JK Kuivunja Sekretariati ya CCM kabla ya 2015?

JK Kuivunja Sekretariati ya CCM kabla ya 2015?

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
5,558
Reaction score
1,462
Wachambuzi na wadadisi wa Mambo wanasema kwamba muda si Mrefu JK ataweza kuivunjilia Mbali Sekretariati Aliyoiunda Dodoma. Sababu ni kwamba Kabla Sekretariati haijaanza Kazi ya Kusafisha Chama Baadhi ya Wajume wanajikuta katika Jukumu kublwa la Kujisafisha wao kwanza. Inaonekana kwamba Badala ya Sekretariati kujikita katika kurejesha Imani ya Wananchi kwa Chama wajumbe wake watakuwa na wakati Mgumu wa Kujibu Tuhuma kama

1. Zakhia Meghji: Huyu alikuwa waziri wa Fedha na alifanikisha Uporaji Mkubwa BOT kupitia Kagoda, Deep Green n.k. Ikumbukwe ni Zakhia Meghji aliyeandika barua kufast Track Malipo ya Kagoda kwa Maelezo kwamba "Ni Suala la Usalama wa Nchi". Sasa huyu anakuwa Mwekahazina wa Chama. Je Sio kwamba amewekwa kwa sababu anajua Loope Holes za BOT na namna ya Kukwapua Pesa za Walipa Kodi?

2. Kinana. Huyu jamaa anatuhumiwa kujihusisha na Meli zinazosafirisha Nyara za Taifa. Ni Juzi tu Meli yake imekamatwa na Pembe za Ndovu. Huyu jamaa ingawa alinekana kama Asset kwa CCM lakini Mara baada ya Kuchaguiliwa tayari ameshakuwa Liability

Je JK atamudu kwenda na Hii Sekretariati mpaka 2015
 
kati ya watu nilikua nawaona ni wasafi ni kinana kumbe jamaa anafanya dili haramu kichizi,kajitetea kuwa kampuni ya kwake ila mzigo si wake anafikiri tz ya leo ni ilee ya 1947.
 
Hiyo ni kama karata ya mwisho ya kukinusuru chama, kama nao hao watapata mrejesho nyuma mbaya basi tayari ule utabiri wa CCM kufa utakuwa umekamilika.

Hebu fikiria kama JK akivunja sekretarieti hiyo atawaweka akina nani??? Wengi wa vijana kama akina Nape na Makamba wanaonekana kama hawawezi kukinusuru chama bila ya uwepo wa nguvu za wakongwe ambao tayari walishachafuka.
 
Natabiri kuvunjwa kwake kutokana na tuhuma za Kinana,MANGULA na Meghji na uzamani wao kutoweza kunusuru chama..KATIBU MKUU WA CCM mwakani atakuwa ajuza Steven Wassira ama Tambwe Hizza
 
mangula kasema watoa rushwa wote watafukuzwa ndani ya 6mnth nani atapona ccm?
Wachambuzi na wadadisi wa
Mambo wanasema kwamba muda si Mrefu JK ataweza kuivunjilia Mbali
Sekretariati Aliyoiunda Dodoma. Sababu ni kwamba Kabla Sekretariati
haijaanza Kazi ya Kusafisha Chama Baadhi ya Wajume wanajikuta katika
Jukumu kublwa la Kujisafisha wao kwanza. Inaonekana kwamba Badala ya
Sekretariati kujikita katika kurejesha Imani ya Wananchi kwa Chama
wajumbe wake watakuwa na wakati Mgumu wa Kujibu Tuhuma kama

1. Zakhia Meghji: Huyu alikuwa waziri wa Fedha na alifanikisha Uporaji
Mkubwa BOT kupitia Kagoda, Deep Green n.k. Ikumbukwe ni Zakhia Meghji
aliyeandika barua kufast Track Malipo ya Kagoda kwa Maelezo kwamba "Ni
Suala la Usalama wa Nchi". Sasa huyu anakuwa Mwekahazina wa Chama. Je
Sio kwamba amewekwa kwa sababu anajua Loope Holes za BOT na namna ya
Kukwapua Pesa za Walipa Kodi?

