Jogoo wa Kichina ataga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,246
33,007
Jogoo wa Kichina ataga

6245758.jpg

Moja ya majogoo ya Kichina

Shirika la habari la egynews limeripoti kuwa, Wasomi na wataalamu nchini China wamepatwa na kiwewe cha mwaka, pale waliposhuhudia Jogoo lisilo la kawaida, ambalo linameshataga mayai kumi na manne 14.

Wasomi hao wameshaanza utafiti wa kina ili kujua imekuwaje na ina athari gani? Televisheni ya China imesema kuwa, tukio la kutaga kwa Jogoo limezua gumzo kubwa katika mitaa ya Uchina. Baadhi ya Wachina wanaenda katika shamba liliopo mji wa Shandong Liaoche anapofugwa jogoo huyo ili kumshuhudia na maajabu yake.

Jogoo huyo ana kilo tatu 3 na ameanza kutaga tangu zamani, na yai lake la mwisho ni tarehe 7/2/2012. Na yai la jogoo huyo ni kubwa kuliko yai la kawaida.

Wakati huo huo duru za kiusalama wa chakula huko China zinaripoti kuwa, maafisa wa afya wanachunguza matukio yanayojulikana katika vyombo vya habari kama (YAI MPIRA), ambapo kiini cha yai kikichemshwa kinakuwa kama vigoroli vya mpira na kuvutika vutika.

<tbody>
</tbody>
 
Hii sio ajabu. Majogoo huwa wanataga lakini viyai vidogo na sio mara kwa mara na hutokea kwa wale walikomaa sana. Sisi tnaofuga Kuku wa kienyeji huku vijijini sio jambo la kushangaza. Ingekuwa kuna ofisi ya JF ningeweza kuleta yai na Jogoo siku ingetokea lakini hata ukiwauliza wazee wa vijijini watakueleza kwamba hiyo sio ajabu lakini sio kwa wingi huo wa mayai 14.
 
Tokapa. Ndo madhara ya kusoma HKL.
 
jogooo uwa anataga ila yai lake linakuwaga dogo sana na siyo mara kwa mara ni mara chache sana.
 
Hii sio ajabu. Majogoo huwa wanataga lakini viyai vidogo na sio mara kwa mara na hutokea kwa wale walikomaa sana. Sisi tnaofuga Kuku wa kienyeji huku vijijini sio jambo la kushangaza. Ingekuwa kuna ofisi ya JF ningeweza kuleta yai na Jogoo siku ingetokea lakini hata ukiwauliza wazee wa vijijini watakueleza kwamba hiyo sio ajabu lakini sio kwa wingi huo wa mayai 14.
Ni kweli hata mimi nilishahi kushuhudia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom