JK: Mafisadi hatutawaonea haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Mafisadi hatutawaonea haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Superman, Apr 24, 2011.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Rais JK, leo akiongea katika Tamasha la Muziki wa Injili liliohusisha vikundi vya kwaya toka nchi mbalimbali alisema:

  "Katika kushughulikia swala la mafisadi, haki itatendeka na hawatamuonea haya mtu yeyote"

  Source: ITV News Bulletin of 8.00 PM

  [​IMG]

  Msafara wa Rais Dr. Jakaya Kikwete ukiwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambako alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka linaloandaliwa kila mwaka na kampuni ya Msama Promotion chini ya Mwenyekiti Alex Msama. Tamasha hilo limekutanisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka nchi za Afrika Mashariki na maziwa makuu kama vile Zambia DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Tanzania.

  Picha: Jiachie Blog​

  Update:

  RAIS Jakaya Kikwete amesema amepata moyo mpya wa kuendeleza kazi ya kujivua gamba na yeye na wenzake watajitahidi kuifanya kazi hiyo kwa haki bila kumwonea mtu. Alisema alitangaza tangu Februari mwaka huu kuwa CCM itajivua gamba na sasa wameanza kuifanya kazi hiyo ingawa watu wengine wameanza kumtupia lawama Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye aliyekuwepo katika tamasha hilo.

  Kabla ya kutoa kauli hiyo katika Tamasha hilo la Pasaka, lililofanyika mjini Dar es Salaam, Askofu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Onesmo Ndegi, alisema hatua ya kujivua gamba inayochukuliwa na CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete ina mkono wa Mungu. Askofu Ndegi alisema sherehe za Pasaka mwaka huu ni maalumu kwa kuwa ni mwaka ambao Tanzania itaadhimisha miaka 50 tangu Uhuru ambayo katika Ukristo inaitwa Jubilee na maana yake ni kuweka kitu huru ama kukiondoa katika mateso.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Mungu amempa ujasiri Rais Kikwete wa kujivua gamba, kitendo ambacho CCM ilikianza hivi karibuni kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya viongozi wake wa juu. “Ujasiri wa Rais wetu ni ujasiri aliopewa na Mwenyezi Mungu pamoja na dua tunazomwombea, tunaomba kujivua gamba huko kuwe kwa ukweli na kusiishie hapo tu,” alisema Askofu Ndegi.

  Baada ya kumaliza kusema hayo, Askofu huyo aliomba maaskofu wengine waliokuwepo ukumbini kumwekea mikono Rais sehemu waliko na kumwombea dua ya kumpa ulinzi, ujasiri na hekina katika uongozi wake.

  Lakini Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani nchini na kuwataka wananchi kuvumiliana baina ya watu wa dini mbalimbali na kutowasikiliza watu wanaohubiri habari za udini kwa lengo la kutaka kuleta mafarakano nchini. Tamasha hilo ambalo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, lililenga kuchangisha fedha za kusaidia yatima, watu wenye ulemavu na mahitaji kwa wanawake wasiojiweza.

  HabariLeo
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Ngoma inogile!

  Inawezekana JK akafanya kweli kama alivyosisitiza?

  Anaposema "Haki Itatendeka" ana maana gani? isije ikawa ni kiini macho.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,946
  Trophy Points: 280
  kiini macho JK hawezi kumgusa Lowasa kirahisi, ndio maana hata zile barua hazijatumwa mpka sasa hivi .
   
 4. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Issue nyingine; amefurahishwa sana na tamasha hilo kwamba uwepo wa watu wa dini mbalimbali na kusema hicho ni kielelezo kuwa Umoja wetu na mshikamano wetu bila kubagua dini.

  Alisema yeye mwenyewe katika familia yake ana ndugu wa kristo na waislamu na wanaishi vizuri. Pia alisema baada ya baba yake kufariki wao walilelewa na Baba yao waliokabidhiwa ambaye ni Mkristo Msabato SDA.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JK bwana anafurahisha sana mambo yake ...
   
 6. S

  Simon B james Member

  #6
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeye mwenyewe ametajwa kwenye orodha ya mafisadi basi aanze kujitendea haki yeye la sivyo anadanganya wajinga. Ama kweli wajinga ndo waliwao jwani huyu Kikwete si ndiye aliwa safisha mafisadi wakati wa uchaguzi
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Ivuga, najua hizo ni habari za magazeti Nipashe in particular. Si vibaya kuvuta subira na kuona what will happen baada ya haya mapumziko. So far source yetu haiko available na hakuna kitu significant jana na leo zaidi ya hii info ya JK.
   
