JK awakuna viongozi wa dini katiba mpya

JK awakuna viongozi wa dini katiba mpya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Imeandikwa tarehe 20 Oktoba 2013 By Theopista Nsanzugwanko

UMOJA wa Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo kutoka madhehebu mbalimbali nchini, wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa busara aliyoitumia kukutana na viongozi wa juu wa vyama vya siasa vya upinzani na kushauriana na kusikilizana kuhusiana na mchakato unaendelea wa Katiba mpya.

Wamesema kitendo hicho ni mfano wa kuigwa kwa nchi za
Afrika, kwani ameonesha uwezo mkubwa wa kisiasa na kwamba, kiongozi wa kweli ni yule anayekuwa muungwana, mvumilivu na msikivu kwa wale
anaowaongoza.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa Umoja huo, Sheikh Said Godigodi kwa niaba ya viongozi wa Baraza la
Maaskofu Katoliki (TEC), Pentekoste, Lutheran, Wasabato na pia Waislamu.

Licha ya pongezi zao kwa Rais Kikwete, Umoja huo umewataka viongozi wa vyama vya upinzani na asasi za
kiraia kuunga mkono juhudi za Rais huku wakionywa wasiwe chanzo cha kuiingiza nchi katika vurugu na machafuko.
Alisema wanasiasa na wanaharakati wanatakiwa kuwa na weledi wa kutosha kwani wapo Watanzania wanaoamini wanapotoa matamko yao lazima wawe makini na kuonesha uzalendo kwa Taifa kama anavyoonesha Rais Kikwete.

“Pia tunapenda kuwatahadharisha Watanzania wote kuwa makini na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na
Asasi za kiraia kwa kuwa historia inaonesha kuwa sehemu mbalimbali katika bara la Afrika, Asia na kote
Ulimwenguni ndiyo chanzo cha vurugu na machafuko,” alisema Shehe Godigodi.

Hivyo aliomba kuwa makini kama anavyofanya Rais Kikwete kwa kuwa na dhamira safi na kupuuza wenye nia wasiotaka Katiba mpya ipatikane nchini.

“Katiba mpya ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa, hivyo tunampongeza Rais Kikwete kwa kukubali kupatikana kwa Katiba mpya ambayo tumekuwa tukiililia kwa miaka mingi,” alisema na kuongeza kuwa, kauli za vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa upinzani hazisaidii, na badala yake kuwataka kujenga hoja za msingi.

Katibu huyo alikumbusha kauli za vitisho za wapinzani walizozitoa Jangwani hazikuwa na sababu wakati walielewa wangeona na Rais Kikwete na kuzungumza naye kwa kina.

“Sasa wameonana na Rais na kufikia mwafaka, sasa zile kauli za kuanza mazoezi na mengineyo zilikuwa za manufaa ya nani? Ni vema viongozi hao wasiyumbishe wananchi, kwani kama Rais asingekuwa na dhamira njema katika kupata Katiba mpya asingekubali kuanza kwa mchakato huo,” alisema Shehe Godigodi.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete alikutana na viongozi wa vyama vya upinzani vyenye wabunge na kuzungumzia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kufikia mwafaka, baada ya awali vyama hivyo kuonesha wasiwasi wa mwenendo wake huku wakitishia kutokuwa tayari mchakato
ukiendelea.

Katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam vyama hivyo pinzani vilifanya mkutano
wa hadhara na kutoa kauli za vitisho kwa Serikali.

Rais angejua kabaisaaa KATIBA itakuwa nzuri kama ikikaa mbali na hao WATU WA DINI; Ndio wanaochefua NCHI in one way or another...

Sasa baada ya kuongea na hao wanasiasa kulikuwa hakuna sababu ya kuwaalika VIONGOZI wa DINI WAO ni wanani kwenye KATIBA???
 
yani nchi hii kila mahali ni UOZO viongozi wa dini nao wanakubali MCHAKATO HARAMU.
cc Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Hao watu wa dini wanachohitaji ni kutambuliwa kuwa wapo, basi...ukifanya hivyo wako tayari kusema Umeteuliwa na Mungu!
 
