JK awashangaa viongozi CCM kupenda anasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK awashangaa viongozi CCM kupenda anasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jul 8, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  WENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amewashangaa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akisema hawajituma, wamesahau wajibu wao na wanapenda anasa. Alisema tabia hiyo imejijenga kwa viongozi hao kiasi cha kusahau majukumu yao ambayo ni pamoja na kudumisha umoja na moyo wa kujituma. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni ajabu kuona viongozi hao wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyoasisiwa na TANU, hata baada ya kuwezeshwa kwa rasilimali nyingi.

  Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika maadhimisho ya kumbukumbu ya TANU na miaka 50 ya uhuru. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, viongozi wa sasa wa CCM wamekosa moyo wa kujituma kiasi cha kusahau wajibu wao, licha ya kuwa na rasilimali nyingi ikilinganishwa na enzi za TANU.
  “Sasa tumewapa magari, lakini hawaendi vijijini kuwatembelea wanachama. Wengine hata matawi hawayajui yanavyoendelea. Tusipokuwa na moyo wa kujituma, ndiyo utaona mambo yaliyopo sasa," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wanachama waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.
  Rais Kikwete aliendelea: “Awali tuliwauliza, wana shida gani? Wakasema wanataka vipando (magari). Tukawapa Mahindra, wakaona hazitoshi. Siku hizi wana Land Cruiser. Lakini baadhi yao hawaonekani.

  Kingunge alikuwa Katibu Mkuu wa TANU alifanya kazi kwa bidii bila gari. Leo wewe una shangingi unashindwa nini?” Akitoa mfano wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete alisema msingi wa TANU, ni umoja na moyo wa kujituma. Alisema TANU ilishinda vikwazo vingi licha ya kutokuwa na rasilimali nyingi kama walizokuwanazo wakoloni, kwa kuwa walitegemea umoja wa wanachama waliokuwa masikini.

  “TANU ilikuwa na uwezo mdogo wa rasilimali hivyo ilitegemea michango ya wanachama waliokuwa masikini. Siri ilikuwa ni umoja na mashikamano wa wanachama wake. Mwalimu Nyerere alisisitiza kitu hicho hadi anakufa, Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu,” alisema Kikwete Rais Kikwete alieleza kuwa kupitia umoja na moyo wa kujitolea, TANU ilishinda pia changamoto ya kuwaondoa wakoloni waliokuwa waking’ang’ania madarakani.
   
 2. i

  in and out Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha mapindunduzi kurudisha sherehe za tanu, je kupitia sherehe hizo tanu itaweza kuimarisha chama hicho, hii ni kutokana na watanzania wengi kukipenda chama hiki kilichodai uhuru kutoka kwa mkoloni.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  The known propensity of a democracy is to licentiousness which the ambitious call and the ignorant believe to be liberty
   
 4. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Juzi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisheherekea miaka 57 ya kuzaliwa kwa TANU kwa mbwembwe na chereko. TANU ilimaliza muda wake wa kuishi baada ya kuungana na ASP mwaka 1977.

  Hii inafanana na kufanya birthday ya marehemu mzazi wako! Kuna kituko kimoja kilifanyika Moshi cha mtu kufanya jubilei ya ndoa yake wakati mwenzi wake alishakufa miaka kumi iliyopita.

  Ukitazama kwa makini inaonyesha kuwa CCM wameshaona kuwa hawana ushawishi wala haiba kwa wananchi na ikapelekea kukumbuka marehemu mzazi wake na kumfanyia birthday party ili walau kupata mapokeo mazuri ya wananchi.

  Kulikuwa na ulazima gani wa kufanya sherehe hiyo? Kwa kizazi cha sasa ambacho kina muamko tofauti (rejea matokeo halisi ya uchaguzi mkuu uliopita), wala hawajui TANU ni nini! Labda wale wenye udadisi wa historia. Na hata wakiijua, haina mantiki yeyote kwao.

