JK - Umelikoroga utalinywa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK - Umelikoroga utalinywa!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bill, May 6, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hakika vita ya ufisadi inayochukua mkondo tofauti kwa sasa inadhihirisha kushindwa kutawala kwa JK na chama chake.

  Dhambi ya ubaguzi aliyoianzisha JK na washirika wake Rostam na Lowassa hakika itawatafuna wao wenyewe, Chama Chao na Taifa kwa ujumla.

  Mwalimu Nyerere alisema hamuwezi kuanzisha dhambi mbaya hii mkabaki salama. Walimbagua Salim A. S mpaka akajuta ni kwa nini alichukua fomu. Sumaye naye hakuachwa hadi akasema mtu anayetumia Magazeti kuchafua wenzake akipata madaraka atatumia mtutu wa Bunduki. Ndicho kitu tunachokisubiri kwa sasa japo kilianza kipindi cha CHACHA WANGWE pale mafisadi walipoligongesha gari lake ili kuivuruga Chadema. Ukiangalia mwendelezo wa sasa hakika utajua walengwa wakuu walikuwa ni Chadema na Mengi kwani Mtikila akitumikia adhabu ya kulipia Vijisenti alivyopewa na ROSTAM aliyapayuka haya kabla hajanyamazishwa na jiwe la kichwa.

  Hali ya kukosekana kwa utengamano wa kisiasa nchini ni mwendelezo wa dhambi ile iliyoasisiwa na JK pamoja na washirika wake Rostam na Lowassa na asitegemee kuwa itakuja kutulia. Anachotakiwa tu kukifanya ni kulinywa kwa namna ileile alivyolikoroga.

  CCM haiwezi kubaki salama chini ya JK asiyeweza kukemea uozo ndani ya Chama, mbaya zaidi nchi yetu inapitia kipindi kigumu kiasi cha kutishia mustakabali wake, kisa ukosefu wa uongozi imara na kupotea kwa uzalendo.

  Hakika JK utalinywa kwa jinsi ulivyolikorogwa
   
Loading...