Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 11,818
- 18,073
- Thread starter
- #21
Hoja yako ni kweli! Lakini kumbuka kuwa tutakuwa na kura ya maoni mwakani na kama rasimu hii ya katiba itakubaliwa, katika uchaguzi mkuu ujao tutahitajika kuchagua rais wa muungano na rais wa Tanganyika!Kama waliingia madarakani kwa katiba ya zamani,bc watatoka kwa kufuata katiba hiyo ya zamani ambayo inasema kuwa uchaguzi utafanyika kila baada ya miaka mitano (5).Lazima watoke 2015,
Bahati mbaya hatuna katiba ya Tanganyika hivyo tutalazimika kuanza mchakato wa katiba hiyo! Kutokana na uzoefu wa kuandaa rasimu hii ya katiba ya muungano ni wazi muda wa kuandaa katiba ya Tanganyika hautapungua miaka miwili! Na katika muda huo na ili kufanikisha kuandikwa kwa katiba ya Tanganyika, Bunge litalazimika kutunga sheria ya kuongeza muda wa uongozi wa serikali iliyopo madarakani!