JK, Ki-Moon wateta mgogoro wa Malawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, Ki-Moon wateta mgogoro wa Malawi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Oct 4, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na kujadili pamoja na mambo mengine, mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi.

  Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, imeeleza kuwa viongozi hao walikutana jijini New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu amesifia jitihada za Tanzania katika kupatia suluhu suala hilo.

  “Majuzi nilikutana na Rais Joyce Banda wa Malawi na akanielezea mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa na mazungumzo ambayo nchi zenu mbili zinafanya ili kupata ufumbuzi wa amani. Hii ndiyo njia sahihi na UN inaunga mkono njia hiyo,” alisema Ban Ki Moon.

  Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alimweleza Katibu Mkuu huyo kuwa Tanzania bado inaamini kuwa njia sahihi na ya maelewano zaidi ni kutafuta ufumbuzi wa mvutano huo wa mpaka kwa njia ya mazungumzo.

  “Wazo la awali la kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili la miaka mingi sana lilitokana na Rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika ambaye aliniandikia barua ya kutaka nchi zetu zianze mazungumzo kuhusu mzozo huo. Nasi tulikubali. Hivyo, ndivyo tulivyoanza kuzungumza,” alisema Rais Kikwete

  Aliendelea:“Mpaka kati ya Malawi na Msumbiji kwenye ziwa hilohilo, umekuwa katikati ya ziwa tangu mwaka 1954 wakati nchi hizo zilipokubaliana kusahihisha makosa ya kuuweka mpaka huo nje ya ziwa. Mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye mto mkubwa zaidi unaoingiza maji katika Ziwa Nyasa uko katikati ya mto wenyewe.”

  Rais Kikwete alibainisha kuwa kila mahali ambako nchi zinatenganishwa na maji, mpaka unakuwa katikati ya nchi. “Sisi tunadhani hata kwenye mpaka wetu na Malawi kwenye Ziwa Nyasa ni lazima uwe katikati ya ziwa,” alisema Rais Kikwete na kuendelea:

  “Katika hali ya sasa wananchi wetu wanapokunywa maji ya Ziwa Nyasa wanakunywa maji ya Malawi, kila watu wetu wanaposafiri ndani ya ziwa kufanya shughuli zao wanasafiri kwenye maji ya Malawi. Hili ni jambo linalohitaji majadiliano ya kuliweka vizuri.”

  Msimamo wa Malawi

  Mazungumzo ya viongozi hao yamekuja huku Rais wa Malawi, Joyce Banda akiwa ametangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo kwa madai kuwa Tanzania imechukua hatua korofi kwa kuchapisha ramani inayoonyesha kuwa mpaka wa ziwa hilo uko katikati.

  Rais Banda alitangaza uamuzi huo wakati alipokuwa akilihutubia taifa hilo baada ya kurejea nchini kwake akitokea Umoja wa Mataifa (UN) alikokuwa kwa ziara ya kikazi.

  "Wakati naondoka kwenda UN nilidhani suala la mpaka wa Malawi na Tanzania lilikuwa likihitaji mazungumzo, lakini nikiwa huko nikasikia kwamba Tanzania imezindua ramani mpya inayogusa ziwa hilo," alisema Banda na kuendelea;

  "Baada ya hatua hiyo wavuvi wa Malawi wameanza kufukuzwa ufukweni na boti zetu zinaondolewa Tanzania. Ni suala zito sasa ambalo tunatakiwa kuchukua hatua nyingine," alisema.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa Tanzania kwa kauli hiyo ya Malawi alisema: "Jana sikumpata Waziri (Membe) kupata ushauri wake, ila ninaendelea kuwasiliana na Balozi wetu Tanzania wa Malawi aifuatilie kauli hiyo kujua kama ni kweli imetolewa na Rais."

  Katibu Mku huyo alisema ikithibitika kuwa ni kauli ya Rais Banda, atawasilina na Waziri Membe ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi ili baadaye ajadiliane na Rais Kikwete wakiwa huko Canada.

  Katika hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Septemba, Rais Jakaya Kikwete alielezea hatua zilizochukuliwa na Serikali yake kushughulikia mzozo huo kuwa tume ya pamoja ilipanga kukutana Septemba 10 hadi 15 mwaka huu, lakini mkutano huo haukufanyika kwa maombi ya Serikali ya Malawi.
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanateta nini wakati Mama wa Shoka Joyce Banda ameshasema Hakuna Mjadala wa mazungumzo kuhusu Mpaka!The chapter closed.:eyebrows:

  Source: BBC focus Africa.
   
 3. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  Kama hataki mazungumzo anataka nini? Bila shaka vita,inaonekana huyu mama washauri wake wanamchanganya.!
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Expectations zake ni kubwa kuliko reality.
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  JK anaishi kwa kudhani hahhahahhahah hili ziwa tumepolwa UNADHANI MHESHIMIWA JK
   
 6. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,251
  Trophy Points: 280
  Mwanaume msimamo.
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  Aliyezindua ramani mpya inayogusa ziwa hili ndo anashauriwa vibaya.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 8. M

  MR.PRESIDENT Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani bado mnazungumzia kuhusu mpaka ipo wazi ziwa 100% ni la malawi.Kinachofanywa na JK ni kupoteza muda tu.Kama hutaki subili sisi wanasheria tunajua mchezo wote
   
 9. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  DM, kuzindua ramani mpya ni jambo la kawaida mno, manake TZ sasa ina Mikoa na Wilaya mpya. Sasa katika kuliweka hilo ulitaka mpaka usiweke, na kama ingekuwa hivyo mbona ramani zao wao wanaweka mpaka mwisho wa maji?. Pia tokea nakuwa ramani zinazotengenezwa na TZ zina mpaka katikati ya maji, hivyo haiwezekani eti sasa tuzindue ramani mpya tusiweke huo mpaka.
   
