JK: Sikuidhalilisha Tume ya Warioba

JK: Sikuidhalilisha Tume ya Warioba

ghilipolla

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
280
Reaction score
53
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa hakuwa na nia ya kuidhalilisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati alipohutubia kulifungua Bunge Maalumu la Katiba, wiki mbili zilizopita.

Rais Kikwete alisema hayo jana kwenye ziara yake ya siku tatu ya kidola nchini Uingereza, moja ya ziara nadra kufanywa na viongozi wa nchi za nje nchini humo.

Alisema kuwa anawaheshimu sana wazee waliokuwa wanashughulikia mchakato mzima wa kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya, hivyo hakukuwa na sababu ya yeye kuwafanyia jambo hilo.

“Watu wamesema eeeh! umeidhalilisha tume!… Siwezi kufanya kazi hiyo! Nawaheshimu sana hao wazee ndio walionilea mpaka hapa nilipofika,” alisema Kikwete.

Alifafanua kuwa hotuba yake ililenga kuwashauri wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuangalia kwa kina masuala yaliyomo ndani ya Katiba ili kufanya uamuzi sahihi.

Wakati akiwasilisha hotuba yake bungeni hivi karibuni, Rais alionekana kutilia shaka takwimu zilizotolewa na tume hiyo.

“Nilitoa maoni yangu ya rasimu kwa sababu ninayo dhamana hiyo… Wao walitaka niseme; wajumbe nimelizindua Bunge. Hiyo haiwezekani,” aliongeza Rais Kikwete akiashiria kuwa ilimpasa pia kutoa nasaha zake.
Chanzo: Mwananchi
 
msiandike kikanjanja mm mwenyew nilikuwa namsikiliza bbc alisem suala serikal3 yy hana tatizo nalo km wananch wameridhia
 
Jk hana tabia hii ni mstarabu sana siku zote hawezi kumdhalilisha mtu wala kumbeza mtu alichofanya ni kuongea ukweli wa mambo ulivyo kasema pumba na mchele ndiyo kaacha jukumu kwa wajumbe wa bunge maalumu wafanye kazi yao.
 
msiandike kikanjanja mm mwenyew nilikuwa namsikiliza bbc alisem suala serikal3 yy hana tatizo nalo km wananch wameridhia
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.
 
Kitendo cha kumtaja Warioba na si tume, kitendo cha kuwadhalilisha akina Salim, Butiku, maprofesa na wasomi mbele ya TV, umma ukiangalia ni laana ambayo JK ataishi nayo milele.

Tulimweleza mapema awaombe radhi siku ile ile kwani ndio uungwana akakataa sasa anakimbia Uingereza baada ya kuwafedhehesha, kuwanyannyasa na kuwatia madole ya macho wazee wetu.

JK umeidhalilisha tume kuliko alivywahi kufanya kiongozi mwingine aliyetangulia.

Huwezi kumwita Jaji Warioba na Augustino Ramadhani wake meza ya juu halafu uanze kuwavua nguo kwa kuzusha.
Si umesema tume imependekeza majeshi 3, wapi hilo lipo.

Baada ya kuawatukana na kuwadhalilisha akina Salim Ahmed Salim, Butiku na wengine ukarudi Ikulu siku hiyo na kuvunja tume ili wasipate nafasi ya kujitetea. Ukawafunga midomo ili wabaki na aibu ya kuvuliwa nguo.

JK hili utaishi nalo miaka yako yote nasisi tunalaani sana dhalili uliyowafanyia hawa wazee
 
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.
Tofautisha qualitative na quantitative Tume ilitumia qualitative approach kwa kutumia focus group discussions na wala si scientific approaches za quantitative ili waweze kufanya sampling na wakimaliza waache kutumia statistic waweze kuweka weights ili wasizungumzie population kwa kufanya inferences. Sample ikiwa ni representative, hakuna issue ya uwingi itasumbua. Hivyo ni kitu cha ajabu kuhusisha results za Tume ya Warioba na Takwimu za Watanzania!!!!!! Kama mlitaka tuzungumzie idadi ya watu ilitakiwa kupata sampuli ya kisayansi (kutoka mtakwimu mkuu wa serikali) la sivyo tusichanganye. Hii tuwaachie Watakwimu.
 
