JK mara ya pili kumtembelea Magufuli

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,011
2,181
Nahesabu ni mara ngapi rais mstaafu amemtembelea rais aliyeko madarakani. Sihitaji kujua anatafuta nini lakini siyo dalili nzuri kwa mstaafu kurudi rudi ofisi uliyotoka. Kwa ajira zingine utaitwa mtu unayesikitika kuacha kazi.

JK alipoingia madarakani mbona hakutemebelewa na Mkapa mara nyingi kwa muda mfupi kama huu? Hakuna anayetaka kuingiliwa ktk utawala wake.
 
Watu walizoea vya kunyonga. Hata kama ni ushauri haoni kama utakuwa hauna maana kwani haya majipu ni kwa mujibu wa utendaji wake mbovu? Si vyema kama ulifanya chini ya kiwango kulazimisha kwenda kwenye ofisi hiyo kujifanya kutoa ushauri ama mazungumzo ya mara kwa mara. Sisi kwetu wananchi tunaona kama ni safari zenye nia ovu.
 
Anaenda kuombea jamaa zake wasishugulikiwe kwa madai kuwa walisaidia kuchangia kampeni za magufuli kuingia ikulu.Bahati mbaya ngosha hajali,akitoa mguu tu anaendelea na jina linalofuata kwenye list..
 
JK ni Mwenyekiti wa CCM, chama ambacho kimeshinda uchaguzi na kinashika dola chini ya Rais Magufuli. Hakuna cha ajabu hapo

Hilo halina ubishi, lakini yeye kwenye nafasi hiyo ya ikulu aliotesha majipu, kama yeye ni sehemu ya uozo uliopo ambao ndio sasa unaisumbua serekali ana kipi kipya? Hapo ikulu sio kijiwe cha story, alishindwa nini huo ushauri kuutumia yeye tena akiwa Rais na mwenyekiti wa chama kwa zaidi ya miaka 9? Ajirekebishe bwana, anaweza kutoa ushauri hata kwa simu au e-mail. Labda asema simu wala e-mail zake hajibiwi. na kama ni mwenyekiti wa chama kila siku ccm inajinasibu kwa kuwa na ofisi nzuri, si wakafanyie kwenye ofisi za chama ambapo yeye ni mwenyekiti?
 
Nahesabu ni mara ngapi rais mstaafu amemtembelea rais aliyeko madarakani. Sihitaji kujua anatafuta nini lakini siyo dalili nzuri kwa mstaafu kurudi rudi ofisi uliyotoka. Kwa ajira zingine utaitwa mtu unayesikitika kuacha kazi.

JK alipoingia madarakani mbona hakutemebelewa na Mkapa mara nyingi kwa muda mfupi kama huu? Hakuna anayetaka kuingiliwa ktk utawala wake.

Waingereza wana kamsemo kao kaendako hivi: "Out of site, out of mind!"; yawezekana JK anakatilia maanani sana kamsemo hako; kwa hiyo anajitahidi kujipitishapitisha ikulu mara kwa mara ili JPM asije kumsahau akamtumbu jumla kama jini lililosahaulika!
The guilty are always afraid; tumuache aendelee kujipilikicha.
 
JK ni Mwenyekiti wa CCM, chama ambacho kimeshinda uchaguzi na kinashika dola chini ya Rais Magufuli. Hakuna cha ajabu hapo

Nawe una matatizo. Yaani anapeleka ajenda za chama kwa rais wa nchi ambaye hana nafasi yoyote kwenye chama hicho? Walipojieleza ktk mchakato wao pale Dom, kila mjumbe alijidai hana swali kwa wagombea, leo hii anaanza kazi maswali kila siku.

Yeye alipoingia Mkapa alikuwa Mwenyekiti. Alirudi rudi kumukumbusha mambo ya chama? Kuna kasoro hapo. Akae kwake ili kama anahitajika atatembelewa Lumumba. Nyerere alikuwa anafuatwa Butiama.
 
Nasikia juzi kuna mtu ameitwa Ikulu , akaambiwa akafunge yale maduka yake ya Unga yaliyoko Kariakoo....

Anajijua hiyo jamaa....manake hata humu yupo.....

Na ndo jk anajaribu kwenda kusawazisha......

M16 kazini..

Mkuu ni unga unao uzungumzia ni ule wa gharama ?
 
Nnaona utumbuaji wa majipu unatakiwa kwenda na miongozo , unafiki mkubwa kabisa hasa nikilinganisha na nidhamu ya uoga aliyo ionesha JPM mbele ya Jk ktk besidei ya CCM!!!!...
 
Waingereza wana kamsemo kao kaendako hivi: "Out of site, out of mind!"; yawezekana JK anakatilia maanani sana kamsemo hako; kwa hiyo anajitahidi kujipitishapitisha ikulu mara kwa mara ili JPM asije kumsahau akamtumbu jumla kama jini lililosahaulika!
The guilty are always afraid; tumuache aendelee kujipilikicha.
Hao wazungu hawakumaanisha hiyo "site" yako.
 
Nasikia juzi kuna mtu ameitwa Ikulu , akaambiwa akafunge yale maduka yake ya Unga yaliyoko Kariakoo....

Anajijua hiyo jamaa....manake hata humu yupo.....

Na ndo jk anajaribu kwenda kusawazisha......

M16 kazini..

Mkuu unaonekana kujua jambo Fulani kuhusu hiki kitu, hebu funguka Zaidi...!

Ni Unga huu Adimu au ni unga wa kawaida?
 
Ukiondoa Mwalimu, naona hawa viongozi wengine wana ajenda zisizoeleweka au unafiki wa kupindukia.
Sijawahi kumsikia Mzee Mwinyi au Njomba akiitisha press conference nyumbani kwake kuelezea hali ya mambo inavyoenda hata kwa suala tete kama la Zanzibar. Na JK anaonekana kuchukua muelekeo huo huo.
Hiwezekani haya majipu yote yanayotumbuliwa wakati wa 'uotaji' wake hawa wastaafu hawakuwahi kuyaona. Na kama kweli hawakuwahi kuyaona basi hawatufai na kama waliyaona na kukaa kimya tuwajue ndiyo mwendelezo wa majipu!
 
Sipendezwi na hii Tabia ya Kikwete kwenda kwenda Ikulu kila Mwezi, yeye mbona hakutaka Ushauri wa Mkapa Enzi zake?

Yeye nani awe bingwa wa Ushauri kwa Magufuli?

Nyerere alishauriwa na nani Enzi hizo?
 
Back
Top Bottom