JK, haya si maisha bora; ni maisha balaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, haya si maisha bora; ni maisha balaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Mar 17, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hakuna kitu kinachoniumiza katika maisha yetu ya kila siku katika nchi yetu tukufu ya Tanzania kama maisha duni waliyonayo Watanzania. Bahati mbaya sana, kila kunapokucha ni heri ya jana- hali ya maisha inaziodi kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele!

  Ajabu ni kuwa takwimu zinazotolewa kila wakati zinaonyesha kuwa kipato cha Watanzania kimepanda na kuashiria kuwa maisha yamekuwa bora. Ukweli ni kuwa Maisha ya Watanzani wengi ni duni mno; kila siku iendayo kwa Mungu hali inazidi kuwa mbaya zaidi na ule msemo wa kila kukicha heri ya jana unajidhirisha!

  Hebu tafakari mabadiliko ya bei hizi bidhaa hizi muhimu tangu mwaka 2005:-

  Sukari
  Mwaka 2005, wakati JK anakabidhiwa nchi na mtangulizi wake Mkapa kilo moja ya sukari ilikuwa shilingi mia tano 500/- leo hii miaka mitano tu bei ya sukari imepanda mara tatu zaidi na kufikia shilingi 1,500/-!

  Mkate
  Mwaka 2005, wakati Mh JK anachukua nchi; bei ya mkate wa kawaida wa Super Loaf, ilikuwa shilingi 300/- leo hii mkate huo huo unauzwa shilingi 700/-!

  Orodha ni ndefu mno na unaweza kuongeza na kuongeza. Hii ni tofauti kabisa na kauli mbiu ya Rais wetu JK wakati akipigania kura na ahadi kemkem na kauli mbiu maarufu "Maisha bora kwa kila Mtanzania"

  Maisha bora sasa imekuwa maisha balaa kwa kila Mtanzania! Watawala wetu waulizwapo kuhusu ahadi ya JK ya Maisha bora hutugeuzia kibao na kujibu ati Maisha bora hayaji kwa kukaa tu! Hivi ni kweli Watanzania tumekaa tu kusubiria hayo maisha bora? Mbona Watawala mnatudhihaki?

  Tukilinganisha hali za Maisha ya Watanzania katika awamu hizi mbili- awamu ya 3 na awamu ya 4 utaona kuwa Awamu hii imechangia sana kudunisha maisha ya Watanzania kwa kiwango kikubwa sana ingawa ni awamu ambayo ina nafasi nzuri sana ya kuboresha maisha kuliko awamu iliyopita maana Mkapa aliwaachi misingi imara ya kiuchumi na namna yha kudhibiti mfumuko wa bei ambao ni kisu kilakali kwenye vifua vya Watanzania wengi. Awamu ya JK ina neema kubwa ya kukuzsanya mapato mengi zaidi kuliko awamu iliyotangulia lakini ni kama vile Utawala wa JK umevaa suruali yenye mifuko iliyotoboka!

  Kwa kuangalia maisha ya Watanzania na matumizi makubwa ya Watawala wa Awamu ya 4- safari nyingi, Warsha na Semina tele tunaona kuwa JK ametusaliti sana Watanzania maana ni marafiki zake na ndugu zao ndo wanaofaidi hayo Maisha bora mabayo kwa Watanzania wengi ni maisha balaa!

  TUTAFAKARI!
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunapaswa kumpa ridhaa ya kuendelea kwa kipindi kingine ili arekebishe mambo hayo!!
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Yah, ni kweli. Lakini hii miaka mitano alikuwa anajifunza na ndiyo maana mambo yamekuwa magumu. Nilikuwa na kikao naye hivi juzi tu akanambia amejipanga vilivyo kuweka mambo sawa miaka mitano ijayo kama ambavyo boramaisha amefafanua!!!? Kwa hiyo tunaombwa kwa pamoja tumuunge mkono katika uchaguzi wa mwaka huu, au mnasemaje? Tuna imani kwamba tutapata asilimia zilezile za 2005 au zaidi.
  Kidumu chama cha mapinduzi!!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I support you 100% maisha yamekuwa magumu uelekeo wa uchumi wetu umekuwa wa kubahatisha mara uchumi umepanda mara Financial crisis imetuaffect sasa hivi cjui watakuja na lipi??????

  kumpa ridhaa kivipi?? hatujaona mwelekeo wake kukuza uchuni wa nchi hii, Please changia mada.......

  Wewe uchangiaji weko haufai, naomba utoe mchanganuo kama kweli anafaa uchumi wetu ataukuza vipi?? na sio kumsifia bila hoja
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu Vangi, alikuwa anajifunza nini, wapi , na kwa nani? The guy has been in leadership for 2 previous regimes. Waziri Wa Nishati na Madini, na baadaye Waziri wa Fedha (Wakati wa Mzee Mwinyi), Waziri wa Mambo ya Nje (Wakati wote wa Mkapa)! Hizo shule alizopitia hazikumtosha? NAsme akuwa wakati wa Mkapa, RAis wetu ana mengi ya kujifunza- Yaani Mafanikio na Failure za Mkapa Vs MZee Mwinyi.

