Mu-Israeli
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 2,454
- 975
Inafurahisha sana kuwa hata wewe umeliona hilo, kama hakuna cha kuzinduwa angekuwa Rais wa uzinduzi?
Nnachompendea Kikwete ni pale ambapo amefanya kuli Rais yeyote yule, kuanzia Afya, Barabara, Elimu, Utalii, Viwanda, Demokrasia, Uwekezaji, Kudhibiti mali za Serikali na Kupambana na Rushwa.
Hakuna yeyote wa kabla yake anaefikia kiwango chake cha utendaji kilichotukuka.
Utendaji wa maovu 'uliotukuka' ??
Angalia hapa....
- Mauaji ya albino hayajawahi kutokea Tanzania isipokuwa ni katika kipindi cha JK !! Na mpaka sasa kesi kibao za mauaji hayo zinaning'inia tu !!
- Ufisadi wa hali ya juu sana Tanzania umetokea wakati wa JK, mpaka fisadi alifikia kukejeli watu kuwa wanahangaishwa na 'vijisenti tu'
- Utoroshaji wanyama pori umekidhiri wakati wa JK. jamaa wala hajali, yeye yuko majuu anatanua..
- Elimu imedorora sana wakati wa JK, mpaka wanafunzi wanachaguliwa kuingia sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika !!!
Huu ndio utendaji 'uliotukuka' wa JK !!!!