Kila kitu kushangaa tu badala ya kuchukua hatua
.....hata mtu mzima kubembea ni anasa.
hana jipya mbaya zaidi kasema ngeleja na mhando hawana kosa tatizo ni maji, anyway mi nilisikia kwenye nukuu za magazeti ya jana, mwenye full story anijuze.
Rais Kikwete amedhihirisha kuwa yeye ni mtu safi asiye na doa, lakini wanaomuangusha ni watendaji wake.
Kama tulikuwa pamoja Mkuu,hata mie nilitaka nihoji Safari zakwenda Kubembea Nje Ya Nchi(Majuu)zenyewe tuziiteje?Kaa Nchini acha safari za Nje... Umesikia Mwai Kibaki akisafiri safiri kama wewe?
Juzi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisheherekea miaka 57 ya kuzaliwa kwa TANU kwa mbwembwe na chereko. TANU ilimaliza muda wake wa kuishi baada ya kuungana na ASP mwaka 1977.
Hii inafanana na kufanya birthday ya marehemu mzazi wako! Kuna kituko kimoja kilifanyika Moshi cha mtu kufanya jubilei ya ndoa yake wakati mwenzi wake alishakufa miaka kumi iliyopita.
Ukitazama kwa makini inaonyesha kuwa CCM wameshaona kuwa hawana ushawishi wala haiba kwa wananchi na ikapelekea kukumbuka marehemu mzazi wake na kumfanyia birthday party ili walau kupata mapokeo mazuri ya wananchi.
Kulikuwa na ulazima gani wa kufanya sherehe hiyo? Kwa kizazi cha sasa ambacho kina muamko tofauti (rejea matokeo halisi ya uchaguzi mkuu uliopita), wala hawajui TANU ni nini! Labda wale wenye udadisi wa historia. Na hata wakiijua, haina mantiki yeyote kwao.
Nasubiri kwa hamu kufanywa kwa birthday party ya ASP. Tena basi mwakani ifanyike sherehe za kuzaliwa kwa TAA maana bila hiyo, TANU isingezaliwa! Halafu tena na sherehe ya kuzaliwa HIZBU. Ushanifahamu?
basi mwambie aache kulalamika,atumie mamlaka tuliyompa.Wananchi walalahoi 2nalalamika na rais wetu jamani nae hivyo hvyo!!!Yani panya kaingia ndani afu baba zima na midevu yake linaomba msaada tena kwa yowe,mke na watoto waende wapi sasa?Rais Kikwete amedhihirisha kuwa yeye ni mtu safi asiye na doa, lakini wanaomuangusha ni watendaji wake.
WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi.
Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU.
Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliendelea: Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani.
Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini? Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini.
TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa wakingangania madarakani.