Kiluilui
Senior Member
- Mar 22, 2012
- 153
- 21
Kwa mujibu wa kada wa CCM ambaye ni mjumbe wa NEC ambaye amavujisha siri hii, inasemekana kuwa Mh Mangula alipotoa kauli ya kukataza wanaccm kujinadi kabla ya kipindi cha uchaguzi alisababisha Mh.Lowasa na wengine wengi wenye uchu na madaraka 2015 kuchukizwa na kauli hiyo na kuamua kufanya kila namna kahakikisha Mangula anadhibitiwa vema ama anafanyiwa kila namna hadi ajiunge na kambi ya Lowassa ili apunguze msuli dhidi ya harakati za mbunge huyu wa monduli.
Kwa mujibu wa kikao cha JK na wabunge kilichofanyika dodoma hivi majuzi, JK amedhihirisha kwenda kinyume na msimamo wa Mangula kwa kutoa amri kuwa wanaccm wanaotaka kuwania nafasi za urais na ubunge kupitia ccm ni ruksa kuanza kujipitisha kwa wapiga kura.
Kauli hii tata ya Mwenyekiti wa ccm mrisho jakaya kikwete imeshangaza wengi hasa baada ya kudhihirisha kuwa ni kauli inayopingana na maazimio ya awali yaliyopitishwa na kikao cha Nec yaliyotangazwa na Mangula ambaye ni m-nec wa ccm.
Viunga vya ccm vya ndani kabisa vinapasha kuwa baada ya JK kuonyesha wazi kuwa anasupport harakati za kujinadi zinazofanywa na Lowasa pamoja na wanasiasa wengi wa ccm kumesababisha mpasuko wa hatari ndani ya ccm ambapo mwisho wa siku tutajionea jinsi Mh. Mangula pia anajisalimisha kwa Lowassa mithili ya mbwa koko aliyekutana na chatu na wengine watasambaratika kila mmoja kivake bila kujitambua.
Huu unaitwa ni mpasuko ndani ya ccm kwasababu makada maarufu wameshaanza kutupiana maneno makali hasa baada ya wengine kugundua kuwa wanatumiwa vibaya na JK mithili ya mbuzi wa kafara.
Nape Nnauye ni Kada mashuhuri wa ccm ambaye ameonekana dhahiri kutetereka na mwenye hofu kubwa hasa baada ya kumuona JK akimsifia Lowasa hadharani na akimpa ruhusa ya kujinadi kwa wapiga kura kwa ajili ya urais 2015.
Wachambuzi wa maswala ya siasa wanakiri kuwa JK ameanza kudhihirisha kuwa anamsanifu Membe na na nia yake kuu ni kumrithisha Lowasa kiti cha kugombea urais 2015 kupitia CCM.
Makambi yote ya ccm yaliyokua yakiwania nafasi ya uwakilishi wa rais yameanza kuyumba gafla baada ya kutatanishwa na msimamo wa nwenyekiti wa CCM Mh.Mrisho Jakaya Kikwete juu ya nafasi ya urais 2015,
' wengi walidhani kuwa JK amemsaliti Lowasa na kuunga mkono kambi ya Membe kumbe la hasha bado JK anamuandalia makao Lowassa'. Hayo ni maneno ya kiongozi wa Nec aliyekuwa akichekelea mtafaruku huu mkubwa unaodhihirisha kuwa JK kama mwenyekiti wa ccm amepanic kutokana na speed ya CHADEMA hadi amejikuta akitoa maagizo yanayopishana wazi kabisa na maazimio ya NEC ya ccm yaliwekwa hadharani hapo awali na Mangula.
My take.
Wale makada waccm wanautumika kama big.G huu ndo muda wao maalum wa kutemwa rasmi na JK pamoja na viongozi wengine wa ccm wenye uchu wa madaraka.
Sakata hili pia linadhihirisha kuwa JK amewaingiza mkenge puppets wengi sana wa ccm.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums