kura, hivyo wasisikilize kelele za watu walio nje ya Bunge hilo.

Cheyo alilazimika kutoa tamko hilo bungeni, kutokana na tamko walilolitoa viongozi wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kwamba hawakubaliani Bunge hilo liendelee, bali lisitishwe kwani kukubali liendelee ni kuvujisha fedha za walipa kodi.

TEC yawashangaa UKAWA.
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severine Niwemugizi, alisema Ukawa walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya kumtaka asitishe Bunge.

Alisema badala yake walitoka kwenye kikao hicho na kuanza kulalamikia wananchi huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.

"Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao chao, badala yake wameamua kuja kwa wananchi na kuanza kulalamika.

"Kwani katika hicho kikao hawakuwa na makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani?" alihoji.

Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa Rais ajaye atakubali kuendelea nao.

"Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa, kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa shughuli hizo, lakini baada ya hapo wanakuja kwa wananchi na kuanza kulalamika huku wakidai kuitisha maandamano, kwani hawakuwa na nafasi ya kumwambia rais malalamiko yao," alisema.


`Urais wa kupokezana ni hatari'
Katika hatua nyingine, Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi ameonya kuwa kuingiza kwenye Katiba urais wa kupokezana, kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, ni hatari kwa nchi, kwani kunaifanya nafasi ya rais ionekane kuwa ni ya kugawana madaraka kati ya pande mbili za Muungano.

Akichangia bungeni jana, Ngwilizi alisema hoja zinazotolewa na baadhi ya wajumbe kuwa Urais wa muungano uwe wa kupokezana kati ya Bara na Zanzibar, hazina tija kwani rais anayechaguliwa lazima awe amevuka ukereketwa wa Bara na Zanzibar, badala yake awe ni Mtanzania.

"Rais tunayemchagua ni wa Tanzania, sio wa upande mmoja wa muungano, hatutarajii rais aingie akiwa ni Mtanganyika na Mzanzibar, fikra za namna hiyo zinazidi kutugawa," alisema Jenerali Ngwilizi.

Alisema hata upande mmoja ukitoa rais kwa miaka 20 mfululizo, kwake anaona ni sawa ili mradi kiongozi anayechaguliwa, anafaa na ni Mtanzania halisi na sio vinginevyo. Alisema kwamba nchi ikimpata kiongozi bila kuwepo na mvutano wa upande gani ametoka rais huyo, hapo hakuna wasiwasi kwani kiongozi huyo ataongoza nchi kizalendo na kujiamini kuwa ni Mtanzania halisia.

Mwanasiasa huyo pia aliunga mkono kundi ambalo linataka kuwepo na makamu wawili wa Rais, kwa maelezo kuwa makamu wa kwanza awe ni Rais wa Zanzibar na makamu wa pili awe Waziri Mkuu wa Tanzania. Kwa upande wa Jeshi, Ngwilizi alisema Jeshi pekee la Wananchi lina sehemu tatu za Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), askari wastaafu ambao wanawajibika kupigana vita inapoingia na mgambo, ambao ni raia wa kujitolea.

Alisema kama kuna vyombo vingine ambavyo itaonekana ni muhimu kushiriki kwenye ulinzi wa nchi, Rais anayaandikia makundi mengine ambayo yamelelewa kwa nidhamu za kijeshi, kama polisi, magereza na KMKM.

"Makundi hayo hayashiriki vita hadi yaandikiwe barua na Amiri Jeshi Mkuu," alisema Ngwilizi. Alisema Katiba lazima itaje chombo cha ulinzi ambacho ni jeshi na alionya kuwa bila kufanya hivyo, Katiba itapoteza dhana ya Jeshi.

Alisema nchi nyingine zinaishangaa Tanzania kuwa ina majeshi mangapi, kutokana na kila kundi lenye nidhamu ya kijeshi kuitwa Jeshi wakati nchi inakuwa na jeshi moja tu.

Kingunge na Katiba ya kiuchumi.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuhakikisha kuwa Katiba wanayoiandika, inaisaidia nchi kujikomboa kiuchumi, badala ya kuandika Katiba yenye haki lukuki zinazowanufaisha kundi dogo la watu ambao ni wanasiasa na wafanyabiashara.

Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Bunge hilo, alisema jana kuwa haki zinazopigiwa kuwemo kwenye Katiba, nchi zote za Afrika zinazo lakini wanaofaidi haki hizo ni wenye nacho, huku wananchi masikini wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la umasikini.

Alitoa mfano kuwa haki ya kuishi, masikini ambaye hana uhakika wa chakula hiyo haki anafaidikaje nayo. Alionya kuwa bila kujenga Katiba ambayo inatambua harakati za kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia elimu, kilimo na viwanda, Katiba hiyo haitakuwa na lolote kwa mwananchi wa kawaida.

Alitoa mfano kuwa licha ya Tanzania kuwa na wahandisi lukuki, lakini wanatumika kukarabati vifaa vilivyotengenezwa na wahandisi wa nchi nyingine. Alisema suala hilo lisipoangaliwa, Watanzania wataendelea kuvaa na kutumia bidhaa zilizotengenezwa nje ya nchi.

"Nashangaa Watanzania tumeridhika kwa kuwa watu tunaokula makombo," alisema Kingunge na aliwataka wajumbe hao wadhamirie kuandika Katiba mpya, ambayo itaondoa na unyonge wa Watanzania kama zilivyofanya nchi za Asia.

Alisema Katiba mpya, lazima itambue kuwepo kwa matumizi ya sayansi na teknolojia, mambo ambayo alisema ndio pekee ambayo yanaweza kuleta ukombozi wa wanyonge wa Watanzania. Alisema kama uamuzi huo utakubaliwa, utakuwa ndio njia pekee ya kuendesha kilimo cha kisasa na ujenzi wa viwanda kwa kutumia maarifa ya watu wetu.

Katika mapendekezo yake aliyoyatoa kwa Bunge hilo, mkongwe huyo alitaka lengo kuu la Katiba, iwe kujenga uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea kwa kulifanya taifa lijikite kwenye mchakato wa kutumia maarifa ya kisasa, yaani sayansi na teknolojia katika nyanja zote za shughuli zake za kiuchumi na kijamii.

Chanzo: Habarileo
 
Waziri katika ofisi ya Rais asiyekuwa na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya alionya kuwa wajumbe walioko nje ya Bunge, ambao wanatarajia kuwa kuna katiba nyingine itaandikwa baada ya mwaka 2015, wamechelewa.
Alisema propaganda wanayoiendesha nje ya Bunge hilo kuwa mchakato huo utaanza upya, hauna tija. Aliwahakikishia wananchi kuwa wajumbe wa bunge hilo, wamefanya kazi kwa weledi mkubwa na watawapatia wananchi katiba mpya.
============================== ============================== ======

Hawa hapa chini ndiyo aina ya wanasiasa tulionao nchini!

Populist politics zitawamaliza!

A picture speaks a thousand words!

Tukisema baadhi yao walikuwa wamelewa juice waliyokunywa Ikulu Ndogo, Dodoma mpaka hawakufahamu hata kile walichokuwa wanakijadili na kukikubali tutakuwa hatukosei.

attachment.php

attachment.php

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika mwanvuli wa TCD wakiwa na furaha baada ya kumaliza kikao na Rais Kikwete

============================== ============================== ============

TAMKO la Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya makubaliano na Rais Kikwete kuhusu suala la Mchakato wa Katiba.

 
Last edited by a moderator:
Kweli, Momose CHEYO si mnafiki.

Siasa ndivyo zilivyo UKAWA wamevuka mstari na kufanya ya kwao wenyewe.
 
cheyo ni mnafiki tunataka katiba yenye maridhiano na si kuendelea na ujinga wnoufanya huko dodoma
 
cheyo ni mnafiki tunataka katiba yenye maridhiano na si kuendelea na ujinga wnoufanya huko dodoma
Ndugu,
Wewe unayefahamu maridhiano, naomba unielimishe angalau kwa kunitajia aina ya maridhiano unayoyasema na yanafanyika kati ya nani na nani katika mantiki na mazingira gani ya kisiasa.

By the way, unafiki wa Cheyo ni upi?
 
Mzee Cheyo hana Jipya ndio wale wale kundi la wamo wamo, alikuwa anataka hisani ni wa kupuuzwa kama wale wengine.
 
