Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Katika mdahalo wa jana JK aliulizwa swali moja zuri sana: kwamba ktk kipindi chake hiki cha miaka mitano kilichopita, anataka Watanzania wamkumbuke (legacy) kwa kitu gani?
Muungwana alitulia kama sekunde 40 hivi bila kujibu, maana anajua fika kwamba hana cha kukumbukwa. Kamera ya mtandao mmoja ikafanya ka-uchokozi kidogo, ilielekea kwa Kinana ambaye macho yalikuwa chini. Kimya kilivyokuwa sindano kama ingeanguka sakafuni ingesikika.
Baadaye akajikakamua (literally, that is) kusema kwamba anataka Watz wamkumbuke kwamba aliwatoa hapa na kuwafikisha hapa – huku akionyesha ishara kwa mikono kuonyesha sehemu moja kwenda nyingine!
Duh! Jamaa hana la kukumbukwa – na anajua hivyo – sijui anataka urais wa nini tena – was matrip ya nje na kula maisha?
Lakini jibu lake lina tafsiri moja tu – ametutoa kwenye hali nzuri kwenda kwenye hali mbaya. Kutoka kilo ya sukari Sh 500/ kwenda Sh 2,000/-. Kutoka bati sh 5,000/- hadi 16,000/-, kutoka cement 6,000/- hadi sasa 13,000/-, petrol sh 800/- hadi sasa 1,700/-, ulaji wa majani badala ya nyama
etc etc etc etc etc.
Kweli muungwana katuhamisha!!!!!
Lile swali halikuwa rahisi kama wengi mnavyofikiri. Mh. Kikwete ametawala kipindi ambacho kulikuwa na mdororo wa uchumi duniani. Madhara yale ya mdororo wa uchumi kwa kiasi kikubwa yamechangia sana kufuta ndoto yake ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Vile vile aliipokea nchi ikiwa katika hali mbaya ya ukame, madhara yake nayo yaligharimu kiasi kikubwa cha pesa ambazo zingeweza kutumika kuboresha maisha ya watanzania. Kama nchi ya Ufaransa inafikia mahali kulazimisha wafanyakazi wake wasistaafu kwa kuwa hawana pesa ya kulipa mafao ya kustaafu jee nchi kama Tanzania ambapo Vita vya Iraq vimepandisha bei ya mafuta zaidi ya mara 10, unadhani ina uwezo wa kustahimili mabadiliko yote hayo bila maisha ya mtanzania kuathirika?

hahahhhahahahhaaa...!!!Katika mdahalo wa jana JK aliulizwa swali moja zuri sana: kwamba ktk kipindi chake hiki cha miaka mitano kilichopita, anataka Watanzania wamkumbuke (legacy) kwa kitu gani?
Muungwana alitulia kama sekunde 40 hivi bila kujibu, maana anajua fika kwamba hana cha kukumbukwa. Kamera ya mtandao mmoja ikafanya ka-uchokozi kidogo, ilielekea kwa Kinana ambaye macho yalikuwa chini. Kimya kilivyokuwa sindano kama ingeanguka sakafuni ingesikika.
Baadaye akajikakamua (literally, that is) kusema kwamba anataka Watz wamkumbuke kwamba aliwatoa hapa na kuwafikisha hapa huku akionyesha ishara kwa mikono kuonyesha sehemu moja kwenda nyingine!
Duh! Jamaa hana la kukumbukwa na anajua hivyo sijui anataka urais wa nini tena was matrip ya nje na kula maisha?
Lakini jibu lake lina tafsiri moja tu ametutoa kwenye hali nzuri kwenda kwenye hali mbaya. Kutoka kilo ya sukari Sh 500/ kwenda Sh 2,000/-. Kutoka bati sh 5,000/- hadi 16,000/-, kutoka cement 6,000/- hadi sasa 13,000/-, petrol sh 800/- hadi sasa 1,700/-, ulaji wa majani badala ya nyama
etc etc etc etc etc.
