Je, ni jukumu la Ofisa Balozi kumlinda Mtanzania awapo nje ya nchi, au ajilinde mwenyewe?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kwa wataalamu wa diplomasia na kwa kuzingatia mada yangu ya pasipoti za Tanzania kushikiliwa na waajiri. Watu wengi wanaona siyo jukumu la Afisa Ubalozi kumlinda kwa hali zote raia wa Tanzania bila kujali makosa yake.

Tuna mfano mzuri wa Marekani wanavyolinda raia wao, kuna Mataifa kama Ufilipino na mengine ambayo RAIA wao ni kipaombele wakati wote wanapokuwa nje ya nchi.

Kwa muundo wa wizara ya mambo ya nje , mabalozi na wasaidizi wao wamepewa ilo jukumu? Taarifa kuhusu hali za watanzania ughaibuni hasa kuhusu unyanyasaji wa kingono, kisaikolojia na kimwili upoje?
Kuna Balozi yoyote nje kwa mwaka 2023 amesaidia kumwokoa Mtanzania aliyeripotiwa kunyanyaswa na kumrejesha nchini? Kuna kesi yoyote ambayo Ubalozi au Wizara inayo kuthibitisha kwamba wanachukua hatua kuwalinda Watanzania wawe huru nje ya mipaka yetu?

Naamini January Makamba ni mtu wa tafiti na ufuatiliaji; lakini pia bado ni kijana ambaye anaelewa ukubwa wa tatizo la unyanyasaji Dunia.....naomba atusaidie sera zetu na mifumo yetu inawasaidia vipi watanzania?

Kuna namba au email kwenye website yao yakuripoti ukatili ? Watanzania wenye ndugu zao wanaopitia mateso nje wakitaka msaada wa wizara yake wanafikisha vipi taarifa zao huku ulinzi wao na taarifa zao ukiimarishwa?

Nikipitia website yao sioni Sehemu yakuripoti ukatili.......do they have hotlines za jambo hili? Polisi wamebaini tatizo ni kubwa na wameanzisha community policing.....Wizara ya mambo nje mnadhani tatizo la ukali lipo nchini pekee?
 
ni jukuku ndio nini?
 
Back
Top Bottom