JK: Hatutaki Rais mzee 2015

Mimi nashangaa kitu kimoja. Aliyesema wazee wanaotaka urais mwaka 2015 ni JK lakini mashambulizi yote yako kwa Zitto ambaye aliyasema haya kujibu hoja na nini mtazamo wake tena basi ktk warsha ya vijana. Hivi mlitaka Zitto aseme kwamba hapana wazee tu ndio waendelee kuongoza nchi wakati hana hata haelewi sifa ya uzee kuwa rais ni nini, halafu mbele ya vijana wwalioandaa warsha hiyo. Au kwa tafisri zenu kusema kwake lazima kunamaanisha unautaka Urais?. Jamani mbona mnayafanya mabadiliko kuwa magumu kiasi hiki hivi kweli vijana nyie mtaweza kutukomboa au ndio tarariraaa kama siye hapa..Vijana hasa wa Chadema kwa nini mnamwogopa Zitto kiasi hiki?
Zito anaandamwa kwasababu ameshagundulika ni mnafiki, mbinafsi na hawezi urais anaouta usiku na mchana. Iko elewa sasa dugu?
 
Kwa iliyokuwa ccm,lakini siyo ccm hii ya sasa.Nominee wa ccm 2015,siyo lazima aje kuwa Rais.Chukulia kwa mfano anayeandaliwa mazingira haya ni Mwinyi.Je huko ccm hao wazee wanaotaka kuondolewa kwa zengwe,watakubali kumpisha na kum support?chadema au chama kingine kikipitisha mgombea 'nguli',Mwinyi ana ubavu wa kusimama nae?
Yaliyotokea Kenya(KANU) ndiyo yatakayotokea Tannzania(ccm) mwaka 2015!


Naona kabisa El akitolewa kwa zengwe na kupeleka nguvu yake ya kiitelejensia, kifedha na kimtandao wake wa kimafia ikiwa hata kichini chini kambi ya upinzani huku akina Sitta na wenzake wakizila kumpigia kampeni mgombea mteule wa Rais Kikwete..huyo atapata shida kushinda lazima tuweke mseto 2015..sioni vinginevyo hawa vilaza wa kikwete akina Mwinyi, Nahodha, Migiro, Membe nk kushinda
 
na wewe akili zako vipi? ameshaona kwamba watu wa umri wake sio ''digital'' hawawezi, kwa hiyo anatumia mamlaka yake kama reisi kutoa huo ushauri na ni sahihi ausimamie kama raisi, sije akapenyeza mtu wa miaka ya ''1947''
 
Katika historia ya Tanzania huru hakuna wakati ambapo wanawake walikuwa hawashiriki kupiga kura; na hakuna sababu ya msingi ya kushusha umri wa kuanza kupiga kura kuja miaka 16. Upigaji kura ni uamuzi wa mtu mzima na tunayo universal suffrage. Kama tunaamini mtoto wa miaka 16 anaweza kufanya uamuzi mkubwa wa kupiga kura basi tushushe universal suffrage ije kwenye 16 ili wenye umri huo waweze kufanya maamuzi mengine ya watu wazima - kuoa, kushtakiwa kama watu wazima, n.k n.k kwanini tushushe tu kwenye kupiga kura?

Hili la kushusha umri wa kugombea Urais kutoka 40 kuja 35 kunaweza kuwa kuzuri lakini kusihusu uchaguzi wa 2015 liwe kwa ajili ya uchaguzi wa 2020. Lakini wakiamua kuondoa hilo waondoe pia ulazima wa kuwa na shahada ya kwanza kwa mgombea wa Urais! Kwanini ni lazima mtu awe na shahada kuwa rais? kwani Urais ni kazi ya usomi?

Hivi hujaelewa kichwa cha habari ? na kwanini MAkamba anataka watoto waruhusiwe ? si anajitayarishia mazingira mazuri ya kupigiwa kura akijua labda yeye ndio atakua mgombea ! CCm juu MAkamba juuu
 
Back
Top Bottom