Kweli muungwana katuhamisha!!!!!
Baadaye akajikakamua (literally, that is) kusema kwamba anataka Watz wamkumbuke kwamba aliwatoa hapa na kuwafikisha hapa – huku akionyesha ishara kwa mikono kuonyesha sehemu moja kwenda nyingine!
Wana JF.
Jana niliandika thread inayohusiana na habari ya Lowassa lakini naona moderator aliipiga chini.
Kwa mnaokumbuka vizuri, Lowassa alikuwa kiongozi shupavu katika kazi yake ya Uwaziri mkuu na pia alikuwa na mapunguzu lakini siyo limbukeni kama JK anajua anachofanya ni mtu asiyecheka cheka na watendaji wake.
Lowassa katika kuchagua wakuu wa mikoa, wilaya aliweka watu wake na strategy yake na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM ilikuwa ni kumtoa JK baada ya miaka mitano ya kwanza kwani CCM ilikuwa imeshaanza kuyumba mapema na kuwepo na kambi mbalimbali.
Watu wa karibu na JK wakamtonya kuwa angalia Lowassa mshikaji wako anataka kukufanyizia na hapo ndipo issue ya Richmond ikaanza na ukiangalia kwa undani Lowassa hakuhusika sana katika mambo yaliyokuwa technical bali kutekeleza ya JK nchi ipate umeme, mengineyo kama gharama yalishapitia kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu na wengine wengi kabla ya Lowassa..mnaweza kuhoji mbona alikubaliana lakini mwishoni mwa siku ilibidi kuwajibika na hii ilikuwa either yeye akatae kujiuzulu na kujiosha, JK na CCM wakaona wamdanganye kuwa ajiuzulu na immediately watamshafisha na hiki hakikufanyika labda tu spika alijaribu kumsafisha.
Sasa mkae mkijua CCM imeoza na viongozi na wakongwe, wastaafu kama kina Mkapa wanampiga chenga kwani wanajua kichwani ni SIFURI na habebeki na chama chao kiko kwenye wakati mgumu. Pia Kikwete mwenyewe anajua uozo uliopo na ndiyo maana aliwekwa chini na CC kuwa chama kimekuwa na taswira mbaya sana na itabidi abebe jukumu kwa sasa…Kikwete personally ni mtu mzuri na kama angekuwa anagombea yeye kama yeye basi idadi kubwa ya waTZ ingempa kura, sasa hawezi kusema anawatimua baadhi ya viongozi kwani wao ndiyo wamemweka madarakani…support za kifedha kutoka kwa mafisadi kama Mramba zinaenda kwenye kampeni za CCM.
Vijana tuchague kiongozi makini kama Dr. Slaa, Prof. Lipumba tunahitaji mabadiliko sasa.
Natofautiana na wewe kabisa.Ni swali rahisi sana, nakumbuka na wewe pia jitahidi ukumbe katika moja ya hotuba zake za kampeni akiwa Bukoba alisema."LENGO LANGU NATAKA NIKIONDOKA MADARAKANI WATANZANIA WANIKUMBUKE" Iweje akose jibu wakati tayari alishatamani kukumbukwa.it is ridiculous!!!!!
Wewe jamaa ni useful idiot. A useful idiot is an intellectual anaetumiwa na wanasiasa kueleza mafanikio yao kielimu zaidi.
Sadly JK hajasema hayo. Kasema mengi katelekeza. Yapi? Anajua yeye na Kinana. You just can't accept the fact that your president is failure ambae hajui sababu gani Tz ni maskini. Sijui mjinga hapa ni wewe au blind followers wa JK. Nadhani wote.
Lilikuwa swali la kijinga.
Mtu bado hata hajamaliza nusu ya utawala wake anaogombea kuendelea nao unamuuliza unataka kukumbukwa kwa kitu gani, ndio maana alisema anataka awatoe hapa awapeleke hapa. Hapa wapi, akimaliza mtaona!