CHADEMA wako makini, hawawezi kujichafua kwa kumkaribisha EL ndani ya chama chao.tusubiri mapinduzi ya kweli? hata CDM sina imani nao.....magamba wana Network ktk vyama vyote hapa nchini......hata sasa EL ametishia kwenda CDM wakiendelea na ajenda ya MAGAMBA..
Kwa hiyo CHADEMA ni mwavuli wao?
Natamani CCJ ingesajiliwa tujue ukweli zaidi wa siri ya CCM......Tendwa anajua undani wake ,najinsi kilivyozuiliwa kwa nguvu zote.
Hata JUKWAA LA KATIBA ni ujanja ujanja wa mafisadi ili nchi isitawalike......hawana msaada wowote.Wananchi acheeni ushabiki wa kisiasa kama mnataka amani .
Tunaanzisha chama Kipya ambacho kitafanya mapinduzi ya kweli......Tunaomba support yenu muda ukifika.
:smash:
CHADEMA wako makini, hawawezi kujichafua kwa kumkaribisha EL ndani ya chama chao.
Hili nalifahamu, kwamba ndilo lililofanya JK apitishwe kuwa mgombea uraisi, baada ya kumwambia Mkapa kwa uwazi kabisa kwamba kama wasingempitisha angehamia upinzani na alikuwa na uhakika wa kushinda. Mkapa akaogopa, akamwambia basi nitakupitisha ila na wewe unilinde utakapokuwa raisi. Wakapeana mkono wa ahadi (kumbuka kauli za JK za mwacheni mzee apumzike mambo yalipomgeukia Mkapa). Zaidi ya hilo ninaloelewa ni kwamba Sitta ndie aliyekuwa "the brain" nyuma ya mkakati huu wa uliomweka Mkapa kwenye hali ngumu kimaamuzi, japo JK, Rostam na Lowasaa walikuja kumtupa Sitta kama ganda la ndizi! Hasira ya Sitta ya sasa imetoka mbali!
Kwa hiyo huyu jamaa anataka kutudanganya kuwa Chadema wasingetoka nje wabunge wa ccm wangeujadili muswada?! Kumbe basi akili zao zimeshikwa na Chadema!! Na atasemaje kuhusu ule mkutano mwingine wa bunge ambao walibaki wanamjadili na kumtukana Lissu hadi wengine wakaanza kufundisha tafsiri ya majina yake? Mbona Chadema hawakuwa wametoka nje?? Mawazo haya kuwa ccm walishindwa kujadili muswada kwa sababu ya Chadema kutoka nje ni upotoshaji uliopindukia.
....Kikwete analikumbuka hilo, ndio maana anamkumbatia Nape na kuona hoja ya ccj sio issue, ila asiwabeze cdm maana Mkapa na chama chake wasingeshtuka angekuwa raisi wa nchi hii kupitia cdm, kwa vile basi shida yake ilikuwa ni urais alikuwa tayari kuingia chama chochote ilimradi afanikiwe hilo; asiwabeze cdm,