JK ilikua atimukie CHADEMA: Absalom Kibanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ilikua atimukie CHADEMA: Absalom Kibanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WAFU FM, Nov 25, 2011.

 1. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  JK wakane, usiwapuuze CHADEMA

  Absalom Kibanda
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] NILIJIPA fursa ya kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia kwa wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Dar es Salaam Ijumaa ya wiki iliyopita.

  Iwe ni kwa mtazamo wake binafsi au kwa ushauri wa wengine, uamuzi wake wa kukutana na wazee na kutoa maelezo kuhusu masuala kadha wa kadha yanayolikabili taifa katika siku za hivi karibuni ulikuwa ni wa msingi.
  Ni jambo la bahati mbaya kwamba, aliamua kukutana na wazee na siyo wahariri na wakuu wa vyombo vya habari akijua kwa uhakika kuwa, mkutano huo ungempa fursa ya kutoa hotuba pasipo kukabiliana na changamoto za maswali mepesi na magumu.

  Kwa kiongozi asiye na uwezo wa kujenga hoja thabiti na aliyekosa kipaji cha kujibu maswali kwa ufasaha na kwa weledi, uamuzi wake wa kuwahutubia wazee wa CCM na si wahariri ulikidhi matarajio yake binafsi na viongozi wenzake serikalini.
  Ni dhahiri pia kwamba, kwa wadadisi wa mambo, utaratibu alioutumia wa kuzungumza na wazee unaweza kuchukuliwa kama mkakati mahususi wa kukwepa maswali na changamoto nyingine za kihoja kutoka kwa wanahabari wenye mitazamo na miguso tofauti.

  Pasipo kujali ukinzani huo wa kimtazamo, bado uamuzi wa Kikwete kuona haja ya kuzungumzia masuala ya kitaifa ambayo yamekuwa yakigusa hisia na maisha ya wananchi moja kwa moja ulikuwa ni wa kimsingi.
  Binafsi niliguswa kwa maana ya kufikirishwa na maelezo aliyoyatoa kuhusu namna anavyouona mchakato wa mabadiliko ya katiba na hatua ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa NCCR Mageuzi kuupinga na pengine kuususa ndani ya bunge.

  Ninakubaliana kwa asilimia 100 na uamuzi wa Rais Kikwete wa kutilia shaka kiwango cha ustahimilivu kilichoonyeshwa na wabunge wa vyama hivyo viwili vya upinzani hususan katika masuala yanayohitaji mijadala ya kidemokrasia na ushawishi wa nguvu ya hoja. Kama nilivyosema katika safu hii wiki iliyopita, nilisononeshwa na hatua ya wabunge wa CHADEMA na wale wa NCCR-Mageuzi kuamua kutoka nje ya Bunge wakipinga kile ambacho walikitafsiri kuwa ni hatua ya Spika wa Bunge kuwaburuza na kubeba maslahi ya chama chake.

  Ni wazi kwamba, hatua ya wapinzani hao kususa ndiyo iliyompa fursa Rais Kikwete kupata ujasiri wa kuhoji kuhusu kiwango cha ustahimilivu na utayari wa wabunge wa CHADEMA kusikiliza mawazo au maoni ambayo hawakubaliani nayo.
  Lakini pengine jambo baya zaidi katika hili ni kwamba, hatua ya wabunge hao wa upinzani kususa mjadala wa muswada wa mabadiliko ya katiba ulitoa fursa kwa wabunge wa CCM na wale wa vyama vya CUF waliobakia kuweka kando jambo la msingi na kuanza kuwapiga vijembe vikiwemo vya kipuuzi kabisa wabunge wa CHADEMA.
  Kosa hilo la wabunge wa CHADEMA na wale wa NCCR likasababisha fursa adhimu ya kulijadili jambo nyeti linalogusa maisha ya Watanzania ambalo limepiganiwa kwa nguvu kubwa kwa miaka mingi ikapotea bure.
  Kwa bahati mbaya kwa taifa, ushabiki wa wabunge wa CCM na wale wa CUF katika mjadala mzima wa muswada huo na kosa la msingi la wenzao wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi likazaa mhemuko wa aina ya kipekee katika jamii.
  Nje ya Bunge CHADEMA huku kikitumia ushawishi wa kauli mbiu yake ya nguvu ya umma inayoungwa mkono na wananchi walio wengi, chama hicho kikajijengea uhalali zaidi na kuungwa mkono zaidi kinyume cha matarajio ya wengi.
  Ni wazi kwamba, dalili za wazi za kupwaya kwa mjadala ndani ya Bunge na hatua ya wananchi walio wengi kuonekana wakibebwa kwa maana ya kuunga mkono msimamo na hoja za CHADEMA, ndiyo uliomsukuma Kikwete kuitisha mkutano wa wazee wa CCM Dar es Salaam na kukisuta chama hicho.

