JK mgeni rasmi uzinduzi wa barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK mgeni rasmi uzinduzi wa barabara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Sep 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumanne, Septemba 18, 2012 05:41 Na Oliver Oswald, Dar es Salaam

  RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja, unaoendelea katika baadhi ya maeneo nchini.

  Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango, alisema uzinduzi huo utahusisha miradi mitatu ambayo ni ya ujenzi wa madaraja, barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi pamoja na barabara za kawaida, ikiwamo Barabara ya Makofia-Msata.

  Alisema kwa sasa Serikali ya awamu ya nne inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa yote.

  Balozi Mrango alisema kuna barabara zenye urefu wa kilomita 11,154, ambazo zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

  Kwa mujibu wa Balozi Mrango, Rais Kikwete, ataanza na uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Makofia-Msata, iliyopo Bagamoyo, yenye urefu wa kilomita 64 na kwamba uzinduzi huo utafanyika katika Kijiji cha Kiwangwa kesho.

  “Kesho (leo), Rais atazindua ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam ambao mkandarasi wa mradi huu ni Strabag International.

  “Mradi huu unahusisha Barabara za Kimara kuelekea Kivukoni, Magomeni kuelekea Morocco na Fire hadi Kariakoo.

  “Septemba kesho kutwa (kesho), atazindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambapo sherehe zitafanyika Kurasini,” alisema Balozi Mrango.

  Alisema pia kwamba, daraja hilo la Kigamboni linajengwa na Mkandarasi wa China Railway Constrution Company Limited, kwa kushirikiana na China Major Bridge Engineering Company Limited.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Naona JK anapambana kutimiza ahadi zake safi sana hizi ndio zitakuwa fimbo kuelekea uchaguzi mkuu.
   
 3. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  saaaaafi saaaaaaana JK maneno kidogo vitendo zaidi.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Si haba!
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa akiona hivyo roho inamuuma sana yeye anatamani kila siku JK akwame tu yeye apate singo ya kutokea.
   
 6. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,596
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  anachokifanya leo jk ni kama mtu mzima kutambaa ...miradi yote ni kwa hisani ya watu wa? na ni madeni kwa kwenda mbele deni la taifa linakuwa faster than ever......nakushauri angalia leo citzen tv saa moja jioni wataonesha jinsi kenya walivyo wanajenga mtambo mkubwa wa umeme wa makaa ya mawe sisi stiglers godge nihistory tangu imeanza kutalk

   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,591
  Likes Received: 9,524
  Trophy Points: 280
  naona kaamua kuchukua jukumu la bilali makamu wake..au ndege ya rais ni mbovu??
   
 8. O

  OPTIMUS TZ JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu issue ya Iran huko kwa wazungu hakuendeke kaka siku hizi anapinga Afrika na ndani
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ritz kumbe hujui kwa nini hatuwataki tena ccm si ahadi ni wizi mlioufanya miaka yote huko nyuma mliiba we eti leo unakisifu jk anatekeleza ahadi, wakati mafisadi wanakula bata tu na wezi wa kuku wanaozea segerea, mshachelewa baba m4c is larger than life itself
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,717
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Rais wa uzinduzi
   
 11. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,591
  Likes Received: 9,524
  Trophy Points: 280
  na mimi ndio naona hivyo mkuu......
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Huko na kutapatapa mkuu kwa hiyo Chadema wakichukuwa nchi pesa watatoa mfukoni kwa Dr Slaa.
  [h=2]Tuesday, August 10, 2010[/h] [h=3]*JK AZINDUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DAR[/h]
  [​IMG] Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre (watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa (kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani (kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilizofanyika Kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  [​IMG]
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Akwame mara ngapi huyo dhaifu!
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,793
  Likes Received: 1,581
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ritz vipi utakuwepo manake nami nataka nihudhurie nisikie Waziri Magufuli akitoa data!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. m

  mwitu JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 858
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  dhaifu
   
 18. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Navyomjua Magufuli atakuwa kanuna kweli(anatamani kupiga mbizi kuvuka kigamboni na kurudi) baada ya kuingiliwa kazi za Ufunguzi na Mwajiri wake.
   
 19. SIERA

  SIERA JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Mpaka ikifika 2015 padre atakua ana rwnd tu hatatoka tena
   
 20. m

  mpunumpunyenye Senior Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 113
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kwa hiyo ulikuwa unashauri aachee kujenga hizo barabara na mafaraja kwa kuwa amechelewa!??? Watu wa chadema kila kitu lazima mpinge duh
   
Loading...