Mzee Cheyo hana Jipya ndio wale wale kundi la wamo wamo, alikuwa anataka hisani ni wa kupuuzwa kama wale wengine.
Ndugu,
Kama Mzee Cheyo hana jipya, basi ingekuwa vizuri ukatutajia ambaye ana jipya kuhusiana na kikao cha TCD na Rais Kikwete, hasa ikichukuliwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa TCD?
 
Hivi ni nani asiyejua kuwa Bwana Mapesa ni kuwadi na wakala wa Chama tawala (aka CCM B) miaka yote hii. Cheyo ni sawa na tembo (soma mpinzani) wa mabua na haijatokea hata siku moja kupigania haki kundi moja na wapinzania halisi.
Amekuwa akitumiwa na CCM miaka yote kugombania Urais kwa nia ya kuvuruga na kugawa matokea mpaka sasa amechuja na kujiona hafai (kwani hakumbea hata 2010) baada ya Watanzania kumstukia janja yake.

Anyway, Aluta Continua! Mapambano ya vita ya kudai haki sawa na ukombozi wa Mtanzania ndio kwanza inaendelea.
 
Hivi ni nani asiyejua kuwa Bwana Mapesa ni kuwadi na wakala wa Chama tawala (aka CCM B) miaka yote hii. Cheyo ni sawa na tembo (soma mpinzani) wa mabua na haijatokea hata siku moja kupigania haki kundi moja na wapinzania halisi.
Amekuwa akitumiwa na CCM miaka yote kugombania Urais kwa nia ya kuvuruga na kugawa matokea mpaka sasa amechuja na kujiona hafai (kwani hakumbea hata 2010) baada ya Watanzania kumstukia janja yake.

Anyway, Aluta Continua! Mapambano ya vita ya kudai haki sawa na ukombozi wa Mtanzania ndio kwanza inaendelea.
Mkuu, usitake kupotosha. Kama viongozi wa upinzani wanajua kuwa Bwana Mapesa ni kuwadi wa CCM, iliwezekana vipi wakamchagua kuwa Mwenyekiti wa TCD?
 
Ndugu,
Kama Mzee Cheyo hana jipya, basi ingekuwa vizuri ukatutajia ambaye ana jipya kuhusiana na kikao cha TCD na Rais Kikwete, hasa ikichukuliwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa TCD?
Mkuu MwanaDiwani, hawa wameshikwa pabaya. Wanaona kuwa malengo yao hayajafanikiwa na wengine wana hasira za kukosa posho za bunge kutokana na ujinga wa viongozi wao. Maskini mtu kama Julius Mtatiro. Namhurumia sana. Kweli nakubali msemo wa kiswahili kuwa "Maskini Jeuri"
 
Hivi ni nani asiyejua kuwa Bwana Mapesa ni kuwadi na wakala wa Chama tawala (aka CCM B) miaka yote hii. Cheyo ni sawa na tembo (soma mpinzani) wa mabua na haijatokea hata siku moja kupigania haki kundi moja na wapinzania halisi.
Amekuwa akitumiwa na CCM miaka yote kugombania Urais kwa nia ya kuvuruga na kugawa matokea mpaka sasa amechuja na kujiona hafai (kwani hakumbea hata 2010) baada ya Watanzania kumstukia janja yake.Anyway, Aluta Continua! Mapambano ya vita ya kudai haki sawa na ukombozi wa Mtanzania ndio kwanza inaendelea.

Mkuu, usitake kupotosha. Kama viongozi wa upinzani wanajua kuwa Bwana Mapesa ni kuwadi wa CCM, iliwezekana vipi wakamchagua kuwa Mwenyekiti wa TCD?

Ukitaka kujua rafu ya siasa ni pale spika Makinda alipokuwa akijaribu kukiuka kanuni ile 2010 ili kumchomekea Hamadi Rashidi Mohamed kuendelea na wadhifa wa Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Na wakati huo CDM ndio iliyobuka na wabunge wengi zaidi kuliko hata CUF.

Na alijaribu kuhamasisha hata kura ili kutumia wingi wa CCM bungeni kupitisha ajenda hiyo wakati kanuni zilikuwa wazi kuwa Mkuu wa kambi ya upinzani ni Chama cha upinzani chenye wabunge wengi zaidi baada ya kile ambacho ni majority. Je utasema spika alikuwa anang'ang'ana kwa kuwa alikuwa hajui kanuni za bunge? Na nimekupa mfano mdogo tu.

