JK na intelijensia ya kishirikina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK na intelijensia ya kishirikina

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chintu, Feb 6, 2011.

 1. C

  Chintu JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,407
  Likes Received: 861
  Trophy Points: 280
  Kwa mshirikina, hata matatizo yenye chanzo kilicho dhahiri hudai kuna mkono wa mtu. Mfano kipindupindu kinapoikumba familia hajiangaishi na uchafu wa nyumbani kwake au kutochemsha maji ya kunywa badala yake anaweza hata kutumia upanga kumdhuru yule anayemuona ndio chanzo cha familia yake kuugua (refer Arusha incidence).
  Shehe Yahya siku moja alieleza chanel ten TV sababu za JK na Mengi kumsupport kutibiwa India kuwa sio hivi hivi tu bali wanamlipa fadhila kwa yale makubwa anayowatendea. Alieleza kwa kifupi mchango wake katika kumfikisha hapo alipo leo. Kuhusu Mengi alidai Mengi mwenyewe anajua anachomfanyia.
  .....Baada ya hiyo background fupi sasa nieleze hoja yangu. Jana JK amesema maandamano ya wananchi kudai haki zao yanachochewa na chama fulani (obviously ni CDM) kwa lengo la kuishambulia serikali yake. Intelijensia ndio wamemwambia hivyo. Binafsi siamini kama intelijensia inaweza kumpa rais wetu sababu za kishirikina kama hizi, kwa sababu kuna mambo ya dhahiri kabisa kuwaudhi wananchi hata bila kushawishiwa na chama chochote. umeme kupanda bei sambamba na serikali kutaka kumlipa LA AZIZ bil 94, mfumuko wa bei, posho kiduchu ya wanafunzi vyuoni 5000 per day -(kuanzia chai, Lunch, Dinner na kulala) wakat wabunge wanalamba zaidi ya 100,000 per day tena juu ya mishahara yao minono. Lakini kinachokera zaidi ni wizi wa akina La Aziz (Kagoda, DeepGreen, Richmond, Meremeta, Rada na wajomba wote wa EPA) kama walivyo elezwa na Dr Slaa. Mimi naamini intelijensia ya kweli haiwezi kumwangalia Dr Slaa na chama chake kuanika ufisadi huo hadharani. Wangemwambia Mzee chanzo cha wananchi kudai haki zao ni dili zenu na washkaji wako kukomba pesa zao na wewe ukabaki bubu wkati wao wanapigika na bili za umeme na gharama za maisha.
  JK anasema eti watakifumua chama kama nyoka anavojivua gamba. swali ni je hilo gamba jipya ni lipi? UVCCM? si wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka?.
  Mi nadhani CCM wamezidiwa wanahitaji ushauri nasaha kama mgonwa wa ukimwi.
  Kwa mfumo tulionao si lazima CCM ifumuliwe Raisi ndiye anayetakiwa kufumuliwa. aache kuchekacheka kwenye mambo serious. Mrema (kabla hajachakachuliwa) aliwahi kusema Rais ndiyo dira ya kila kitu Tz, mkiwa na rais mla rushwa basi mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wakuu wa mikoa, ma DC wote watakula rushwa, na mkiwa na rais serious ktk maslahi ya taifa basi wote watakuwa serious.
  Viongozi wote waliochini ya raisi huangalia msimamo wa bosi wao katika kila wanachokifanya.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Katika maandamano ya Arusha hakuna aliyekuwa akidai haki bali ulikuwa ni uhuni wa viongozi wa cdm.
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unataka kusema Katiba ya JMT inaruhusu kuuwa wahuni?
  Acha kujisaidia wakati una ning'inia kichwa chini miguu juu kama popo-Unajichafua mwenyewe!
   
Loading...