  Sina uhakika iwapo, Rais Kikwete ambaye kwa walio wengi anaonekana kuwa kiongozi aliyepwaya na anayeongoza chama kilichozeeka na kuchakaa kifikra alifanikiwa kubadili upepo katika hotuba yake hiyo.
  Pamoja na kuwapo kwa hali hiyo, ni dhahiri kwamba, hotuba hiyo ya Kikwete kama ilivyokuwa kwa vijembe vya wabunge waliojadili muswada wenyewe ilisababisha makada na wapenzi wa CCM na wale wa CUF kuziweka kando hoja za msingi na kurejea katika mstari wa kuvishabikia vyama vyao dhidi ya CHADEMA.
  Kwa upande mwingine hotuba hiyo ya Kikwete kama ilivyokuwa katika muswada wenyewe ilishindwa kutoa majibu yanayojitosheleza kuhusu hoja za wabunge wa CHADEMA kuhusu suala zima linalogusa muungano.
  Kwa staili na historia ile ile ya viongozi wa CCM kuogopa kuuzungumzia na kuutetea muungano katika muktadha wa utaifa wetu, Kikwete akaishia katika kusisitiza tu kwamba ajenda ya kuuvunja haikuwa moja ya masuala ya kuyajadili wakati wa mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba.

  Ni wazi kwamba, katika mazingira ambayo muungano wenyewe una makovu na vidonda vya kuraruliwa na wanasiasa hao hao wakiwamo wale walio ndani ya CCM ambao baadhi yao wanaficha sura yao ndani ya hoja za CHADEMA kwa kuhofia kutimuliwa, majibu ya Kikwete yalikuwa mepesi sana katika kujibu hoja nzito zilizoibuliwa na wapinzani.
  Kwa rais anayetokana na genge la mtandao ambao wakati likimpigania ili atwae uteuzi kwa mara ya kwanza ndani ya CCM mwaka 2005 lilifanya kazi kubwa kuzima na kuipiga vita hoja ya kuufanya urais wa muungano kuwa ni suala la kupokezana kati ya Watanganyika na Wazanzibari msimamo wake kuhusu muungano ni jambo linalotia shaka.
  Upo uwezekano wa wazi na ushahidi wa kihistoria unaoonyesha kwamba, Kikwete kama walivyo wana CCM wenzake anaugua maradhi ya kuogopa kuonekana wasaliti wa ushawishi na hoja za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu muungano.

  Hivi nani hasa hajui kwamba, makada wengi waandamizi wa CCM wanateswa na kivuli cha maneno ya Mwalimu Nyerere ambaye wakati fulani alipata kuuita mfumo wa muungano wa serikali mbili ni sera ya chama hicho tawala na yeyote anayehoji hilo anapaswa kufanya hivyo akiwa nje ya chama hicho.
  Miaka 12 baada ya kifo cha Mwalimu, CCM ya Kikwete imeshindwa kuandaa semina elekezi, midahalo ya wazi au ya ndani ili kuujadili kwa kina mfumo huo wa muungano na kuyaweka katika mizani inayostahili maneno hayo ya Mwalimu.
  Ni wazi kwamba, kwa mtu aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, kuchanganua mambo na kufahamu mifumo ya kitawala duniani kama alivyokuwa Mwalimu, kauli yake ya kuudhalilisha ‘utaifa wetu' hata kuufanya ni sera ya chama chake.

  Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba hata baada ya viongozi wengi ndani ya CCM na wale walio serikalini kutambua kwamba kauli hii ya Baba wa Taifa ilichochea mijadala ya kuhoji kuhusu uhalali wa muungano, hakuna kiongozi yeyote anayetokana na chama hicho aliyewahi kuthubutu kulihoji achilia mbali kulisahihisha.
  Jaribio pekee la CCM kujaribu kuligusa jambo hili lilifanywa miaka miwili au mitatu hivi ya mwisho ya serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi ambayo baada ya kauli hiyo ya Mwalimu Nyerere ilitangaza kwamba sera ya chama hicho ilikuwa ni kutoka katika mfumo wa serikali mbili na kuelekea serikali moja.

  Kwa bahati mbaya sana, kwa sababu ya hofu ya Wazanzibari wengi kuhofia kumezwa na mfumo huo, CCM kwa namna ambayo haijapata kuiweka sawa, iliachana na azma yake hiyo ya kuundwa kwa serikali moja ya muungano tangu wakati huo.
  Udhaifu huo wa kiuongozi ndani ya chama hicho tawala ambao umeendelea kurithiwa ndiyo ambao ulisababisha takriban vyama vyote vya upinzani vijikute vikiingiza katika ilani zao kila nyakati za uchaguzi sera ya serikali tatu katika muungano.
  Kwa namna ya kustaajabisha na inayoeleza unafiki wa kisiasa uliovuka mipaka kwa njia za siri na vificho vigogo wengi wa CCM wamekuwa wakikutana na viongozi wa vyama vya upinzani na kuwahimiza waendelee kushikilia msimamo wa kuhimiza mabadiliko ya mfumo wa muungano.

  Wakati wakifanya hivyo ‘uvunguni mwa vitanda vyao' katika mikutano ya hadhara, viongozi hao wa CCM wamekuwa mabingwa wa kuwaponda kweli kweli wanasiasa wa upinzani wanaohoji kuhusu masuala ya muungano. Huu ni unafiki unaopaswa kukemewa hadharani.

  Katika mazingira ya namna hii, Rais Kikwete aliyetokana na kundi la mtandao ambalo kwao Zanzibar ilikuwa ni shuruti la lazima la kisiasa alipaswa katika hotuba yake na pengine katika zama hizi awe ni kiongozi wa kwanza kuliweka hili bayana na kugoma kuingizwa katika mtego wa kuwashambulia na kuziponda hoja za CHADEMA na NCCR-Mageuzi pasipo kuzisikiliza.

  Ni dhahiri pia kwamba, kwa Kikwete ambaye wapambe wake wa mwaka 2005 na mabingwa wa mkakati wake wa ushindi ndani ya CCM walifikia hatua ya kuwa tayari kuishawishi CHADEMA impokee na kuwa mgombea wake wa urais iwapo chama hicho tawala kingemtema, anapaswa kuwa ni mtu wa mwisho kuzidharau hoja za CHADEMA.
  Lakini pamoja na makosa waliyofanya CHADEMA ndani ya Bunge katika kulipigania suala hili, uzito wa hoja zao kuhusu mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba na hofu yao katika mambo kadhaa yaliyokuwa katika muswada ule, ni sehemu ya mambo mengine muhimu yanayopaswa kumfanya Kikwete aone unyeti wa kuwapa sikio viongozi wa chama hicho cha upinzani ambao sasa wako tayari kukutana naye.

  Mwisho. Kikwete na CHADEMA kwa pamoja na kila mmoja kwa sehemu yake, wanao wajibu wa kutambua kwamba, mzaha wa namna yoyote katika kulishughulikia suala hili ambao leo tunauona kuwa ni turufu ya ushindi wa kisiasa, huko tuendako itakuwa ni hukumu ya kihistoria. Hatuko tayari kusubiri majuto.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  ........busy connecting :A S-confused1: the dots.........
   
 3. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huitaji kwanini walibadir utaratbu kupeana zamu kati ya watanganyika na waunguja! nabashiri Edo kua rais ajae kwa utaratibu huu...
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hii nilishaipata kule Mwanahalisi nikashangaa sana
  ila baada ya kusoma storo na nani waliokutana nao nikaamini
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  edit kidogo mkuu inasumbua kusoma
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  amka kwanza usingizini.
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Si rahisi.
   
 8. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika mazingira ya namna hii, Rais Kikwete aliyetokana na kundi la mtandao ambalo kwao Zanzibar ilikuwa ni shuruti la lazima la kisiasa alipaswa katika hotuba yake na pengine katika zama hizi awe ni kiongozi wa kwanza kuliweka hili bayana na kugoma kuingizwa katika mtego wa kuwashambulia na kuziponda hoja za CHADEMA na NCCR-Mageuzi pasipo kuzisikiliza.

