JK hujawatendea haki wabunge wa CCM

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,495
113,591
Wanabodi,

Naomba nianze na nilichokisema kuhusu wabunge wapya wa CCM niliobahatika kukutana nao pale bungeni Dodoma November, 2010, ile siku wanaapishwa.
Wanabodi,

Nikiwa hapa Dom, nimebahatika kukutana baadhi ya wabunge wapya wa CCM na wa kambi ya upinzani, kujaribu kufahamiana, sio siri, baadhi yao hawana hata substance ya ni nini kilichowafanya washinde, na viti maalum ndio usiseme kabisa, wengi ni makapi tuu, kama sio vidumu, basi ni kwa ajili ya kutoa huduma na kibinaadamu, na hili litathibitishwa na michango yao kikao cha Januari.!

Leo nilikuwa nafanya mapitio ya nilichokisema miaka miwili iliyopita kuhusu wabunge wa CCM. Nilisema baadhi ya wabunge wapya wa CCM wengi ni makapi tuu, hawana substance!. Hili limethibitishwa na JK, katika kulisuka upya baraza lake, kwenye hao wabunge waliopo, amesaka sana akakuta patupu!, yaani hamna kitu mle!, ndipo akajaribu kuvikombeleza vile vichwa vichache vilivyobakia na kulazimika kujaza nakisi kwa kufanya uteuzi mpya wa wabunge wa kumsaidia.

Jee kuna uwezekano wabunge wa CCM waliopo mjengoni kweli ni makapi, vilaza, ni bure kabisa na hana kitu na hawana jipya lolote la kudeliver hadi kumlazimisha mkuu wa nchi kutafuta vichwa vya maana nje ya wabunge waliopo kwa kukopa (bila kuapishwa) ili ajenge timu yake?!.

Nauliza jee ni kweli JK amekosa kabisa watu wa kumsaidia miongoni mwa wabunge wa CCM kwa sababu waliobakia wote ni vilaza tuu au mule bungeni kuna watu wazuri tuu miongoni mwa wabunge wa CCM bali JK ana lake jambo na hao aliowateua?!.

Pasco.
 
jana rais ametangaza baraza jipya la mawaziri,cha kushangaza kuna watu hawakua wabunge lakini wameteuliwa kuwa wabunge na kupewa wizara.swali langu je,katika wabunge wote wa ccm hakuna msafi au mtu mwenye uwezo wa kua mawaziri ni akina wasira pekeyao? Mpaka atoe mawaziri nje? Filipnjombe, malole,baduel,lusinde,mama malecela
 
Ni ukweli uliowazi most of wabunge wa ccm wana sifa ulozitaja. Hawajui wako bungeni for what, sana sana wanaweza kugonga meza kwa bidii kunapotokea kebehi za kuzomea n.k n.k. Kumbuka hoja ya Tundu Lissu kupinga mswada wa marekebisho ya katiba Nov 2011. Unapokuwa na wabunge wenye elimu ya kindergatten kama Mheshimiwa sana Livingstone Lusinde, proffesor Maji marefu, Jah People na Ma dr feki kibao unategemea kupata result gani??? Hiyo ndiyo CCM bana.
 
Wewe mkaka wa Dodoma habari yako, kwani ameanza jana kjuwazalau wabunge wa ccm hawana jina maalumu jina lao ni lile ambalo nikikwambia nitapigwa ban humu jf. Ila jamaa anawazalau, 1)mswada wa katiba pamoja na makelele yote aliwatosa 2) majadiliano ya juzi waliyokuwa wanaogopa kujadili mwenzao kayasifu 3)hata kama watamg'oa pinda atasifu. JK hana option zaidi ya kuona upepo unaelekea wapi na yeye kuufuata.
 
jana rais ametangaza baraza jipya la mawaziri,cha kushangaza kuna watu hawakua wabunge lakini wameteuliwa kuwa wabunge na kupewa wizara.swali langu je,katika wabunge wote wa ccm hakuna msafi au mtu mwenye uwezo wa kua mawaziri ni akina wasira pekeyao? Mpaka atoe mawaziri nje? Filipnjombe, malole,badue,lusinde,mama malecela

nadhani ulitaka angalau tutabasam ulipomtaja ludinde. lakini si umeona kamchukua amosi makalla!! hii ni ng'anda tatu.
 
Imekula kwao hao manamba wa CCM Kaz yao kupiga makofi kuunga hoja za kijinga . Kama wamechukia ni wakati wao sasa kuunga hoja ya mh Zito ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu
 
hata huyu Dalali Kafumu aliyekuwa katibu mkuu wizara ya Madini naye sijui ni nini hasa tatizo?
 
Brainless thread.
Yaani wewe huyo F-Njombe umemwona dili sana kisa ni viji-kelele vya siku chache tu? Na kwako Lusinde na mitusi yoote na ukichaa (alikiri hadharani kuwa hamnazo) kwako wanafaa kukuongoza? Good for you but not for Tz, and certainly they can't be my leaders anyway!

