JK mwombe radhi Dr Salim..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK mwombe radhi Dr Salim..!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KYALOSANGI, Feb 25, 2011.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Kati ya mambo yaliyonifanya nimchukie zaidi JK ,ni zile njama zilifanywa kumchafua DK Salim wakati wa uchaguzi 2005!Hakuna haja ya kuyarudia lakini kumtendea mtu mwema maovu ni laana !.inawezekana yanayokupata Mkwere ni laana hiyo ,hebu geuka nyuma umwombe radhi huyu mzee .Maisha yako huko mbele na familia yako na wafuasi wako yapo gizani mawazo ya Watanzania yanageuka kwa kasi ....BADO UNA MUDA WA KUTUBU.
   
 2. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Muombe wewe Dr salum manake unajipendekeza kwa yule mwarabu balaaa!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  kwani nani amekwambia yanayompata leo kj ni sababu ya Dk salim?

  huyu mzee ccm nzima lakin hasa wazanzibari hawampendi sasa wewe leo unakuja hapa na hoha isiyo na mashiko


  jk hakui kuongoza full stop wala hakuna mkono wa mtu hapo
   
 4. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Na kweli Umelengwa kati hata mawazo yako ni ya kulengwa kati! pole sana watakuumiza !
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  thread zingine bana...zinajaza seva tu
   
 6. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Source?
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Nimekugongea thanks maana wengine hata kufikiri hawawezi.

  Na ni Wazanzibari gani waliokuwa hawamtaki, hebu jiulize hiyo si ndiyo ilikuwa sehemu ya propaganda chafu zilizoenezwa na munaowafahamu nyinyi?
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe wengine pia mliliona hili la Dr Salim kupakwa 'kinyesi' mwaka 2005 alimradi tu urais ausikie tu radioni?

  Sasa ile laana ya Mwana-TANU Mzee Ndesamburo, kama walivyo Wazee wastaafu wa Afrika Mashariki, ni kule sisi vijana wao kutumwa kule kwenda kuwapiga virungu eti kwa sababu tu wengine tuliandika kazi ya Fanya Fujo Uone.

  Kwani hata huko makwenu huwa hakuna wazee???
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Siku 9 za kishindo zatangazwa
  [​IMG]
  Polisi wa Mwanza wafagiliwa

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akiwahutubia maelfu ya wananchi walioshiriki maandamano ya chama hicho ya kupinga mfumuko wa bei na malipo ya Dowans yaliyofanyika jijini Mwanza jana.  Maelfu ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walifanya maandamano ya amani yaliyoongozwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ambayo yalikuwa na msisimko mkubwa bila ya vurugu yoyote.
  Maandamano hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kutoilipa Kampuni ya Dowans, kupanda kwa bei ya umeme na kutokubali uchaguzi uliomweka madarakani meya wa Jiji la Arusha. Maandamano hayo yaliyoongozwa na
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilibrod Slaa na wabunge karibu wote wa chama hicho kutoka karibu majimbo yote Tanzania, yalianzia katika viwanja vya shule ya msingi Bugarika na kumalizikia katika viwanja vya Furahisha jijini hapa ikiwa ni karibu ya kilometa 10, ambapo viongozi hao wote walishiriki mwanzo hadi mwisho pamoja na maelfu ya wananchi wa Jiji la Mwanza, Baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
  Akizungumza katika mkutano huo mkubwa kwenye viwanja vya Furahisha, Dk. Slaa alisema kuwa Chadema inamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua kali wale wote walioliingiza taifa katika matatizo ya kampuni ya Dowans.
  Alisema kuwa anaamini kuwa kabla ya kumaliza maandamano hayo ya siku tisa katika mikoa tofauti, Kikwete atatangaza kuwachukulia watu hao waliosababisha taifa kutaka kuilipa Dowans wakati kampuni hiyo ni haramu kutokana na Kamati ya Bunge kutamka kuwa mkataba wa Kampuni ya Richmond uliorithiwa na Dowans haukuwa halali.
  "Tunajua kabla hatumaliza maandamano yetu ya siku tisa tuna imani kubwa kuwa (Rais) Kikwete atangaza kuwachukulia hatua waliohusika la sivyo wananchi watatumia nguvu ya umma kama nchi za Kaskazini ya Afrika ambako kuna wimbi la nguvu ya umma ambalo linawatoa madarakani viongozi," alisema Slaa.
  Pia aliwaomba wananchi kuwazomea wabunge wote wa CCM watakapokuwa majukwaani kama walivyofanya wakati ule wa EPA, ambapo walikuwa wakiwazomea wabunge kila walipokuwa wakihutubia.
  Naye Mbowe pamoja na mambo mengine ya kuishinikiza serikali kupunguza bei ya umeme na kutoilipa Dowans, aliwataka askari wote kuielewa Chadema na kulinda maslahi ya umma badala ya kuwalinda mafisadi wachache wanaoimaliza nchi kila uchao.
  "Askari mgome kuwapiga watu, kama Misri askari waligoma kabisa kuwapiga watu, lakini Arusha askari walikubali kuwapiga ndugu zao risasi wakati hawakuwa na hatia," alisema Mbowe.
  Mbowe alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, kwa kukubali maandamano hayo na kutowapiga mabomu watu wa Mwanza tofauti na Arusha ambako polisi wa huko kila mara wamekuwa wakiwapiga mabomu wananchi wa huko.
  Mbunge wa Arusha Mjini, Godobless Lema, naye alikuwepo katika maandamano hayo alilaani polisi wa Arusha kuwapiga wananchi kila uchao, ambapo alisisitiza kuwa wananchi wa Arusha sasa hawaogopi mabomu ya machozi na wanayaona kama manukato tu.
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  UNGANISHA NA HII
  Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.
  Sasa ilikuwa hivi,
  Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombewengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwawingi wakati huohuo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.
  Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwamengi mno na mazao yametapakaa mashambani,. akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.
  Aliendelea kufanya hivyokwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