Anyway, mwisho kukujibu swali lako la msingi mkuu ni kuwa Uwenyekiti wa TCD ni 'rotational'. Ni wa kupokezana vijiti kwa kila chama cha upinzani na hata vile visivyo na wabunge wanapata staili ya uwenyekiti huu ifikapo zamu yao..
 
Nimeyapenda maneno ya Mzee kingunge ,nakumbuka maneno kama haya aliyasema kwenye kongamano Fulani pale morogoro,ukumbi wa usambara lodge
Ni maneno mazuri na yenye tija kwa taifa
 
John Cheyo anaweweseka, hajui anachokisema, anaongozwa kwa hisia tu. hakuna mahala, katika matamshi yao kwa waandishi wa habari, viongozi wa Ukawa (Mbatia, Lipumba na dr Slaa) walitamka kuwa kusitisha BMK haikuwa miongoni mwa makubaliano kati ya JK na TCD.

Hakika kusitisha Bunge hakukuwa miongoni mwa makubaliano. lakini hawa Ukawa wanachokisema, wakiungwa mkono na vyombo vya habari, wasomi na wananchi wengine ni kwamba kutokana na hayo mengine waliyokubaliana, BMK sasa linafanya majadiliano yasiyokuwa na manufaa kwa nchi, na ni bora lisimamishwe kuliko kupoteza fedha za umma!

Hicho ndicho viongozi wa ukawa walichokisema.
 
Dodoma. Mwenyekiti wa Taasisi ya Demokrasia
Tanzania (TCD), John Cheyo amewavaa viongozi
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
akieleza kuwa walichokubaliana katika kikao chao
na Rais Jakaya Kikwete ni kwamba Bunge
liahirishwe Oktoba 4 na si kama wanavyodai wakiwa nje.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Cheyo
alisema hakuna makubaliano ya kutaka Bunge
lisitishwe kabla ya kukamilisha kazi zake Oktoba
4, ikiwamo kutoa Katiba itakayopendekezwa kwa
wananchi. “Mojawapo tulilokubaliana ni Bunge hili lipate
Katiba itayopendekezwa kwa wananchi,” alisema
Cheyo huku akipigiwa makofi na kelele kutoka
kwa baadhi ya wajumbe. “Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda
tulionao, haiwezekani mchakato mzima
ukamalizika na maana ya kumalizika mchakato ni
kura ya maoni ya wananchi na ndiyo wenye
Katiba.” “Tukasema kama inabidi tufike mpaka kule (kura
ya maoni) inatubidi tuahirishe uchaguzi wa 2015
jambo ambalo sisi wote hatuliafiki na mheshimiwa
Rais alisema msinitwishe mzigo huu,” alisisitiza
Cheyo.

Cheyo alisema Rais katika mazungumzo hayo
alitaka utaratibu wa kufanya uchaguzi kila Oktoba
ya mwisho wa kipindi cha miaka mitano uendelee
ili wananchi wenyewe watoe ridhaa kupitia
uchaguzi wa viongozi. “Bunge hili haliendeshwi kwa amri ya mtu ambaye
yuko barabarani. Bunge hili linaendeshwa kwa
mujibu wa Sheria na sheria tuliyokuwa nayo kwa
sasa ni GN 254 (tangazo la Serikali) ambayo
inasema uhai wa Bunge ni mpaka Oktoba
4,”alisema Cheyo.

Cheyo alisema haiwezekani Rais akasimama mara
baada ya makubaliano na kutangaza kuwa siku
inayofuata Bunge lisitishe shughuli zake. “Watu tumekubaliana na kuna video ambayo kila mmoja aliyekuwa akizungumza alirekodiwa. Kweli mnataka
tumuombe sasa mheshimiwa Rais tutengenezewe kipindi maalumu kila mmoja aonekane anasema nini?”
alihoji. “Tuwe waungwana. Itoshe mimi kusema yale niliyotangaza hayo ndiyo makubaliano.
 
Bila UKAWA - CCM wangetutungia katiba nyingine mbovu zaidi - Hongera sana Mbowe, Mbatia na Prof. Lipumba kukaa meza moja kuliokoa taifa.
 
Back
Top Bottom