 8. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kikwete aachane na umbea wa kupoteza muda eti kupambana na mafisadi? wote ni wezi nasema woote.
  Mi namshauri aipe hiyo kazi taasisi husika ya rushwa, yeye achape kazi kama enzi zile akiwa na mwenzake Lowassa, walikuwa moto kweli kweli.
  hizi habari za kumpotezea muda rais tu.
   
 9. LivingBody

  LivingBody Senior Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunasubili utekelezaji kwani mafisadi wako wengi mno.
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Yeye mwenye ni fisadi, aanze kujishughilikia yeye mwenye kwanza kwa kuwa yupo kwenye list of shame aliyoitaja Rais dr.Slaa tena anacheza no.11 Huyu Fisadi Kikwete, na hizo barua wanazopeana je na yeye huyu Fisadi Papa Kikwete atapewa
   
 11. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135


  Hii data, tumekuwa tunaitafuta sana...!!

  Jk anaonekana waziwazi ..ana incomplete realtionship with father figer!

  ... Kwa namana fulani.. Baba yake kutokuwepo kulimpelekea misuguanao fulani ambayo ...leo inamfanya kuwa na CHARACTER!! aliyokuwa nayo
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Haki itatendeka tu endapo na yeye ataandikiwa barua vinginevyo itakuwa uonevu.
   
 13. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kautoa ujarisi huo wapi na lini.

  JK kama rais wa tanzania serikali yake imewashtaki Mramba na yona. Lakini JK huyo huyo kama mwenyekitu wa CCM kashindwa kumwambia mramba kaa pembeni kwenye ubunge kwa chama ninachoongoza.

  JK kama rais serikali yake imemchunguza chenge juu ya utata vijisenti vyake na kuhusika na ufisadi wa rada. hakuna asiyeua UK kufunga jalda la kesi ile sio uhalaai wa cheg kutokua na hatia. JK huyo huyo kashindwa si tu kumshatiki chenge lakini hata kumzuia asigombee ubunge

  Sasa kama hata ambao kwake ni dagaa kawashindwa sasa kina EL na RA atawaweza au ataendelea kufanya maigizo ya kudeal na kina liyumba

  EL kuwa pembeni ni msaada ulifanywa na Bunge na sio ujasiri wa . Ndio kusema Jk anategema msaada wa Nape na mkama na yeye mwenyewe hana ujasiri wa wa kuwatosa. Je JK hajui mamlaka na nguvu ya rais na mwenyeiti wa chama.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,946
  Trophy Points: 280
  kwani baba yao aliwaacha wakiwa na umri wa miaka mingapi?
   
 15. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kwa nini umefikiria hivyo?

  Can u tell us more Mkuu?
   
 16. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Unapokuwa rais wa nchi hiyo ni issue nyingine japo na yeye ni fisadi alikuwa ana uwezo na nafasi ya kujisafisha kwa kuwakomalia mafisadi wenzake. nakuwaambia no michezo hii ife. watamshangaa lakini ukiwa rais ndo hivyo uko abovethe law. taizo la JK hasomi nyakati . anatka kuendeleza sana walizofanya five or ten yars back.

  Tatizo ni yeye kuwa above the law na kutaka kendelea kula na mafisadi. JK anauwezo wa k ung'arisha nyota yake kwa kufanya vitu vichache sana. La sivyo kwa madcho ya watanzania anaandika file baya kwake, kwa chama chake na hata kwa familia yake.

  Bosi wa TAKUKURU Wikialeaks cables alinukuliwa akisema kuwa JK ni kikwazo. Anachotakiwa kuwaambia washikaji kuwa nimejitahidi kuwatetea na kuwalinda nimeshindwa . Kwa manufaa ya nchi yangu, uzalendo na familia wote nawapeleka ukonga.

  Kwa mtu aliyepita jeshini sio kazi kubwa lakini Jk anashangaza anakosa kaujasiri ka geshini. teh teh
   
 17. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Unafikiri suluhisho mwafaka lingekuwa ni lipi hasa ikizingatiwa kuwa "amechaguliwa" kuwa Rais recently?
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  JK ni msanii tu ana mamlaka makubwa lakini hajui kuyatumia vizuri subiri wenzake wayapate, usanii wake ulidhihirika siku ya NEC badala ya kuwataja majina kama M/kiti akasikika akisema anayewajua si awataje utadhani yeye alikuwa hawajui.
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Apr 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hata Obama na Clinton hawakulelewa na baba zao lakini waliongoza na wanaongoza vizuri.
   
 20. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu, taasisi gani husika itakayoweza kufanya hiyo kazi kwa uadilifu ambayo RACHEL hawawezi ku-control? Why?
   
Loading...