JK sasa fanya hivi!!

It's a good advice and all points can be put into consideration. Ni vizuri muda mwingine kushauri na sio kuleta ushabiki wa kisiasa muda wote. Naimani kama sio yeye au watu wake wakaribu wanapita humu na watayawakilisha kwa Rais.
 
mkuu, hao uliowataja ni cha mtoto ukilinganisha na marafiki zetu. ukiigusa Tanzania utakuwa umeigusa Marekani, China, Ufaransa, Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Namibia na nchi zote za SADC. Tanzania imejitengenezea jina na ina permanent friends ambao ni mataifa makubwa tofauti na hao nyang'au uliowataja

"Hatuna marafiki wa kudumu wala maadui wa kudumu", G. W. Bush. We vipi bwana unadiliki kumuita rafiki mtu anayegeuka kama kinyonga?! Mtu ambaye mkianza kupigana atauza silaha pande zote mbili na kuchochea mpigane zaidi ili avune hadi vitu vyako vyote vya ndani! Unawategemea watu ambao mkianza kupigana wao wanakaa kikao kujadili nani achukue nini ndani mwako wanakubaliana na kukomba kila chako. Nakumbuka kauli moja kwenye movie flani inayohusu hali ilivyo Liberia "While they are busy killing each other, we got busy making money out of it"
 
Mayenga, Bila shaka hili bandiko lako litabaki kuwa miongoni mwa mabandiko bora kabisa na ushauri bora kabisa wa kufanyiwa kazi. Lakini kuna watu watakuja kupotosha hapa, mpaka utashangaa wanatumia ubongo gani kufikiria kabla hawajaandika.
 
Obama atamponza sana JK... Wananchi inabidi tuelewe kuwa ukubwa wa nchi yetu haimaanishi kuwa sisi tunajua vita sana kuliko wengine!

Naona dalili za kuibiwa rasilimali zetu na wajanja! Wanatujaza kiburi cha kijinga, tuingie vitani ili wao wakwapue!

Mheshimiwa rais,

Kila mzalendo mwenye kupenda taifa hili,amefarijika sana na hotuba yako ya jana ulyoitoa katika kambi ya Kaboya,pale wilayani Muleba,karibu kabisa na kijijini kwetu.Umeonesha na kuudhihirisha ulimwengu kuwa pengine kimya kingi kina mshindo_Onyo lako limepeleka ujumbe kwa nchi maadui na rafiki ya kwamba nchi hii iko imara na iko tayari kujilinda na kamwe mtu asidhubutu kutuchezea.

Kama raia mwema,ningependa kutoa ushauri ufuatao ili agizo na karipio lako liwe na mashiko.

1.Kuunda tume ya kijeshi au ya majaji kupitia mfumo mzima wa ajira katika majeshi yetu.Zipo tuhuma kuwa na ni ukweli ulio wazi kuwa nchii hii ina idadi ya wanajeshi,maaskari na maafisa wa ngazi za juu wa Usalama wa taifa, ambao si raia wa nchi hii.Katika hili,waraka wa Mtikila unaodai nchi jirani kupenyeza raia wa nchi zao na kuingia katika vyombo vya usalama,utakusaidia sana

2.Kuzifanyia kazi tuhuma juu ya chama chako,watendaji wako na ikiwezekana kuwafuta kazi mara moja watendaji wa ngazi za juu wa majeshi yetu ambao wamekuwa na tuhuma lukuki.

3.Kumfuta kazi mara moja Waziri wa sasa wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa,ambaye zipo tuhuma za wazi juu ya PHD yake.Ni aibu kwa jeshi kuongozwa na mtu ambaye ni mwongo.Kwa uwezo wake wa namna hiyo siyo kwamba uwepo wake waweza kuwa unachochea roho na moyo wa uasi dhidi ya wanajeshi wetu wapendwa?

