Kumbukumbu zangu zinanionesha kwamba mara ya mwisho ilikuwa kipindi cha kampeni na alifika saa 12 jioni baada ya kusubiriwa tangu saa 5 asubuhi. Aliishia kumkabidhi kadi ya chama Nakaaya Sumari hapo uwanjani. Na kwakuwa muda ulikuwa umekwisha, alimwacha Batilda ajinadi na mkutano kufungwa. Ni zaidi ya mwaka sasa anarudi arusha baada ya kushindwa vibaya na kuamua hata kuhamisha watoto shule. Arusha ambayo hakuwahi kumaliza miezi mi 5 bila kufika kwenye awamu yake ya kwanza!
Anyway, labda surua ni tatizo sana Arusha ndio maana ameamua kuja kufanyia huku! Karibu tena Arusha.
Angalizo langu ni kwa polisi. Demokrasia ya Arusha imekuwa mno. Asishangae kukutana na mabango ya wananchi wakielezea hisia zao kuhusu hali ya kiuchumi, kijamii, kielimu, kisiasa nk. Nawaomba tu polisi wawaache watu waeleze hisia zao kwa upole na amani ili kuepusha maafa kwa wana wa Arusha na raisi mwenyewe.
Mwisho ningependa kusahihisha thread title. Nadhani hai"reflect" content. Kikwete sio tu hangurumi bali hawezi kufanya hivyo. Na hawezi kabisa kufanya hivyo Arusha. Wala hataweza kufanya hivyo. Sababu ni kwamba hakubaliki huku na chama chake ni chama cha upinzani hapa jijini. Kwahiyo hana hiyo confidence ya kufanya hivyo hapa! Ataishia tu kuzomewa.
Halafu, Ole Millya ni m/kiti wa uvccm. M/kiti wa ccm mkoa ni Ole Nangoro. Nadhani mleta mada atasahihisha.