Job Ndugai - Tembo ukilisifia huwa maji

Meander

Member
Nov 2, 2010
62
18
Nasikitika kuona Mh. Naibu Spika Job Ndugai anavyobadilika kwa kasi sana katika usimimazi wa Bunge. Mh.Job alikuwa ni mwanasiasa niliyekuwa namheshimu na kumkubali katika wanasiasa toka chama tawala.

Kwa sasa napata mashaka kutokana na mwenendo wake. Imenishangangaza sana jinsi alivyocomment baada ya Tundu Lissu kutoa maelezo ya kikanuni kuhusu mwongozo alioomba Mh. Ole Sendeka dhidi ya hoja ya Mh.Zito Kabwe kuhusu vigogo walioficha mabilioni kule Uswis. Nimemsikia Mh.Job akimjibu Lissu 'na wewe sijui nani kakupa ruhusa ya kufundisha' . Sasa naona kuwa Mh.Job na baadhi ya wabunge CCM wanatumia nguvu sana katika kuhandle hoja za Mh. Lissu
 
Nadhani heshima yako ulikuwa unampa mtu asiyestahili,ukweli ni kwamba Job Ndugai yupo kigambagamba
zaidi.magamba yote ndo yalivyo hakuna anyestahili kuaminiwa.
 
Yaani ni hivi ukimsikia tu Speaker anamtaja Tundu Lisu kama mchangiaji anayefuatia au kaomba mwongozo ujue hata wale wanaopenda kulala usingizi huwa unawafyatuka! Eeh ndiyo! He is always well detailed na hapo huwa anakuja na summary tu shauri ya muda sijui itakuwaje akipata saa zima!
 
Nasikitika kuona Mh. Naibu Spika Job Ndugai anavyobadilika kwa kasi sana katika usimimazi wa Bunge. Mh.Job alikuwa ni mwanasiasa niliyekuwa namheshimu na kumkubali katika wanasiasa toka chama tawala.

Kwa sasa napata mashaka kutokana na mwenendo wake. Imenishangangaza sana jinsi alivyocomment baada ya Tundu Lissu kutoa maelezo ya kikanuni kuhusu mwongozo alioomba Mh. Ole Sendeka dhidi ya hoja ya Mh.Zito Kabwe kuhusu vigogo walioficha mabilioni kule Uswis. Nimemsikia Mh.Job akimjibu Lissu 'na wewe sijui nani kakupa ruhusa ya kufundisha' . Sasa naona kuwa Mh.Job na baadhi ya wabunge CCM wanatumia nguvu sana katika kuhandle hoja za Mh. Lissu

Mi nakushangaa ulimheshimu kwa kipi zaidi to begin with.
 
Katika bunge la 2010-2015, hakuna kiongozi makini wa bunge kama dada yetu Jenista Mhagama.
 
exactly......
huyu jamaa ni ovyo right from the start
sasa lini alistahili kuchukuliwa serious?

Watu wanapenda sana kuishi kwenye fantasyland. Akija mwanamazingaombwe yeyote anayejua kusema "abracadabra" wanaona "this must be the second coming of the messiah".

By the time wanaamka na kuona real world inawasubiri pale pale walipoiacha, mazingaombwe yale yale, cheapo,wanakuwa disappointed.
 
Watu wanapenda sana kuishi kwenye fantasyland.

By the time wanaamka na kuona real world inawasubiri pale pale walipoiacha, wanakuwa disappointed.
Kiranga,

..Ndugai aliniacha hoi alivyokwenda kwenye kipindi cha TV kulumbana na mwenyekiti wa CDM, Freeman Mbowe.

..mhuni mwingine huko bungeni ni Katibu wa Bunge, anaitwa Dr.Kashilila. yeye kila siku ni kuwarushia vijembe wabunge wa upinzani.

..bunge la awamu hii kwa kweli viroja vitupu. nina wasiwasi ipo siku watatiana ngeu humo bungeni.
 
Last edited by a moderator:
Tundu Lissu anapingwa na wengi sana....kila mtu bungeni huwa hataki kuukubali ukweli....rejea bunge la kujadili mswada wa katiba mpya...kila aliekuwa akisimama anaunga mkono hoja halafu anaanza kumchambua Lissu mpaka muda unaisha.
Sasa hivi yuko kwenye kamati ya maadili anamwaga sumu....mpaka kitaeleweka tu mbona!
 
Kiranga,

..Ndugai aliniacha hoi alivyokwenda kwenye kipindi cha TV kulumbana na mwenyekiti wa CDM, Freeman Mbowe.

..mhuni mwingine huko bungeni ni Katibu wa Bunge, anaitwa Dr.Kashilila. yeye kila siku ni kuwarushia vijembe wabunge wa upinzani.

..bunge la awamu hii kwa kweli viroja vitupu. nina wasiwasi ipo siku watatiana ngeu humo bungeni.

Ebwana kumbe uliidaka ile ya kulumbana na wewe?

Mie nikaona aibu vibaya sana kwa sababu mtu yeyote anayejua heshima ya ofisi ya Spika ule mjadala hata asingeenda hata kama mtazamaji tu, maana rabsha zinaweza kumrukia bila kutaka hata kama kakaa backbench huko.

Ndo nashangaa watu wanakuja kushtuka leo kwamba huyu jamaa bomu?
 
Ndugai,bi kiroboto na yule sijui mabumba ni mijitu ya ajabu sana,afadhali "kidogo" na Mhagama
 
Hata mimi sikuelewa ile kauli ya Ndugai kudai kuwa kiti hakiwezi kufundishwa. Hii ina maana kiti cha spika/naibu wake ni malaika na hawawezi kukosea/kupotoka/kukiuka taratibu zozote katika bunge! Katiba ijayo ije na Mihimili minne, wakome ubishi!
 
Ndugai,bi kiroboto na yule sijui mabumba ni mijitu ya ajabu sana,afadhali "kidogo" na Mhagama

hata kama wangekuja wazuri kama keki ya kula, tatizo litabakia palepale.hakuna kanuni ambazo ziko wazi kukuwajibisha meza ya spika.na pia hata kama zikiwepo, bado wingi wa wabunge wa ccm watakataa tu.Ni kwamba huu ni mkakati wa ccm kudhibiti upinzani kwa namna yeyote ile.Kwa kutumia bunge, serikali, vyombo vya dola , vyombo vya ulinzi, mahakama.Ni hatari sana kupigana na mtu nayekaribia kufa, anaweza kukuua , sababu anakua hana cha kupoteza na hana huruma wa soni ya kiutu.CCM kwa sasa imepoteza dira na haina kiongozi mweledi
 
Back
Top Bottom