  Sasa bwana ,,kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa raisi kipindi hicho JK Nyerere.
  Katika barua hiyo akaandika lawama nyiingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwakuwa navunja miiko ya uongozi na mambo mengine meengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)....basi bwana, akamalizia mwisho kwakujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa rais wa nchi wakati huo!......

  Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.
  Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni maMbo yenu kayamalizeni hukohuko".

  Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yakee...., sasa siku mija alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

  Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwette aliyomwandikia raisi!!....
  Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! na akafurra kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

  Alipofika tu yule mmasaai aliitisha kikao cha wakufunzi woote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copi ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....
  Balipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwaliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwette!!!
  Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa mkwere...
  Sayore akaanza kuwagawia zile nakala(copi) za ile barua ya kikwete kwenda kw a raisi akawagawia wooote inlcuding Kkwete!!! Huku yule mmasasi Sayoreakiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo baru!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

  Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani.......
  Alichokifanya ni kuondoka harakapale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu...
  Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER!! hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! just imagine kutoka monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimi ilikuwa kusalimisha maisha yake......

  Basi huo ndiyo ukawa mwishi wa JK monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama...lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!! Hicho ndicho chanzo cha JK kumchikia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadileo! yeye humwita mzee nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita father of our nation, laikini ni pale napotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....

  **Ndugu zangu hiki ni kisa cha ukweli kwa 100%, inawezakana uandishi wangu ukawa na upungufu, lakini niemekipata kutoka watu mbalimbali waliowahi kuwa karibu sana na mkasa huu...
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Aisee! Ilikuwa mwaka huu mkasa ulipotokea?
   
 12. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hmmm! Tutasikia yote!
   
 13. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bintimkongwe,

  Na wewe nimekugongea thanks leo. Hata wewe leo umekubali kwamba kuna mtandao wa fitna wa kuwaharibia wenzao ili umma uwachukie.
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  wewe hata ukitajiwa lini ulitokea utauliza tena soma alama za nyakati ---

  Hujui hata nyerere aliishi kipindi cha miaka gani
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  kuanza upya si ujinga
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania hawana tabia ya kuomba radhi ndio maana hulaanika na nchi pia huwa matatizoni kama ilivyo sasa nchi yetu.
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee hana shida nadhani aombe kwa Mola wake
   
 18. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo kumbe yameanza kitambo eee kwali historia ni nouma
   
Loading...