Saa nyingine watu kama wewe mlistahili mnachopata.
 
Mbunge yoyote wa CCM ambaye hayuko kwenye baraza la Mawaziri basi anatakiwa afiche uso. Kwa week mbili rais na team yake wamekuwa wanasaka mawaziri na sasa ameaona iko lazima kuteuwa wabunge 'wapya'. How 200 na ushee hawafai?
 
Labda hawaamini.
Kweli wengi ni vilaza.
Wengine wapo kuvizia nafasi za juu bila kujua watakachofanya. Hata familia nyumbani kuna wakati mzazi anashindwa kuwaamini watoto wake mwenyewe kwa kuwa anawaafahamu vema, hivyo ndugu au rafiki hutumika.
Kwani wakati inasemwa pia wengi wao ni kundi la "jamaa" na wengi wanapokea amri kutoka kwake.
Wakati mwingine kiashiria kuwa wafanye kazi iliyowapeleka bungeni na si kujipendekeza kwa kuwa wanakivuruga chama zaidi ya kukijenga.

Wengi ni wachumia tumbo tu. Pamoja na kujua ukata uliopo, wanataka posho zaidi na zaidi.

Pia wakati mwingine ni kubadili ladha ya chakula jamani au kusema na nyie njooni muone wenyewe kilichomo.
 
Of Course CCM imeoza.., kwahio huenda ikija damu mpya from outside huenda ikasaidia (ingawa hii sio damu mpya ni wale wale jamaa ila walikuwa reserve..,) tutegemee kasi mpya na zaidi ya yale yale tuliyoyazoea
 
Ukweli nikwamba Jk kawadharau na mimi nawaambia wareact kabisa na wapige kura yakutokuwa na imani hata na Jk
 
jana rais ametangaza baraza jipya la mawaziri,cha kushangaza kuna watu hawakua wabunge lakini wameteuliwa kuwa wabunge na kupewa wizara.swali langu je,katika wabunge wote wa ccm hakuna msafi au mtu mwenye uwezo wa kua mawaziri ni akina wasira pekeyao? Mpaka atoe mawaziri nje? Filipnjombe, malole,baduel,lusinde,mama malecela

ndo manake
 
Sio kila mtu anaweza kuwa mbuge na sio kila mbuge anaweza kuwa waziri, wizzo rais anatambua nn atendalo anawajua kila mbunge na kipaji chake tabia na uelewa kuliko unavyowajua wewe sasa ndugu yangu usimfundishe kazi kwani amekosa washauri mpaka uwe wewe atmeans unataka kusema rais na makamo wake pamoja na waziri mkuu sio bora kuliko wewe. Ukinitukana utakuwa umeshindwa na hoja ukinijibu kwa points utakuwa more great thinker
 
Sio kila mtu anaweza kuwa mbuge na sio kila mbuge anaweza kuwa waziri, wizzo rais anatambua nn atendalo anawajua kila mbunge na kipaji chake tabia na uelewa kuliko unavyowajua wewe sasa ndugu yangu usimfundishe kazi kwani amekosa washauri mpaka uwe wewe atmeans unataka kusema rais na makamo wake pamoja na waziri mkuu sio bora kuliko wewe. Ukinitukana utakuwa umeshindwa na hoja ukinijibu kwa points utakuwa more great thinker

Ungekuwa unaongea ungeonekana katika hali ya panic. Mleta mada ana maswali mawili makuu 1. Je, waliomo ni vilaza/hawafai kuwa mawaziri? 2. rais kawadharau?

Wewe umejibu mada kwa kuunga namba 1 kwahiyo huna haja ya kumlaumu au kumtupia hayo maneno na kujilinda.
 
Wapendwa wabunge wa CCM, kweli nyote hamfai mpaka JK ana-sample nje ili ampate anayefaa wa kumpa uwaziri!! Kweli mmekwisha na mlivyo wema hamlioni hili. Sio uchochezi bali ni fact ambayo inauma, mi ingeliniuma sana.
 
Wana jamvi kila uchwao wabunge wa CCM wamekuwa wakijinadi kuwa wao wooote ni mawaziri watarajiwa na lazima wailinde na kuitetea serikali yao sasa imekaaje baba Mwanaasha kuteuwa wabunge wapya na chini ya masaa 24 anawatunuku uwaziri? ina maana wabunge zaidi ya 200 wa CCM hawafai kuwa mawaziri? wananchi tulichemka kuwachagua? sio chaguo la chama? hawawezi kutetea ilani ya chama na kusimamia maagizo ya chama au?

Nabaki na maswali mengi kuliko majibu, ila naamini JK amefanya bunge litakuwa tamu zaidi kwa kuwa wabunge wa ccm sasa wataonyesha hasira na chuki zao dhidi ya serikali yao wazi wazi.

Wako wapi kina Hamisi Kigangwalla waliocha kusaini fomu ya Zitto wakitaraji kupewa uwaziri

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom