JK sio rais makini

cj21125

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
3,588
Reaction score
3,521
Udhaifu wake uko wazi kuanzia anapomteua waziri mkuu pamoja na baraza la mawaziri. Yani hajifunzi chochote kutokana na makosa ya huko nyuma? Kule kulikuwa na EPA mara akaingia RICHMOND akang'oka mwenye nywele nyeupe ingawa sio mzee, kisha OPERATION TOKOMEZA UJANGILI wakang'oka watu 3, sasa ESCROW huyo tena ni baba lao. Yani ina maana hakuna hata jambo moja JK alilojifunza kutoka kwenye EPA-----RICHMOND----OPERATION TOKOMEZA na sasa ESCROW? Angekuwa makini angekuwa ameshajifunza jambo ili kuzuia ESCROW. Je; huyu ni rais au ni dalali wa mafisadi?
 
ukweli ni kwamba JK yupo strong kiasi ambacho kila anayeharibu anabeba mzigo wake. na kwa sababu mitanzania mmezoea kuiba na hasa nyie mnaojiita wasomi (uchwara) dawa yenu nikuwaacha muumbuke tu kwenye jamii. kama utakumbuka mkapa alilia sana na prof simon mbilinyi baada ya wabunge kumshikia bango. ilifikia kipindi akaanza hata kuwatishia wanaccm wenzake kuwa hatawapitisha kwenye ubunge tena wakati wakuteuliwa.
big up Kikwete for this. hutaki, acha.


 
atajifunza saa ngapi wakati kila kukicha ni kigulu na njia ughaibuni utafikiri yeye ni waziri wa mambo ya nje wa marekani... sijui sasa zimefinga siku ngapi kwa ile safari counter humu JF , mara ya mwisho niliona siku 365 alizo safari au kukaa nje ya Tanzania.. kila anaporudi ni deal nyingine behind his back.. labda hawa mafisadi wanampangiaga hizi safari ili watakatishe fedha na kupanga au kutayarisha na kutakatisha madeal yao huko mkombozi bank...
 
Namwonea huruma sana jk, maana akitoka ikulu kuanzia mwakani hatasaulika kabisa na pengine makashfa yote yataibuliwa kivingine na wananchi na hata mahasimu wake kisiasa!
 
Hili lilijulikana miaka mingi, hata humu kulikuwa na mjadala mrefu kama alistahili kupewa nafasi ya kugombea tena awamu ya pili. Mjadala ule mrefu ulisababisha John Malecela atoe kauli kwamba MACCM "wana utaratibu wao wa kuachiana Rais aliyeko madarakani amalize awamu zake mbili" Kama 2010 wangemtosa au kama si wizi wa kura nchi yetu ingeyaepuka majanga mengi makubwa yaliyosababishwa na DHAIFU kuendelea kuwemo Ikulu.
 
Jana kama ulimsikia Deo filikunjombe alivyomnukuu Thabit kombo utagundua kuwa kuna mamlaka kubwa aliificha kuisema ambayo ni Rais mwenyewe, rejea nukuu yake kwa Thabit kombo.
 
ni kweli ila kwa sasa haisaidii, cha msingi tu Waziri mkuu wake ajiuzulu na wenzake wote, nimefurahishwa sana maana jana nchi ilisimama kwa muda.
 
Even my 80 y.o dauntless militant mother Ms. Hawa binti Juma could make a better president than this pompous but useless Sultan from Bagamoyo.
 
Hakupaswa na hapaswi kuwa kiongozi.Alikuwa kiongozi wa maonesho
 
Kinachotokea ni ushabiki na homage minimum haziongelewi. Tusubiri application ya Natural justice
 
Kwa katiba inayotawala sasa na katiba pendekezwa ya mwandishi chenge na udhaifu wa Jk tegemea kilio tuu. Uhalisia tuna President wa wasinii tz
 
Kiongozi gani asiye kemea maovu? Maovu mangapi tumeyasikia hapo nchini? Kuna mawili, aidha anawaogopa waovu au yeye mwenyewe ndiye kinara cha maovu. Hakuna pungufu ya haya mawili. Kwa kifupi kazi iliisha mshinda siku nyingi sana. Kilichobakia kwake ni kutumia vyombo vya dola kuua wasema ukweli. Atakumbukwa kwa kuua watanzania wengi kuliko wakati mwingine wowote. Nimewakilisha
 
Yaani unamiweka kando na ufisadi unaofanyika nchini? Ulitaka uone Imeandikwa 3.36bil transfered to jakaya kikwete?
Sio kwamba hayuko makini ila anapiga hela kimyakimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…