4.Kujenga heshima ya Ikulu hasa katika mfumo mzima wa utendaji na utoaji wa matamko.Mtamko yanayotolewa na nyumba yetu pale Magogoni,yamekuwa yakiacha maswali mengi juu ya umakini na mfumo mzima wa utendaji katika nyumba yetu takatifu.Efficiency starts from WITHIN not from WITHOUT.

5.Kujiondoa mara moja katika shrikisho la Afrika Mashariki na kubakia na SADC pamoja na mashirika mengine ya kimataifa ambayo yana lengo la kutunufaisha.Kwa sasa hali ilivyo,kutokana na udhaifu wa watendaji tulionao katika wizara zetu,Wakenya na Waganda,hasa Wakenya,wamelitumia vizuri shirikisho hilo kujichukulia ardhi,kujipatia kazi,kufungua makampuni utitiri bila kufuata kanuni na taratibu za uwekezaji.Hii inapunguza usalama.

6.Kutopuuza kabisa,narudia kutopuuza kabisa malalamiko yanayotolewa na wanajeshi wetu dhidi ya maisha duni na stahili nyingine.Uzoefu unaonesha kuwa,mapinduzi katika nchi nyingi yamefanywa na wanajeshi wa kawaida na wala siyo mabrigedia,makanali wala majenerali.

7.Kuunda Wizara ya vijana peke yao,bila kuichanganya na wizara nyingine.Unda vijiji vya vijana,tunayo mapori mengi nchi hii,yatenge mapori tuliyo nayo,wape zana za kisasa vijana,wazazalishe chakula na uzalendo katika vijiji hivyo.Uangalizi wao uwe chini ya watu wenye upeo na maadili.Wasiwasi wangu ni kuwa kwa hali inavyokwenda,wimbi la vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT,wanaofukuzwa toka CCP,wanaomaliza vyuo na shule ni BOMU kama alivyosema mshirika wako Edward.

8.Mwisho kabisa,ikitokea nchi hii iakenda vitani,ni raia wa nchi hii ambao watapigana kuikomboa,ni raia wa nchii hii watakaotoa senti yao ya mwisho ili nchi iwe salama.Jeshi haliwezi kupigana peke yake bila kuungwa mkono na raia.Hivyo basi,kwa hali ilivyo sasa,mahusiano ya majeshi yetu na raia lazima yaangaliwe kwa umakini mkubwa.Matukio ya polisi na wanajeshi wetu katika siku za karibuni,yanazidi kujenga usugu wa chuki miongoni mwa raia.Mshauri Waziri wako Mkuu aombe radhi kwa kauli yake kwa wananchi na azuie vyombo vya usalama kupiga raia.Hii itasaidia kuungwa mkono ikiwa mambo yatakwenda mrama.


Ni ushauri tu Mzee wa Magogoni.
 
Una mawazo mazuri sana mpendwa katika kristo but kwa Tanzania.... inawezekana....... ila ni kiongozi aliyejitoa kwa dhamira ya kuikomboa nchi yake na wananchi wake ndio anaweza kufanya haya.
 
Mkuu ni ushauri mzuri, lakini wananchi nao hasa wanasiasa ambao wanatumia makjukwaa ya kisiasa kujipatia umaarufu kwa kukebehi, kupotosha na hata kudhihaki vyombo vyetu vya ulinzi watambue kuwa kufanya hivyo ni kujijengea uadui na vyombo hivyo na ni vyema wakatafuta umaarufu kupitia sehemu zingine.

Hakuna mtu anatafuta umaarufu kwa kukebei vyombo vya ulinzi. Ikitokea nyumbani kwako ukamuajiri mlinzi, alafu mlinzi huyo akawa anachora mipango uibiwe, utaendelea kumuajiri au?
Serikali imeajiriwa na wananchi (hata kama ni kwa mlango usioruhusiwa) na serikali hiyo ndo msimmizi mkuu wa vyombo vya dola, vyombo hivyo badala ya kulinda raia na mali zao (polisi) - vimegeuka kuwa magenge ya waporaji, majangiri, majabazi, watekaji nk, - wakisemwa ili wajirekebishe wanaibuka watu wa kuwatetea (kama wewe thatha aka Chacha) eti ni kebei, WACHA MARA MOJA KUPINDISHA UKWELI, Majuzi tu askali magereza wamebambwa kwa tuhuma za ujangiri, wakisemwa ni kebei hizo?
 