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.
we jamaa bhana sidhani hata kama ulishiriki kwenye mchakato wa utoaji maoni .......ww hukuona wakati tume inapita?? haikupaswa kutoa maoni ya kujirudia rudia hivo watu ilipaswa wajikite katika hoja zingine pia kwani katiba ina vifungu vingi bwana,.... hivo ukienda kwa idadi na vipi waliozungumzia mgombea binafsi takwimu iko vp?.......madaraka ya raisi nao je? tueme idadi yao haitoshi hivo tusibadili ki2?
 
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.

Ni 62% wanaotaka serikali tatu. Kama alitaka mil 45 wote watoe maoni, Warioba asinge ruhusiwa kufanya sampling. Angepitisha kura ya maoni nchi nzima juu ya ya aina ya Muungano unaotakiwa. Madam sampling ilikubaliwa kwa ToR, basi Warioba yuko sahihi mpaka kesho.

AnayepingaTnaganyika urudi aondoe na Zanziba maana ndio washirika wa uungano.
 
Jk hana tabia hii ni mstarabu sana siku zote hawezi kumdhalilisha mtu wala kumbeza mtu alichofanya ni kuongea ukweli wa mambo ulivyo kasema pumba na mchele ndiyo kaacha jukumu kwa wajumbe wa bunge maalumu wafanye kazi yao.

eti unasemaje?
Acha kujitoa fahamu, kila mtu alishuhudia namna mheshimiwa alivyowadhalilisha wale wazee wa tume.
 
Mimi nakubaliana naye 100% kwamba hakuwa na nia ya kuidhalilisha tume ya Warioba, ila ALIKUSUDIA KUMDHALILISHA WARIOBA mbona mmekuwa wavivu wa kumuelewa JK? Alimteua ili kumtegeshea akashittukia Warioba ni mjanja anapata umaarufu, hivyo akaamua kumdhalilisha bungeni, kwani alichoendea pale ilikuwa kulifungua Bunge hilo na sio kuijadili Rasimu, kama na wenzake pale Ikulu naye alikuwa na nafasi adhimu sana kutoa maoni yake kama mwakanchi halali, pale bungeni alitoa maoni kama nani? Kwani naye ni mbnge mteule pale? Kama angekuwa mpinzani ungesikia 6 anamwambia KAA CHINI huna uhalali kutoa maoni hayo.
 
Mhs Hon Jdg Warioba sio mla rushwa, fisadi, jangili wala mwizi pamoja na familia!!
Mzee anajiheshimu pamoja na familia yake, ni kati wazarendo wachache tuliobaki nao!!!
Laana ya ufisadi itawaandama MaCCM daima na M/Kiti wao!!
Tunautaka Tanganyika yetu period!!
 
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.

Mkuu, naomba nikuulize:
1. Umewahi kufanya utafiti na unajua maana ya utafiti?
2. Hao Watz 49m unajua mgawanyo wao kiumri?
3. Nipatie uwezekano wa kuwahoji watoto wachanga.
 
Apeleke unafki wake, yy alienda kufungua bunge la katiba si kutoa maoni yake,
Kama aliweza kupokea Rasimu ya kwanza na ya pili akaipokea, angetoa maon kipindi hicho si bungen,
Pale alitakiwa kufungua bunge la katiba tu si kuichambua katiba,
Ndo maana tukisema Rais ni dhaifu sn aache unafki,
Kwenye uzinduz Rais hajahutubia kama rais ila alihutubia kama mwekiti wa ccm,
Ccm ni chama dhaifu sn!!
 
J.k amemdhalilisha Warioba asijifanye hamnazo, alimanisha yaliyopendekezwa na tume ya warioba ni upuuzi na haufai kuingizwa ktk katiba mpya!
 
Wananchi wanaotaka serikali tatu ni 49 elfu tu wakati nchi inawatu zaidi ya milioni 45.

Shule za kata.
Hivi Kikwete alichaguliwa na watu wangapi kuongoza watu 45m? Basi pia hii nchi haina rais.
 
Back
Top Bottom