JK mara ya pili kumtembelea Magufuli

JK mara ya pili kumtembelea Magufuli

Nahesabu ni mara ngapi rais mstaafu amemtembelea rais aliyeko madarakani. Sihitaji kujua anatafuta nini lakini siyo dalili nzuri kwa mstaafu kurudi rudi ofisi uliyotoka. Kwa ajira zingine utaitwa mtu unayesikitika kuacha kazi.

JK alipoingia madarakani mbona hakutemebelewa na Mkapa mara nyingi kwa muda mfupi kama huu? Hakuna anayetaka kuingiliwa ktk utawala wake.

hamuachi mwenzake akafanya kazi kwa raha .....kila siku kiguu na njia .....anaenda kumuwangia nini?? .....naona hata taarifa ya habari hawakutoa video footage bali waliweka picha tu..na hawakusema wameongea eneo gani ...watakuwa wamechoka ugeni wake pale ...kasahau nini ??
muda kama huu mwenzake Mkapa alihamia Lushoto kabisa mwaka mzima hakuonekana mjini akawa anapiga whisky zake akimuacha Kikwete afanye kazi kwa utulivu na kupanga serikali ...
 
Ukiondoa Mwalimu, naona hawa viongozi wengine wana ajenda zisizoeleweka au unafiki wa kupindukia.
Sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi au Njomba akiitisha press conference nyumbani kwake kuelezea hali ya mambo inavyoenda hata kwa suala tete kama la Zanzibar. Na JK anaonekana kuchukua muelekeo huo huo.
Hiwezekani haya majipu yote yanayotumbuliwa wakati wa 'uotaji' wake hawa wastaafu hawakuwahi kuyaona. Na kama kweli hawakuwahi kuyaona basi hawatufai na kama waliyaona na kukaa kimya tuwajue ndiyo mwendelezo wa majipu!


Tofautisha marais waliofuatia na Mwalimu ...mwalimu aliondoka madarakani ili aweze kuandaa utamaduni mzuri wa succession kwa nchi ambao hadi leo tunaufuata ....wa kuheshimu mihula na kadhalika ......hivyo alichokuwa akikifanya mwalimu ni kuandaa misingi imara ....na technically Rais alietawala baada ya Mwalimu ..mzee mwinyi na mkapa walikuwa wakiongoza kwa kivuli cha Mwalimu kwa mambo mengi .........yeye akiwa kama baba ......
Mwalimu kafariki nafasi yake kwenye mioyo ya watu haiwezi kuzibwa kwa Mwinyi au Mkapa kutaka kuvaa viatu vyake .....kwa kuwa wote ni wanafunzi wake
 
mkuu yule amezoea kufanya mazoezi, kukaa home tu sio mpango, anatembeatembea...!
 
Ninachoona hapa ni umbea na usengenyaji usio na maana, kabla hamjaanza kumsema mtu vibaya ni bora mkafanya uchunguzi au kuuliza je alikwenda ikulu kwa inshu gani, aliitwa na raisi au kuna suala gani limempeleka pale, sizani kama JK ni mpuuzi kiasi hicho kwenda ikulu bila ya mwaliko.. Mkishajua kilichompeleka ndio muanze kulaumu au kupongeza sasa

period
 
yaani ningekuwa ni mimi ningeona aibu sana, nisingejitokeza kabisa hata kwenye vyombo vya habari na hata ikulu nisingegusa. ni aibu sana, watz tumeishi maisha kama nyakati za ujima kwa miaka kumi, na bado tunaamini mtu fulani anaweza kumpa ushauri magufuli utakaotatua tatizo lolote hapa tz wakati kwa miaka kumi alishindwa kujishauri yeye mwenyewe. wakati mwingine huwa nazima hata tv akitokea mtu anayenitonesha kidonda.
 
Tofautisha marais waliofuatia na Mwalimu ...mwalimu aliondoka madarakani ili aweze kuandaa utamaduni mzuri wa succession kwa nchi ambao hadi leo tunaufuata ....wa kuheshimu mihula na kadhalika ......hivyo alichokuwa akikifanya mwalimu ni kuandaa misingi imara ....na technically Rais alietawala baada ya Mwalimu ..mzee mwinyi na mkapa walikuwa wakiongoza kwa kivuli cha Mwalimu kwa mambo mengi .........yeye akiwa kama baba ......
Mwalimu kafariki nafasi yake kwenye mioyo ya watu haiwezi kuzibwa kwa Mwinyi au Mkapa kutaka kuvaa viatu vyake .....kwa kuwa wote ni wanafunzi wake
Sawa mkuu lakini argument yako ni sawa na Professor anavyostaafu na kuwaacha vijana ndio wameanza degree ya kwanza haina maana kuwa unakuwa mwisho wa 'mihadhara'.
Mnaanza kwa kuwasikiliza 'lecturer' waliopo hata kama wana kadgree kamoja mapaka pale watakapopanda nao kuwa maprofesa pia. Mtihani unabaki kwa wasikilizaji ambao ndio watafanya kazi ya kuwapima na kuwalinganisha kuwa kama Mwalimu alikuwa 75% basi wenyewe walau wanafikia 25% au vinginevyo na si kukaa kimya!
Hoja yangu hapa ni unafiki na hii inaonekana kuwa sera ya ccm kama alivyotanabaisha JPM mwenyewe siku 'alipochaguliwa'. Ni kuwa majipu mengi hayajatokea kwa bahati mbaya bali yalitengenezwa katika harakati za kujinufaisha binafsi. Sio ajabu hata wale walio prove failure walipachikwa vyeo hadi dakika 5 za kumalizia kipindi cha miaka 10 kwa kigezo kwamba JPM asingeweza kutengua uteuzi wao.
Nawasikitikia wanaoendelea kuwaamini watu wa aina hii!
 
Ujumbe wa Balozi wa Uingereza kwa JPM umehitaji JPM kuteta na JK
 
JK ni Mwenyekiti wa CCM, chama ambacho kimeshinda uchaguzi na kinashika dola chini ya Rais Magufuli. Hakuna cha ajabu hapo
Ajabu ipo, ikulu sio mali ya chama wala si ukumbi wa mikutano ama vikao vya chama!!
 
Kikwete ndo mwenyekiti wa CCM Taifa, labda Magu kazidisha fukuza fukuza na kuwabana wala rushwa. Amekumbushwa kuwa siyo sera ya chama,vinginevyo naye Magu atumbuliwe na CCM. Inawezekana amekwenda kuomba permit kwenda nje...ulaya/marekani/mashariki ya kati.
 
Kwa mazingira marahisi tuu, magufuli anaweza kumpiga mtu stop kisa anauza Sembe/ Dona?

Asante kwa majibu mazuri ,nnayaunganisha na operation iliyoanzishwa kwa watumiaji/wauzaji na.waingizaji wa dawa za kulevya..
 
Kwa ustaarabu kabisa JK hatakiwi kurudi rudi Ikulu
hivi pale aliacha nini?. Kama ni jambo linalohusu CCM ni vema akamuita Mhe. Rais pale Ikulu Ndogo kuliko kurudi rudi Ikulu. Mimi nilistaafu miaka michache iliyopita, mpaka leo sijakanyaga ile ofisi tena.
 
Kila likitumbuliwa jipu anapiga hodi magogoni ili asiguswe
 
Sipendezwi na hii Tabia ya Kikwete kwenda kwenda Ikulu kila Mwezi, yeye mbona hakutaka Ushauri wa Mkapa Enzi zake?

Yeye nani awe bingwa wa Ushauri kwa Magufuli?

Nyerere alishauriwa na nani Enzi hizo?

Kwa Ugoro na Uozo alioukuta Magufuli, JK anatakiwa aende kujificha mahali angalau miaka miwili tusimwone usoni. Ni mnafiki wa Kutosha. Hivi Mliona alivyocheka kwa Kebehi akimkabidhi Magufuli "Mwongozo" Nilijua tu kuwa walitaka Kumtumia awarudishe madarakani waendelee na Maovu yao. Mwoombeeni sana Magufuli, Na Usione JK akitabasamu Ni Jeuri wa Kutupa!

Sikiliza Kwa Makini Kicheko na Maneno aliyosema JK juu ya kutatua matatizo. Yaani Kilikuwa Ni Kicheko cha Kebehi ya wazi.
 
Back
Top Bottom