KWA UHUSIANO ULIOPO KATI YA RAIA WA KAWAIDA NA JESHI LETU LA WANANCHI(JWTZ) NI DHAHILI KABISA KWAMBA UWEZEKANO WA KUPIGWA JWTZ NI MKUBWA SABABU ikitokea vita hata leo wananzengo watakuwa upande wa ADUI.Tukio walilo lifanya kule MTWARA limewavunjia heshima(JWTZ) kwa kiwango cha juu mno.Hawatakuwa na pa kujifichia, siri zote za minendo yao wakati wa vita zitakuwa wazi mno kwa ADUI.
 
KWA UHUSIANO ULIOPO KATI YA RAIA WA KAWAIDA NA JESHI LETU LA WANANCHI(JWTZ) NI DHAHILI KABISA KWAMBA UWEZEKANO WA KUPIGWA JWTZ NI MKUBWA SABABU ikitokea vita hata leo wananzengo watakuwa upande wa ADUI.Tukio walilo lifanya kule MTWARA limewavunjia heshima(JWTZ) kwa kiwango cha juu mno.Hawatakuwa na pa kujifichia, siri zote za minendo yao wakati wa vita zitakuwa wazi mno kwa ADUI.

Tuombe Mungu awafungue masikio na wasikie.
 
MWANAMKE ALIBAKWA NA KUPASULIWA TUMBO KWA RISAS(sio movie ni kweli) KULE MTWARA, WATU WANACHOMEWA NYUMBA, WANAPIGWA N.K ET VITA ITOKEE AMWAMBIE JAMAA ALIYEMUUA MKEWE ADUI KAPITA HAPA,ITAKUWA MAAJABU,LEO HATA MTU ASIKIE KUNA NJAMA YA KUVAMIA KITUO NANI ATAENDA TOA TAARIFA? KAMA UKIENDA TU KESI INAKUGEUKIA AU WANAKUTAJA KUWA UMEVUJISHA SIRI KWAN WAKUBWA WANAHUSIKA.HV MNADHAN HAKUNA ALIYEJUA KABLA KUWA POLIS CENTRE MWANZA KUNA UHALIFU UTATOKEA? WALIJUA NA WENGINE NI ASKAR BUT UZALENDO UKATUPWA KWAN WANAFAMILIA MASKIN ZINAWATEGEMEA.
 
MWANAMKE ALIBAKWA NA KUPASULIWA TUMBO KWA RISAS(sio movie ni kweli) KULE MTWARA, WATU WANACHOMEWA NYUMBA, WANAPIGWA N.K ET VITA ITOKEE AMWAMBIE JAMAA ALIYEMUUA MKEWE ADUI KAPITA HAPA,ITAKUWA MAAJABU,LEO HATA MTU ASIKIE KUNA NJAMA YA KUVAMIA KITUO NANI ATAENDA TOA TAARIFA? KAMA UKIENDA TU KESI INAKUGEUKIA AU WANAKUTAJA KUWA UMEVUJISHA SIRI KWAN WAKUBWA WANAHUSIKA.HV MNADHAN HAKUNA ALIYEJUA KABLA KUWA POLIS CENTRE MWANZA KUNA UHALIFU UTATOKEA? WALIJUA NA WENGINE NI ASKAR BUT UZALENDO UKATUPWA KWAN WANAFAMILIA MASKIN ZINAWATEGEMEA.

Hii ni hatari sana Mkuu
 
Back
Top Bottom