JK ziarani Uswisi

JK ziarani Uswisi

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
Amewasili Zurich akiambatana na Waziri Maghembe, Mwakyembe na Chiza.

Lengo ni kushiriki mkutano wa World Economic Forum.
 
overtime jamaa analipwa sh ngapi ????

akitoka nje ya nchi sh ngapi kwa siku??

akiwa nje ya ofisi ndani ya nchi analipwa sh ngapi kwa siku????

daaaa mwenyewe rais na wasaidizi wake wakija kumaliza muda mwaka 2015 watakuwa matajiri wa kutisha

halafu msiwasingizie kuwa walikuwa wezi ila jueni kuwa hizi safari wanapata marupurupu yalio kubuhu.
 
Tulizani tumempata Rais...kumbe tumepata Ndege John....huyu kiguu na njia anapaa sana angani...hivi wasaidizi wake wapo likizo...?
Makamu wa Rais Bilal bado anatembea na mikasi mfukoni hapewi airtime ya kupaa hata kidogo....kazi tunayo
 
Akitaka aunganishe na nchi zingine na ikiwezekana asirudi aendelee kuzurura tu!

Huyu mtu mzururaji mno!
 
Maghembe yupo kwenye list ya mawaziri mizigo kama sikosei. mwache na yeye akajipongeze baada ya kupewa chance nyingine.
 
Ni muda muafaka kwa CHADEMA kuangalia namna ya kufanya Maandamano kupinga safari za rais zisizo na mashiko wala ukomo. Watanzania waliopo vijijini wanahitaji rais awatembelee ilia atatue matatizo yao lakini kinachotokea ni kinyume chake. Hii inabidi idhibitiwe kwenye katiba mpya.
 
Huyu rais wetu inaelekea alivyokuwa mdogo alikuwa anakula sana miguu ya kuku sijawahi ona mtu anaruka na ndege km huyu tulidhani tumepata kumbe tumepatikana.
 
Huyu rais wetu inaelekea alivyokuwa mdogo alikuwa anakula sana miguu ya kuku sijawahi ona mtu anaruka na ndege km huyu tulidhani tumepata kumbe tumepatikana.
Mkuu, hebu nikuulize swali. Mara ngapi unashinda nyumbani kwako siku zote nyakati za mchana?
 
Ni muda muafaka kwa CHADEMA kuangalia namna ya kufanya Maandamano kupinga safari za rais zisizo na mashiko wala ukomo. Watanzania waliopo vijijini wanahitaji rais awatembelee ilia atatue matatizo yao lakini kinachotokea ni kinyume chake. Hii inabidi idhibitiwe kwenye katiba mpya.
Duh! Badala ya kupinga kitendo cha Freeman Mbowe kula fedha za ruzuku na Joyce Mukya, nyie mnaandamana katika masuala yasiyo ya msingi
 
Back
Top Bottom