JKT kuanzishwa upya

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa Serikali inakamilisha mipango ya kuanzisha upya utaratibu wa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria kama ilivyokuwa zamani.

Pia alisema kuwa Tanzania iko tayari kutoa uzoefu wake wa jinsi ya kuendesha Jeshi la Kujenga Taifa kwa Zimbabwe ambayo nayo inaangalia jinsi ya kuanzisha jeshi kama hilo kwa ajili ya vijana.

Rais Kikwete alisema hayo juzi Ikulu, Dar es Salaam alipofanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Zimbabwe, Jenerali Costantine G. Chiwenga ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi Tanzania.

Katika mazungumzo hayo, Jenerali Chiwenga alimweleza Rais Kikwete kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi ya Zimbabwe ikiwa ni pamoja na mchakato wa maandalizi ya katiba mpya ya nchi hiyo ambayo inafungua mlango wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwingine nchini humo.

Jenerali Chiwenga ambaye alifuatana na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, pia alitumia mazungumzo hayo na Rais Kikwete kuishukuru tena Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika mapambano ya ukombozi wa Zimbabwe. “Tuko nanyi.

Tanzania iko na wananchi wa Zimbabwe. Huu ni uhusiano wa kihistoria ulioanzia kwenye makambi ya wapigania Uhuru ya Kongwa na Nachingwea hadi kwenye misitu ya Mozambique mpaka ndani ya Zimbabwe yenyewe,” alisema.
 
Kwa maneno ishaanzishwa vitendo ndo kazi labda baada ya miaka 100
 
Uongo mtupu, wana kamilisha mpango gani kila siku wanakamilisha mpango? Hakuna hata pesa ya kula halafu waanzishe kwa pesa gani? watu wengine bhana, kwani ukikaa kimya si tutajua tu kuwa upo pia hadi uongee? enzi hizi sio za kuanzisha JKT watajimaliza, huwezi kwenda kuwafundisha watu jinsi ya kutumia silaha, kuwajengea ujasiri wa kile wanachokiamini kisha wakirudi mtani hakuna ajira weee, watakua moto wa kuotea mbali kuliko hata vibaka wenyewe, hapatatosha, haya wapelekeni muone mwisho wenu unavyokuja fasta
 
wameshindwa kulipia wanafunzi chuo
itawezekanaje hii kitu?

na kizazi cha siku hizi ni cha kijasiriamali wataoenda wachache!
 
Back
Top Bottom