JK ndio Mkombozi wa Taifa hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ndio Mkombozi wa Taifa hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, May 22, 2012.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jana nikuwa kwenya daladala kukawa na majadala baina ya abiria. Wenga wa wawachangiaji walikuwa wanasema ukitaka nchi hii itoke hapa ilipo na ipige maendeleo ya haraka ni lazima CCM ife na iondoke madarakani. Wakawa wanesema CCM ndio chanzo cha matatizo yote haya na jinsi kilivyojichanganya na wanyonyaji wa nchi hii hakiwezi tena kuiondoa nchi hapa ilipo kunahitajika chama kingine. Wakaendea kusema ili CCM ife ni lazima atokee mtu ndani ya CCM mwenye uzalendo na kuielewa CCM kiundani aweke na kuandaa mkakati wa kuiwa CCM. Mazungumzo yale yaliendelea kusema kuwa mtu huyo atapata heshima kubwa sana huko tuendakako. Mazungumzo yale yamenifanya nikaingiwa na ushawishi kuwa huenda JK ndio mtu huyo. Wanajamii mnasemaje?
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwani si yuko kwenye the same chama
  atakuwa mkombozi kukiua chama chake na kuleta ukombozi kwa chama kingine kupata madaraka
  maana alicho nacho kishajifia na kinahitaji kabisa kuzikwa
  May be hilo linawezekana na yeye kuwa mmaliziaji wa hilo zimwi la chama chake
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,799
  Trophy Points: 280
  Ametukomboaje sasa? Kwa kupatia dawa rushwa na ufisadi au vipi?
   
 4. m

  mamajack JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  jk ni mteketezaji wa taifa hili! ila kama akiwajibishwa yeye na watu wake kwa kufilisiwa labda ndo atakuwa mtu mwenye historia lakini bila hivyo,twakwisha tusipotaka mabadiliko.
   
 5. J

  Joblube JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo husomi unakurupuka
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,653
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Nafikiri hukumuelewa muanzisha uzi huu,kama mimi nimemuelewa ni kuwa kipindi hiki cha utawala wa JK ufisadi ndiyo umerutubishwa mpaka kufika kiwango ambacho haihitajiki tena operesheni sangara kuulezea uozo wa CCM hivyo iwe rahisi kwa watanzania wenye akili timamu kuikataa CCM na kuicha ikifa kifo cha Mende. Ndiyo maana wengine wanasema kuwa JK ni chaguo la Mungu ili CCM ife na Tanzania ipone.
   
 7. k

  kumchaya Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inabididi kuwa na upembuzi yakinifu kutambua ulichosema kuwa JK nimkombozi wa taifa hili,nakumbuka wakati anaingia madarakani kuna mwandishi mmoja wa RAI kipindikile chini ya uongozi wa jenerali ulimwengu aliandika makala kuwa JK ndio atakayeweza kuiua CCM au kuifanya itawale kwa miongo mingine mingi sana,akimaanisha kama utawala wake utfanana na waliomtangulia basi itakuwa mbinde kuitoa CCM madarakani,enzi za mwalimu enzi za zidumu **** za mwenyekiti ulikuwa ukitofautiana nae kimawzo ukatafute kuwa mkimbizi au urudi kijijini kufuga kuku,kumbuka kambona alikimbilia uk,mtei aling'atuka ugavana wa BOT kwa kuwa alimshauri mambo kitaalamu akakataa.kipindi cha mzee ruksa ukiwa upinzani ulifukuzwa ama kunyang'anywa haki zako zote kazini,hata wafanyabishara walishindwa hata kusalimiana na upinzani maana ndio ingekuwa mwishowako,ben naye ndio usiseme ubabe kwa kwenda mbele,alitumia gharama kubwa sana mpaka kuzaliwa akina EPA na wenzake kwa ajili ya kuisaidia CCM kuendelea kutawala na kuzima kila dalili ya upinzani ama kupingwa kwa jambo lolote linaloonekana halina mustabali mzuri na taifa, kumbuka alishawahi kuwaita waandishi wa habari wana wivu wa kike kwakile tu cha mawaziri wake kukosolewa, JK nitofauti sana na waliomtangulia,kwanza hana jazba,alipoingia madarakan kuna baadhi ya hii mitandao ya kijamii ilimchora anafanyiwa jambo moja baya sana na aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi,ilikuwa sababu tosha ya kuizuia isitumike tena hapa nchini,hata pale walipompelekea wazo hilo la kuifungia alikataa na kusema hatuwezi kuifungia yote kwa kosa la mtu mmoja,JK nikama kondoo aliyendani ya kundi la chui,akiamini taifa hili kwa upinzani kuwa na nguvu ndio itakuwa salama yetu,kwa haraka haraka ukiangalia maamuzi mengi anayoyachukua ni kama kukiweka chama uchi,1.michakato ya kugombea ubunge kwa kuanza na kura za maoni ni moja ya mambo yaliyochangia kukikoroga chama kwa kuondoa yale mazoea yao ya kuchaguana kimtindo huku akijua result yake itakuaje,2.mchakato wa katiba, haikuwa agenda ya CCM,wakijua kama itapatikana kwa njia ya kidemokrasi basi itawaweka pabaya kisiasa,3.riport ya CAG kwa mara ya kwanza ndio raisi wa kwanza kusema ikajadiliwe kwa kina bungeni huku akijua matokeo yake ni serikali yake kutukanwa na kukosolewa vikali,na hivyo kuzidi kukipelekea chama chake kukosa mvuto,4.wapinzani kwake sio ugomvi,chuki, na husuda,yupo tayari kuzungumza nao pale inapoitajika na kitendo cha kukubaliana nao jambo lolote,kisiasa ni kukishusha hadhi chama chako kwa kushindwa kukushauri mpaka anakuja mtu pembeni kukuonyesha mapungufu, kwa mtazamo huu mdogo kwa kulinganisha na wengine anaonekana yupo tayari hata kukabidhi nchi hii kw chama kingine.5.vyombo vya habari vinafanya kazi bila kuingiliwa kwa kiwango kikubwa sana,jambo ambalo ni hatari kwa chama chake,kwa maana chama kilichopo madarakani siku zote matatizo yake ni rais kuonekana,6.KUMKATA LOWASA MIGUU,alikuwa na nguvu kubwa sana na ushawishi mkubwa ndani na nje ya chama,lakini hatufai kuwa raisi wetu kwa idadi ya mali alizonazo inatisha,jazba , kiburi na dharau inayojengwa na utajiri wake.
  JK nimkombozi wa taifa hili kwa kukiweka chama chake REHANI.
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mr Rocky umekurupuka.. joblube anasema JK nimkombozi kwa kututoa kwenye makucha ya zimwi ccm, anachofanya JK ni kuiua kisha kutaibuka wengine watakaotawala kwa ridhaa ya watawaliwa, hivyo ndivyo alivyomaanisha huyu mwenzetu..
   
Loading...