  Historia ya Marais wetu haiko hivyo labda aandike historia mpya. TAfakari haya:-

  1985-1990 Mzee Mwinyi alifanya vizuri sana hadi tukampa lile fagio maarufu la Chuma! Baada ya kchaguliwa kipindi cha Pili, lile fagio akalificha uvunguni na mambo yakaanza kwenda kombo hadi alipoondioka 1995!

  1990-1995 Mkapa alifanya mambo makubwa sana na kwa mafanikio makubwa. Ingawa alikuja kuitwa Mr Ukapa lakini Ukapa ule ulifanya maisdha ya Wataznaia wengi yawe stable maana mfumuko wa bei ulipungua mno. Baada ya kuchaguyliwa awamu yake ya pili Mkapa akaanza vituko vya kujilimbikizia mali yeye na wapambe wake hadi kujikabidhisha Mgodi wa Kiwira! Biashara na Makampuni ya uwekezaji yakafungukiwa hadi Ikulu!

  KWa historia hiyo nina matumaini madogo sana ya kuwa maisha ya Wataznanai yataimarika labda JK na tumuombee aandike historia mpya tofauti na watangulizi wake (Mungu amsaidie).
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa hawezi kufahamu. Si unajua kodi yako ndio inanunua supplies za pale Magogoni.
  Neither he nor his family feel the pinch.
  Kuna sehemu TZ ukienda sukari ni hanasa. Sembuse mkate (mkate ndio nini?).
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda viotu vimepanda bei kwa sababu kipato cha watanzania nacho kimepanda... labda
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Una maana gani unaposema kipato cha watanzania kimepanda
   
 9. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawe jifunze kuheshimu michango ya wenzio! Mimi naitwa Boramaisha, jina langu ni mchango tosha usiohitaji maelezo marefu.
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Haya changia
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  hii lawama iende katika chama kwa ujumla- kuwadanganya watanzania - kutoa ilani ya uchaguzi isiyotekelezeka ni usanii na dhambi kubwa - Chama tawala kinadiriki kusema uwongo?

  CCM ni wasanii - na sasa hivi wanatunga gia nyingine ya kuja kutudanganya kwa mara ya pili.
   
 12. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  bora maisha. porojo hazitakwisha hata akipewa miaka 50. lazima atakuja na sababu. kama kweli angekuwa amezamilia angeanza na wahuni kama RA na wengine kwa sababu alikuwa na support ya public, lakini aliwakumbatia na kuisahau jamii. sasa hivi tunasema tumpe ridhaa nyingine ya nini? kama ni wafata upepo sawa.
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  best kuna haja kweli ya kumwongezea muda? Ni kumpiga kibuti tuchukue wengine tu. hadi ifike 2015 hatutaweza kutumia sukari hasa sisi wenye maisha ya chini. Ni balaa tupu, tatizo ni kutoa ahadi zisizotekelezeka!
   
 14. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,172
  Trophy Points: 280
  Hawa watu mnawaongelesha kila siku lakini kama vile hawasikii wala hawaelewi. Leo Mkullo anasema mfumuko wa bei umepungua. Teh teh hii inji bwana ni kujicontradict kwa kwenda mbele.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona hatusikii tena ule wimbo wake wa kuongoza kwa 'NGUVU MPYA, KASI MPYA na ARI MPYA?'. Mie naona yamemshinda! Akae pembeni ampishe mtu mwingine. Ameshindwa!
   
 16. T

  TANURU Senior Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnataka ashindwe mara ngapi?????!!!!!!
   
 17. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani si imesemwa aliyeshiba hawezi jua shida za mwenye njaa? na tangu lini aliye chini ya kivuli cha mti akajua shuruba ya mchumia juani? nenda oysterbay na masaki uone watanzania wenye maisha bora! JK aliposema maisha bora kwa kila Mtanzania nadhani hao ndio walikuwa walengwa wake! Ibra unaongelea sukari na mkate! nenda huko vijiji ukaone mkate na sukari ni anasa, vyakula basic kama unga, maharage, mchele na hata chumvi havikamtiki kwa bei. JK sio tu ametusaliti watanzania, amesaliti hata imani yetu kwake, huyu jamaa hafai nimeamini once a politician always a politician! JK hatobadilika hata tumpe miaka kumi, hakuweza miaka mitani iliyopita atawezaje sasa?
   
 18. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kuna rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa rais hana tatizo, tatizo ni wasaidizi wake!
  nami nikamuuliza; nani anachagua/teua hao wasaidizi wake?
  huyu jamaa hana kitu kabisaaaaa! nchi imemshinda hii
   
Loading...