2. Kinana. Huyu jamaa anatuhumiwa kujihusisha na Meli zinazosafirisha
Nyara za Taifa. Ni Juzi tu Meli yake imekamatwa na Pembe za Ndovu. Huyu
jamaa ingawa alinekana kama Asset kwa CCM lakini Mara baada ya
Kuchaguiliwa tayari ameshakuwa Liability

Je JK atamudu kwenda na Hii Sekretariati mpaka 2015
 
Hivi kumbe ccm hawana hazina ya viongozi bora mpaka wameamua kuweka huu uozo kwenye sekretarieti???
Hakika ccm ni sawa na mbwa anayejisaidia na kula kinyesi chake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
300089_10150318586135942_1905171732_n.jpg
 
Wamepoteza dira kitambo sana kwa kuwakumbatia wala rushwa na watoa rushwa mwenye chaguzi zao. Kunawatu wanajiona ndo wanafaa kuongoza mtanzania kwa sababu wanapesa. JK achana na marafiki wanafiki watakuangusha ucje ukarogwa ukawapa nafasi wakagombea uraisi kwani watakuletea shida ww na Watz wote. Ni Nyoka. Wa ndimi 2
 
kati ya watu nilikua nawaona ni wasafi ni kinana kumbe jamaa anafanya dili haramu kichizi,kajitetea kuwa kampuni ya kwake ila mzigo si wake anafikiri tz ya leo ni ilee ya 1947.

Kinana si mgeni katika uhujumu uchumi Tanzania, ndio moja ya waasisi wa kuhujumu uchumi wa taifa nchini kwa kukwapua pesa za serikali alipokuwa waziri.
 
kati ya watu nilikua nawaona ni wasafi ni kinana kumbe jamaa anafanya dili haramu kichizi,kajitetea kuwa kampuni ya kwake ila mzigo si wake anafikiri tz ya leo ni ilee ya 1947.

Cv ya Kinana kwenye suala la utoroshwaji wa Wanyama Pori Hai na Nyara na uingiaji wa the Arabic-untouchables kwenye mbuga za wanyama hasa wale wa Roliondo ni chafu sana. Niishie hapo kwa leo kubusu mtu huyu.
 
Sidhani kama kuna mtu yeyote msafi ndani ya CCM na akaweza kuwa kiongozi katika level za juu. Maana ili wakuchague kuwaongoza lazima uwe mwenzao katika maswala yao!! Hakuna siku nilitarajia Meghji na Kinana kurejea tena kuwaongoza watanzania maana wote wamekuwa na scandal za kifisadi!!!
 
Uchambuzi wako kame vile umesomea Computer Science halafu umejingiza kwenye siasa.Ila ndo JF ya siku hizi
 
Kikwete amezungumza kweli kuwa rushwa imekidhiri katika uchaguzi zote ndani ya chama chake na nje.afanye kweli sasa tuone.kipindi cha kugombea nec nagu alileta pikipiki na trekta za mikopo na kudai yeye kaleta je hiyo inamamanisha nini hiyo je si mianya ya rushwa kwanini asileta wakati hakuna mchakato wa uchaguzi na kama ni mkopo wa benki kwanni adai yeye kauleta.na kwanini asiboreshe shule za msingi na kusomesha wasio na uwezo yeye huwapa wapiganaji wake pikipiki na kututambia wamepewa bure kwa kazi wanazofanya kama kweli takukuru fanyeni uchunguzi wa kina.na wenye kupewa mkopo kutishiwa wakiweka bendera ya chama kingine kukamatiwa na kunyanganywa hiyo inawanyima uhuru wakopaji
mwambie kikwete alione hilo ndani ya hanang kumejaa rushwa tumekosa imani na mhe.nagu anza na huyo ili wanahanang turudishe imani yetu
 
Upumbavu, Ujinga, Usahaulifu, Woga, Ulalamishi bila kuchukua hatua na mengine yanayo fanana na hayo ndiyo yanaiweka madarakani CCM mpaka leo. Naomba watu, vikundi vya kiraia wenye ufahamu mzuri wa Elimu nzuri ya Uraia watengeneze vijarida na kuvisambaza Tanzania nzima kupitia wauza magazeti, au kama vijarida vya FEMA. Hii itasaidia Wa-TZ kujua hakizao za msingi na nini wanatakiwa kufanya kama Wananchi na Serikali ina wajibu gani katika maisha yao ya kilasiku.
 
Back
Top Bottom