Mimi ninasubiri kwa shauku kubwa kuona Watanzania tukianza kuona umuhimu wa mwelemeo wa uwiano wa nguvu za kisiasa (tilt in the balance of political power) katika kuwafanya wanasiasa wetu na vyama vyao watuthamini sisi binafsi na mahitaji yetu badala ya dharau na kebehi wanayotuonyesha sasa. Kinachotakiwa, kwa kuanzia, ni CCM kupunguziwa viti vya uwakilishi Bungeni na kwenye Halmashauri. HILO NI LAZIMA LIFANYIKE KAMA KWELI TUNAJIJALI. Kuwaongezea ni kosa lisilo na msamaha kabisa na, likitokea, basi Watanzania tuwe radhi kuendelea kudhalilishwa na utawala wa kibazazi usio na soni. Na hapo tusisumbuke kumnyooshea kidole mtu mmoja mmoja au CCM kama chama. Hata ingekuwa CHADEMA mnawapa asilimia 90 na kuwahakikishia uhai wa kisiasa usio na ukomo, wataendelea kuwala tu. Surely they are not your uncles.