 10. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  "Katibu Mku huyo alisema ikithibitika kuwa ni kauli ya Rais Banda, atawasilina na Waziri Membe ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi ili baadaye ajadiliane na Rais Kikwete wakiwa huko Canada"


  Duuu wameamua kuendesha nchi tokea ughaibuni sasa
   
 11. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,782
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Kwahili lazima tuwe na JK bega kwa bega nadhani ata kuonana na Ban-kimoon ni ktk hatua za kujaribu kumlobby kwani kwa hali inavyoonekana ziwa sio letu ata mpaka haupiti katikati ila sisi hoja yetu na ambayo ni ya msingi ni kua km ziwa lote ni la Malawi basi ata na sehemu ya nchi kavu ya TZ inaweza kudaiwa na incase maji yamepungua basi na sisi tutaongeza mpaka...Cha msingi ni kumsaport kwa hali yote kwani ukitembelea NYASA LAND NEWS utaona jinsi wamalawi walivyo na umoja na kumpa nguvu rais wao...The only option left on the table is good deplomacy in international arena otherwise ziwa hatuna
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  jenga hoja, acha hofu!
  Ramani yetu huonyesha mpaka upo katikati ya ziwa, kwa mfano huo, ikatokea kenya watoe ramani inayoonyesha mlima kilimanjaro upo kenya sisi tukinyamaza bila kuitangazia dunia kuwa kenya wanaleta chokochoko ya kuivamia nchi yetu kwa kubadili mipaka, tutakuwa tumekubaliana na mtizamo wa kenya.

  Ukweli unabaki kuwa mpaka wa tanzania na malawi unapita katikati ta ziwa nyasa.
   
 13. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,370
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Nina hamu navita kweli.
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  waingereza wanaipenda sana Malawi kwa sasa na kwa namna sera ya mambo ya nje David Cameron ilivyo ikiwa ni pamoja na jamaa wa Lib Democrat ni sharti Tanzania iwe makini na namna inavyotatua mgogoro wa mpaka, Malawi kupitia kwa mama Banda ni kipenzi ch wakubwa kwa sasa, JK asipokua makini mgogoro wa Mapaka utaiondoa CCM madarakani kwa Bunduki kwa Nchi ambayo haina umoja tena, chuki za kisiasa na chokochoko za kidini zilizotamaraki kwa msaada wa viongozi wa dini na siasa, hivyo watanzania si wamoja tena.
   
 15. s

  swrc JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli uko serious?
   
 16. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...karibu Syria mkuu...
   
 17. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Natamani Iron lady Joyce banda angekuwa rais wa Tanzania. Huyu mwanamama ni jasiri sana angetusaidia kuvunja mikataba ya kifisadi ya madini,gesi,mafuta,uranium.
   
 18. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu MAMA anaweza kuwa na hoja gani ya msingi kuhusu utata wa kuligawa ziwa katikati inapokuja suala la mpaka kati ya Malawi na Msumbiji, alafu ziwa hilo hilo upande wa Tanzania na Malawi anasema eti "ziwa lote ni mali ya MALAWI!"

  Wamalawi wanajisumbua bure wasifikili wanaweza kupata support katika suala hilo - watapata mataifa machache wazabazabina ambao walikuwa wanashirikiana nao kupinga ukombozi kusini mwa Africa kwa ku-support RENAMO na SAVIMBI, sihajabu ndio wanachangia kuwapa kichwa Wamalawi; swali ni je pakifumuka vita watakuja kuwasaidia?
   
 19. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Kwa nini mpaka huko katikati ya ziwa Nyasa upande wa Msumbiji na Malawi - kumbuka marekebisho hayo yalifanyika mwaka 1956 kati ya wakoloni wa Kireno na Waingereza, kwa nini Waingereza hao hao waliacha kurekebisha mpaka kati ya Tanganyika na Malawi; actually nilipo kuwa mdogo ramani ya Tanzania tulikuwa tunachora mpaka ukiwa katikati ya ziwa Nyasa. Kitu kingine wanaweza kutuonyesha ramani yoyote duniani inaonyesha kwamba nchi mbili zikiwa zinapakana na ziwa moja basi majawapo ya nchi hiyo inapewa umiliki wa ziwa na kuacha nyingine kwenye mataa. Chukulia mfano wa Lake Tanganyika, Victoria, Albert, Lake Superior nk.
   
 20. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilipokuwa nasoma darasa la nne mwaka wa sitini, ramani ya Tanganyika enzi hizo mpaka ulikuwa katikati ya ziwa Nyasa halikuitwa Malawi. Nchi zote zilikuwa hazijapata uhuru sasa ni nani aliyebadilisha mpaka huo? By the way sheria ya kimataifa kuhusu littoral waters inasemaje? Wanasheria tuambieni. Kama taifa tumuunge rais mkono.
   
Loading...