Saana tu mkuu hiyo picha inatufundisha sana... Tena ujumbe huu kwa sasa ni mahususi kwa wale wanaowaua tembo kwa unyama na ukatili wa hali ya juu ili wapate pembe za ndovu. Wao pia nawalinganisha na Pazi sema kwa stage nyingine tofauti! Wao ukatili wao umekaa kibepari sana na hawatosheki na kile walichonacho. Pia wana umimi sana manake kwao kujilimbikizia hela na mali kwa gharama yoyote ile kwao sio tabu hata kama itagharimu maisha ya binadamu wenzao ni bora ilimradi wapate wanachokitaka. Ndio maana walipoona ndovu zinathamani wameamua kuwachinja watakavyowao ili tu waendelee kujilimbikizia mali.
Nadhani watu kama hawa walikuwa na tabia kama ya Pazi toka wakiwa wadogo na pengine wazazi/ walezi wao waliliona jambo hilo wakakemewa na hawakusikia inawezekana pia wengine hawakukemewa kabisa!
Wito wangu kwa wazazi na walezi tujifunze kukomesha tabia za watoto wetu ambazo tunaziona hazipendezi na pia haziwasaidii mapema kabla hawajaja kuwa Pazi wakubwa (mafisadi, makatili, majambazi, n.k). This is simply because I believe that Charity begins at Home!