  Nasubiri kwa hamu kufanywa kwa birthday party ya ASP. Tena basi mwakani ifanyike sherehe za kuzaliwa kwa TAA maana bila hiyo, TANU isingezaliwa! Halafu tena na sherehe ya kuzaliwa HIZBU. Ushanifahamu?
   
 5. S

  Sobangeja Senior Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mbinu walioitumia kurejesha sherehe za TANU ni mbinu fikirika ya kurejesha heshima ya chama chao kitu ambacho hakiendani na fikra na matendo yao.Wanaotaka mabadiliko ni vijana waliozaliwa baada ya uhuru, hawana sababu wala haja ya kurudi nyuma na kuwaza namna uhuru ulivyopatikana.Ni jambo lisilona shaka wanatwanga maji kwenye kinu.Matunda yake ni madogo sana.wananchi wanahitaji hali ya maisha na uchumi wao uboreshwe na si bra! Bra! wanazoleta!!!!!!!!!!
   
 6. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kusema ukkweli nami hili limenishangaza au wanataka kukufufua tena?
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kaa Nchini acha safari za Nje... Umesikia Mwai Kibaki akisafiri safiri kama wewe?
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  jamani mkuu wa kaya anatafuta sehemu nzur ya kupmzika au bado umwelewa@nngu007
   
 9. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Hajagusia lini watawavua magamba hao mapacha watatu?
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,476
  Trophy Points: 280
  hana jipya mbaya zaidi kasema ngeleja na mhando hawana kosa tatizo ni maji, anyway mi nilisikia kwenye nukuu za magazeti ya jana, mwenye full story anijuze.
   
 11. A

  Andre02150 JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Anashangaa? Mbona hajishangai yy mwenyewe na misafara ya BMW? Mkuu inabidi aache visingizio!
   
 12. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  kuwashangaa tu haitoshi...kama mtu hatimizi wajibu wake fukuzia mbali waajiriwe wenye uchungu na kazi.
   
 13. Chaser

  Chaser Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete amedhihirisha kuwa yeye ni mtu safi asiye na doa, lakini wanaomuangusha ni watendaji wake.
   
 14. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CDM oyeeeeeeeee!!!! mbowe oyeeeeee!! slaaa oyeeeee!!! zitto oyeeeeeee!!! Tundu lissu oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Msajili wa vyama anajua kuwa kuna chama kipya TANU tanzania?maana ccm imekufa sasa waisajili TANU
   
 16. MANI

  MANI Platinum Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,408
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Hivi yeye haoni tofauti kati ya TANU ile ya zamani na CCM yake hii ya sasa?
   
 17. b

  baba koku JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mimi naamini kuwa hizi shereheni zina lengo la kuweka historia sahihi haa kwa vijana. Tukumbuke kuwa historia ya Tanzania ina uhusiano mkubwa na TANU.
   
 18. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kikwete anakuwa komedia siku hizi mara sio mwaingu ya mvua ya kujaza mtera, sasa awewaambia watendaji wa serikali waache anasa.

  Swali linakuja Je yeye ameacha hizo ANASA za KUSAFIRI NJE YA NCHI? mimi naona yeye anafanya anasa kubwa kuliko wengine hapa nchi.

  anasema amewapa magari viongozi waende vijijini wakatembelea wananchama sio Wakajue wananchi wana matatizo gani ili serikali iweze kuyatatua.

  Ndio nasema hivi Mtawala Jinga, Watanzania tumelala bado hakujakucha
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukizungumzia siasa za TANU unazungumzia miiko ya AZIMIO LA ARUSHA,tena kwa viongozi.....je jk anafuata na ccm yake????
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Dalili nyingine hiyo ya kuvunjika muungano kwani hili likitokea CCM inakufa technically ndio maana jamaa wanafufua TANU. Kwa wasiojua TANU(bara) iliungana na ASP(visiwani) 1977 kuunda CCM baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar Kuunda Tanzania 1964.
   
Loading...