January Makamba na Zito Kabwe hawanivutii, ninawaonya leo watanzania wenzangu, itakua afadhali mlivyokosea kumteua na hatimaye kumchagua ****** kwa vigezo mlivyovitumia, kuliko majuto mtakayosababishiwa na mmoja wa vijana hawa. Hoja ya ujana ni sawa tu na hoja ya uzuri wa sura (kwa wanaouona) iliyovuma na hatimaye kutupatia mkuu wa nchi anayejumuishwa kwenye genge la uhalifu dhidi ya wananchi wake. Hivi vihoja ni hatari, na wa kulaumiwa hapa ni CCM, kipo katika hali ya kufani kinatapatapa ili angalau kiishi kitambo kidogo, kimekwisha tufanyizia hasara kubwa, tunaonekana kukipa nafasi kimalizie silaha zake kilizoziweka kwa pigo la mwisho. hawa vijana kabwe na makamba, ikiwa wanaamini ujana ndiyo suluhisho la kiuongozi kuelekea uchumi tunaouota, watuapie kwa kusema "kamwe sitagombea urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania" wawaache vijana wengine kugombea, kinyume chake hata baada ya maziko ya ccm tutashindwa kusimamia mali zetu tunavyotarajia, kikwazo kitakuwa Nyoka kijana wa ccm January ama Zitto Kabwe (mimi na makamba hatukukutania barabarani) hutaweza kuhoji mali za chenge, hutahoji ubaya wa ubinafsishaji na mamikataba mabovu ya madini, gesi, mafuta ············· eeh! kikwete alituahidi angeipitia upya mikataba ya madini kwa lengo la kuiboresha, kiko wapi? Hapo sijui mtakuja kutamani rais mtoto!!!!!! mtanzania mwenye akili timamu ndiyo sifa pekee inayo accommodate mengine mazuri yote.