John Boko apumzishwe sasa

Boko ni simba simba ni Boko bila Boko hatutoboi sisi kama mashibiki tunamuelewa sana boko
 
Huwa anawasaidia sana kwenye yale magoli ya offside. Hivyo mnatakiwa kumvumila.
 
Kama ni uganga basi huyu mwamba mganga wake hatari, ukitizama work rate yake, unyumbulifu yaani jamaa anaonekana kachoka haswaa, one vs one battle anashindwa sana.

Kila mwenye macho anaona mwenyewe.
Bocco na kocha wake wanatuchelewesha sana.

Mechi na Singida tungepata matokeo ya maana MAPEMA km tungeanza na kina Phiri, Baleke , Chilunda ambao hawachezeshwi.
 
Kama ni uganga basi huyu mwamba mganga wake hatari, ukitizama work rate yake, unyumbulifu yaani jamaa anaonekana kachoka haswaa, one vs one battle anashindwa sana.

Kila mwenye macho anaona mwenyewe.
nilikuwa namdharau tangu apigwe kidole na juma nyoso na hakurudisha hata ngumi. ila kwa michezo ya hivi karibuni kila akiingia huwa anawasaidia simba kushinda na analeta mabadiliko. nadhani bado ana muda wa kucheza.
 
Kama ni uganga basi huyu mwamba mganga wake hatari, ukitizama work rate yake, unyumbulifu yaani jamaa anaonekana kachoka haswaa, one vs one battle anashindwa sana.

Kila mwenye macho anaona mwenyewe.
Duh ndio chaguo la kocha
 
Kosa sio lake walaumiwe viongozi waliomungozea mkataba na benchi la ufundi linalompa muda mwingi wa kucheza wakati kuna vijana wa kufanya hivyo. Tatizo la benchi la ufundi wakiona tu kaufunga mechi moja basi mechi ijayo atapangwa mwanzo mwisho wala hawaangalii idadi ya nafasi anazopoteza na hata mipira inayoharibika miguuni kwake.

Kama Simba ingekuwa na benchi la ufundi lenye weledi basi Boko angekuwa anacheza si zaidi ya dakika 30 kwa mechi moja ili akupe ufanisi. Boko akili inataka mwili unagoma.
 
Akizungumza na Mwanaspoti jana,
kocha Robertinho alisema ameiona
hali ya mashabiki wa klabu hiyo
kutomkubali Bocco, ila kwa
mtazamo wake bado ni
mshambuliaji bora anayeweza
kucheza kwa maelekezo na
kuisaidia timu, hivyo hawezi
kumuacha nje kizembe.
Mbrazili huyo alisema Bocco pekee
amekuwa akifanikiwa kucheza kwa
maelekezo yake kwa kutumia muda
mwingi kukaa ndani ya eneo la
wapinzani faida ambayo imewapa
nafasi ya timu hiyo kufunga mabao.
"Sikiliza, ni kweli naiona hiyo hali,
mashabiki waje uwanjani kuangalia
Simba inacheza mpira vizuri.
Kwangu Bocco bado ni
mshambuliaji mzuri kwani
anakwenda kufanya kile
ninachokitaka afanye,” alisema
Robertinho na kuongeza;

"Hata katika mechi dhidi ya
Dynamos (Power) aliingia akafanya
nilichotaka tukapata bao lililosaidia
kutuvusha makundi na leo (juzi)
nimempa nafasi ya kuanza
amefunga tena, lakini akawafanya
mabeki wa Prisons kwa muda
mwingi kubaki nyuma, nataka
mshambuliaji wa aina hii anayekaa
muda mrefu eneo la hatari la
wapinzani na hili ndicho anafanya
Bocco huyu bado ni bora kwangu.”
Kocha huyo alisema anao
washambuliaji wengine kama Jean
Baleke na Moses Phiri ambao nao ni
wazuri kwa kukimbia pembeni
lakini wamekuwa hawajaweza
kucheza kwa nidhamu kama
anavyofanya Bocco.
"Nimezungumza na Bocco
nimemwambia aachane na mambo
ya mashabiki anisikilize mimi kama
kocha wake, mashabiki wanataka
ushindi hesabu zetu ndio
zitakazowapa furaha, unaona
amefunga wamenyamaza nataka
aendelee kufanya hivyo hivyo kila
mara kwani nitaendelea kumtumia,”
alisisitiza Robertinho aliyefikisha
jumla ya mechi 15 bila kupoteza
katika Ligi Kuu Bara.
 
Bocco na kocha wake wanatuchelewesha sana.

Mechi na Singida tungepata matokeo ya maana MAPEMA km tungeanza na kina Phiri, Baleke , Chilunda ambao hawachezeshwi.
Illusions tu hizo. Mbona huwa wanaanza na magoli hayapatikani?
 
Boko inatakiwa aingie dakika angalau 15 za mwisho Kama alivyofanya siku ya mechi na Power Dynamo.

Kuna wachezaji vijana Kama Chilunda. Muhammedi Musa, Muhammedi Kazi, Mwenda nk, wanatakiwa kuwezeshwa na kupewa nafasi za kuanza.

Kipa bado ni tatizo Simba. Sijui kiwango cha kipa Abeli ila anaonekana kuwa na kitu Kama ataaminiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom