JK ndani ya mji wa Moshi....

kwa jinsi anavyopiga mwereka sidhani kama ana nia ya kuupanda mlima. Wasi wasi wangu ni kwamba labda anataka kuupiga bei mlima wetu!

Unaweza kukuta ana dogo dogo mpya Moshi ameifuaa halafu hilo ni changa la macho tu.

Nasikia tarehe 07.03 atakuwa Loliondo kuzindua umeme wa kutumia majeneta. Sijui kama ataenda kwa babu kumsalimu au kurenew charge kwa kupiga kikombe tena.
 
Mar 5
[h=1]Rais Jakaya Kikwete Atua Mkoani Kilimanjaro Kwa Ziara Ya Kikazi Ya Siku Tatu[/h]


MO2.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)jana jioni tayari kwa ziara ya siku tatu.
MO1.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni Jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
MO4.jpg
MO3.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi Jana Jioni.Picha na IKULU
------​
306px-Coat_of_arms_of_tanzania_svg1.png
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi jana, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.

Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

MWISHO

Imetolewa na

KURUGENZI YA MAWASILINO YA RAIS
MARCH 4, 2012
MOSHI
 
Dunia hii ina vituko kweli...baada ya kuharibu Ulaya na Marekeni sasa tunaharibu humu humu ndani.
 
Na kale kaugonjwa ketu kalikompatia sifa Babu wa Loliondo katamuacha kweli? Nasikia na yeye alikwenda kupiga kikombe cha babu! Nijuavyo mimi kama afya yako inahitaji msaada wa kikombe cha Babu basi ukijidai shujaa wa kupanda mlima Kilimanjaro ujue huo ndo mwisho wa maisha yako au utasababisha watu wakubebe kwenye yale machela yetu!............. Mungu ongoza mkono wako ili mheshimiwa rais wetu asikubali kupanda mlima Kilimanjaro kwani bado miaka mitatu tu tumpe heshima ya ustaafu!.........

Kwenye ushauri nasaha tunaambiwa Usimwonyeshee mwenzio kidole, wewe vidole vingapi vinaangalia kwako?
 
Back
Top Bottom