  Ni dhahiri pia kwamba, kwa Kikwete ambaye wapambe wake wa mwaka 2005 na mabingwa wa mkakati wake wa ushindi ndani ya CCM walifikia hatua ya kuwa tayari kuishawishi CHADEMA impokee na kuwa mgombea wake wa urais iwapo chama hicho tawala kingemtema, anapaswa kuwa ni mtu wa mwisho kuzidharau hoja za CHADEMA.
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Duh! nimeshafika nusu, wacha kwanza nimalizie baghia zangu kabla cjaendelea!!!
   
 10. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Hili nalifahamu, kwamba ndilo lililofanya JK apitishwe kuwa mgombea uraisi, baada ya kumwambia Mkapa kwa uwazi kabisa kwamba kama wasingempitisha angehamia upinzani na alikuwa na uhakika wa kushinda. Mkapa akaogopa, akamwambia basi nitakupitisha ila na wewe unilinde utakapokuwa raisi. Wakapeana mkono wa ahadi (kumbuka kauli za JK za mwacheni mzee apumzike mambo yalipomgeukia Mkapa). Zaidi ya hilo ninaloelewa ni kwamba Sitta ndie aliyekuwa "the brain" nyuma ya mkakati huu wa uliomweka Mkapa kwenye hali ngumu kimaamuzi, japo JK, Rostam na Lowasaa walikuja kumtupa Sitta kama ganda la ndizi! Hasira ya Sitta ya sasa imetoka mbali!
   
 11. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Napita tu!
   
 12. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwita25 anapita tu. imemgusa pabaya?
   
 13. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Maskini 6!
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hv ingekuwaje kikwete ANGEKUWA CHADEMA NA UDHAIFU ALIONAO WA KUANGUKA ANGUKA KILA MARA..NA HUKU CHADEMA MAKAMANDA WANATAKIWA KUSHIRIKI MAANDAMANO KILA YANAPOTOKEA! DUH! SIPATI PICHA... SIKU ILE ANGEWEZA KUKESHA NMC HUYU!.. INGEKUWA VP! INGEKUWA VP!
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo huyu jamaa anataka kutudanganya kuwa Chadema wasingetoka nje wabunge wa ccm wangeujadili muswada?! Kumbe basi akili zao zimeshikwa na Chadema!! Na atasemaje kuhusu ule mkutano mwingine wa bunge ambao walibaki wanamjadili na kumtukana Lissu hadi wengine wakaanza kufundisha tafsiri ya majina yake? Mbona Chadema hawakuwa wametoka nje?? Mawazo haya kuwa ccm walishindwa kujadili muswada kwa sababu ya Chadema kutoka nje ni upotoshaji uliopindukia.
   
 16. g

  greenstar JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tusubiri mapinduzi ya kweli? hata CDM sina imani nao.....magamba wana Network ktk vyama vyote hapa nchini......hata sasa EL ametishia kwenda CDM wakiendelea na ajenda ya MAGAMBA..

  Kwa hiyo CHADEMA ni mwavuli wao?

  Natamani CCJ ingesajiliwa tujue ukweli zaidi wa siri ya CCM......Tendwa anajua undani wake ,najinsi kilivyozuiliwa kwa nguvu zote.

  Hata JUKWAA LA KATIBA ni ujanja ujanja wa mafisadi ili nchi isitawalike......hawana msaada wowote.Wananchi acheeni ushabiki wa kisiasa kama mnataka amani .

  Tunaanzisha chama Kipya ambacho kitafanya mapinduzi ya kweli......Tunaomba support yenu muda ukifika.


  :smash:
   
 17. B

  Brother Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh.! Mnaandika page za kubwa utafikiri daily news. Hamjui hata kufupisha habari.
   
 18. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  laisi na sio Rais wa nchi yangu ni JEI KEI anashindwa na mwanangu kufanya maamuzi sasa siwezi kumsikiliza kabisa
   
 19. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAha haha haaaaaa! Mkuu umeifanya siku yangu duh!:eyebrows:
   
 20. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ....Kikwete analikumbuka hilo, ndio maana anamkumbatia Nape na kuona hoja ya ccj sio issue, ila asiwabeze cdm maana Mkapa na chama chake wasingeshtuka angekuwa raisi wa nchi hii kupitia cdm, kwa vile basi shida yake ilikuwa ni urais alikuwa tayari kuingia chama chochote ilimradi afanikiwe hilo; asiwabeze cdm,
   
Loading...