Shekhe kuwasemea TEC ? Hii inaingia akilini ? Siamini jambo hili kwamba TEC hawana watu wa kutoa matamko yao .
 
Dini inavyoendelee akutaumika Kama ngazi ya wanasiasa. Katiba Mpya inaweza patikana lakini Kama haitafuata misingi ya uzalendo kwanza, tutafika papaya Kama Taifa. Hawa viongozi wanaweza kujitofautisha vipi na wanasiasa SA Leo?
 
Watanzania wenzangu, amini msiamini viongozi wetu wa dini wengi ni wanafiki na wazandiki. Tusipokuwa makini ccm wataweka mapandikizi mpaka kwenye madhehebu ya dini. Siku hizi viongozi wa dini wengi sio wa kweli na ni wachumia tumbo! Nadhani mnakumbuka matamko ya mwaka 2005, kuwa baadhi ya wagombea urais walikuwa chaguo la mungu, hizi ni moja ya kauli za kuliangamiza taifa na si kuliunganisha taifa!
 
JK anafaa sana aongezewe kipindi kingine,hana papara kama wenyeviti wa vile vyama vya Jangwani.
 
Dini inavyoendelee akutaumika Kama ngazi ya wanasiasa. Katiba Mpya inaweza patikana lakini Kama haitafuata misingi ya uzalendo kwanza, tutafika papaya Kama Taifa. Hawa viongozi wanaweza kujitofautisha vipi na wanasiasa SA Leo?
Dini ni mdau mkubwa sana wa Katiba mpya! Bila katiba kutamka uhuru wa kuabudu kutakuwa na matatizo makubwa mno. Viongozi wa dini wakitoa maoni yao kuhusu mchakato wasionekane kama wanaoingilia mambo ya kisiasa!
 
Rais angejua kabaisaaa KATIBA itakuwa nzuri kama ikikaa mbali na hao WATU WA DINI; Ndio wanaochefua NCHI in one way or another...

Sasa baada ya kuongea na hao wanasiasa kulikuwa hakuna sababu ya kuwaalika VIONGOZI wa DINI WAO ni wanani kwenye KATIBA???
Nyie watu wa ajabu sana unataka viongozi wa dini watengwe wakati nyie ndiyo mliokuwa mnamtetea Tundu Lissu aliposema TEC hawakushirikishwa kwenye katiba.

Roho zinawauma huu mchakato wa katiba unapopata uungwaji mkono na viongozi wa dini.
 
yani nchi hii kila mahali ni UOZO viongozi wa dini nao wanakubali MCHAKATO HARAMU.
cc Mzee Mwanakijiji
Hivi wewe kuna kitu cha maana umeishawahi kuandika humu JF, sasa unamshtakia Mwanakijiji wakati haujawahi hata kumuona.
 
Last edited by a moderator:
Baadhi ya hawa viongozi wa dini ni wanafiki kwelikweli!Wakati ma-CCM yanapitisha rasimu ya katiba 'ya CCM' aalikuwa kimyaaa,wanasubiria muda wa kuongea!Raisi angelikubali yaliyopitishwa bungeni ni hawa hawa ungewasikia wanawabeza wapinzani!

Hata hivyo nafikiri hayo ni maoni yake 'ya kichokonnozi' dhidi,sidhani kama TEC wamemtuma hayo aliyosema kwani kwa jambo nyeti kama hilo sidhani kama watamtuma Godigodi 'awasemee'!
 
Nyie watu wa ajabu sana unataka viongozi wa dini watengwe wakati nyie ndiyo mliokuwa mnamtetea Tundu Lissu aliposema TEC hawakushirikishwa kwenye katiba.

Roho zinawauma huu mchakato wa katiba unapopata uungwaji mkono na viongozi wa dini.

Sijui ya TUNDU LISSU ninaongelea kufuatilia studies nilizofanya za KATIBA za NCHI MBALIMBALI... walijaribu kuweka DINI na VIONGOZI wao MBALI pamoja na kuwa walichukua baadhi ya Maombi yao lakini hawakupewa kipaumbele kama Wananchi wa nchi hizo...

Ukiangalia kila NCHI iliyoendekeza DINI kwenye katiba zao zote zina Matatizo

c.c FaizaFoxy
 
[/FONT][/SIZE][/COLOR]
c.c FaizaFoxy
Are you serious?.

Pamoja na kwamba sikubaliani na process ya mchakato wa katiba ilivyoanza lakini jaribu kuwa objective kwenye hoja zako kama unapenda zisimame.

Nchi kama German zina vyama vinavyoongoza nchi venye mlengo wa dini.

Uingereza kiongozi wa nchi ni mkuu wa kanisa.

Italy dini iko mbele ya siasa.

Huo umbali wa viongozi wa dini na siasa uko wapi kwenye hizi nchi zenye "amani".

The list goes on and on
 
Inaonekana kama mkono wa Iddi wa Rais Kikwete kwa viongozi wa dini umeanza kufanya kazi.

Rais Kikwete ameanza kuruka kiunzi cha kisiasa kwa kuwaingiza ndani ya timu yake viongozi wa dini mbali mbali nchini.

Tutaona na kusikia mengi.

D92A8582.jpg
 
Hivi wewe kuna kitu cha maana umeishawahi kuandika humu JF, sasa unamshtakia Mwanakijiji wakati haujawahi hata kumuona.
Too low. I can't argue with left hand brains
 
Are you serious?.

Pamoja na kwamba sikubaliani na process ya mchakato wa katiba ilivyoanza lakini jaribu kuwa objective kwenye hoja zako kama unapenda zisimame.

Nchi kama German zina vyama vinavyoongoza nchi venye mlengo wa dini.

Uingereza kiongozi wa nchi ni mkuu wa kanisa.

Italy dini iko mbele ya siasa.

Huo umbali wa viongozi wa dini na siasa uko wapi kwenye hizi nchi zenye "amani".

The list goes on and on

Yes, Vina MRENGO wa KIDINI lakini haviashirii kufuata MALENGO YA DINI kama Lazima UBEBE BIBLE kwenda OFISINI au QRAN kabla hajaingia ndani ya OFISI zenu lazima MZIONYESHE...

Au, Mashuleni kila Asubuhi lazima sala iwe ya DINI FULANI... ndio ninayoyasema...

Vyama vinaweza vikawa na MAJINA hayo lakini sio VYA KIDINI; Ukimwangalia CHANCELLOR ANGELA MERKEL anahudhuria kanisani wakati wa SHEREHE TUU... kama vile X-MAS kwa kifupi sio MDINi aliyebobea... ni Mwanasiasa aliyebobea...

Na kwao ni hivyo sababu vilianzishwa zamani hauwezi ukaanzisha CHAMA ukapata wanachama kama tunavyofanya BONGO... same as what's happening in the USA...

So be careful when you try to relate those countries with their religion...

Kabla ya kujaribu kubishana JARIBU kusoma MAJARIDA ya HISTORIA za VYAMA VYAO ni fupi na Una INTERNET... It will brighten you UP
 
Sijui ya TUNDU LISSU ninaongelea kufuatilia studies nilizofanya za KATIBA za NCHI MBALIMBALI... walijaribu kuweka DINI na VIONGOZI wao MBALI pamoja na kuwa walichukua baadhi ya Maombi yao lakini hawakupewa kipaumbele kama Wananchi wa nchi hizo...

Ukiangalia kila NCHI iliyoendekeza DINI kwenye katiba zao zote zina Matatizo
[/FONT][/SIZE][/COLOR]
c.c FaizaFoxy
Kila nchi na utaratibu wake kuna nchi zingine hazina katiba. Tunaitaji watu wajifunze kwetu maadili yetu na utamaduni na kuheshimu viongozi wa dini.
 
Kitu waje kujifunza huku?Kulala Bungeni,Kugonga meza na kusema ndiooooo!Waje kujifunza kuzembea kuzilinda rasilimali zao,Kufanya ufisadi i mean waje kujifunza nini hasa huku.This administration has proven to be a failure in many ways.No one is ready to learn to be a failure...No one!!
 
Back
Top Bottom