Mwanabodi,
Nimejaribu kwa muda mrefu kuvumilia haya nayoyasoma hapa lakini imefikia wakati inabidi nizitoe hizi pamba masikioni kuyapokea yote kisha kusema yangu machache kwa haki hiyo hiyo mnayoitangaza wengine.
Ni lazima katiba iwe na vifungu vinavyoruhusu baadhi ya sheria kutambua uhuru wa watu fulani ili kutimiza haki mnayozungumzia. Mnaposema Fedha na kodi za Watanzania wote mna maana gani?.... maanake hili swala sasa hivi linaanza kujenga hoja za Udini zaidi na watu mnajibu mengi kwa kutazama rangi zenu za dini.
Sasa ikiwa serikali haitambui mafundisho ya Kikristu inawezaje jenga kinga ya dini hii kuweza kuendesha shughuli zake nchini?..Kila sheria nchini inajengwa kwa kutazama vipengele vyote (Objective) ktk kujenga na sio ktk kubomoa (Negative) manner. Katiba inajengwa kulingana na mazingira yetu, watu wake na mambo yote yanayohusu jamii nzima kwa mtazamo wa kujenga na kuimarisha jamii hiyo. Hata mikataba inayotiwa sahihi ina sheria zake ktk Katiba kwa kuwatazama wawekeshaji, miradi na kadhalika kwa manufaa yetu sote hata kama ni kundi dogo la hawa watu wanaopewa sheria hiyo. Kuna sheria za Kikatiba zinazowapa nguvu na haki wanawake, watoto na hata wageni tofauti na kundi la watu wengine kwa sababu hizi Sheria zipo kwa ajili ya kuweka usawa ama kuleta maendeleo kwa jamii nzima.
Wanabodi, rais wetu alitoa ahadi ya kuwepo kwa korti ya Kadhi na zipo sababu ambazo zilifanya yeye kuafiki ama kutoa ahadi swala ambalo sisi kama raia wake inabidi tujenge hoja zinazolinda maslahi ya Taifa na sio kubomoa. Tatizo kubwa linalojitokeza hapa yaonyesha wazi sio korti hizi ila ni hofu yenu kwa Uislaam. Hofu ambayo Mtikila kama kiongozi wenu wa dini kainjenga ktk mioyo yenu na sasa mnaanza kuamini kabisa kuwa korti za kadhi ni mbinu ya waislaam kuutokomeza Ukristu. Hoja zenu zinajieleza wazi kabisa na hata hizo kodi mnazozungumzia ni sababu finyu zilizotanguliwa na hofu yenu kuhusu Uislaam.
Kitu cha maana hapa ni kutoa mapendekezo yetu ktk swala hili kisha tujenge hoja inayolingana na kuprotect maslahi ya nchi na sio kuzungumzia maswala ya fedha na kodi wakati ni fedha na kodi hizo hizo zinazoendesha serikali yetu ktk kila taasisi. Ni sawa na mtu kusema sheria za Uhalifu kuwepo kwa Polisi ama Jela ni upotozaji wa kodi za wananchi kwani mimi sio mhalifu na wala sintakuwa. Ukitazama kujitenga wewe na hao wahalifu kisha ukajenga hoja. Ikiwa kriti za kadhi ni too much kwenu jengeni hoja inayohusu korti hizi na waislaam sio kutazama nje ya waislaam kama tunavyozitazama korti zetu, Polisi na jela zetu tukitazama na kuzingatia Uhalifu (crime).
As a Muslim sioni sababu ya muhimu kwa Kikwete kwenda Vatican na naweza jenga hoja za kipuuzi lakini kama naelewa nini mahusiano ya jamiii ktk mawasiliano siwezi kuweka visingizio na kudai kwa nini kodi za waislaam zimelipia ziara hiyo ya rais huko Vatican!. Huu ni ufinyu wa kutazama swala zima linalohusiana na ziara za rais na kama nita raise swali kwa njia hiyo nitakuwa nachekesha. Zipo sababu nyingi za kuhoji ziara za rais lakini sio kwa mtazamo wa dini.
Rais Mwinyi alitoa ahadi ya kurudisha shule na mahospital kwa madhehebu ya dini hasa wakatoliki mbona hamkupiga makelele na kuuliza kulikoni kwa mtazamo huu mnaoutumia hapa. Naelewa kwa uhakika kuna walimu waislaam kibao walifukuzwa kazi zao kwa sababu tu ni waislaam lakini sijasikia mkisema yote haya isipokuwa leo Mtikila mshenzi mmoja kajenga mioyo yetu kuamini kuwa Waislaam ni Magaidi basi nanyi mnadakia na kuanza kumwita rais wenu GAIDI just because ni Muislaam aliyetoa ahadi kwa waislaam. Mbona Nyerere alitoa ahadi nyingi tu kwa Vatican na hakuna muislaam aliyejenga hoja za kipuuzi kuulizia kodi za waislaam.. ahadi ambazo alikuja zitimiza lakini bila kuathiri maisha ya waislaam.
Guys sisi tumesoma ktk shule za katoliki na tumelazimika kutumia majina ya kikristu kuweza kupata nafasi ya kusoma. Tazama huko Tanga kuna watu kibao wenye majina mchanganyiko utasikia mtu akiitwa Gregory Hamid, wote hawa wamebadilisha majina yao kwa sababu ya kutafuta elimu chini ya himaya ya kikristu leo sheria zinabadilika kidogo mnaanza kutazama ni kwa faida ya waislaam.
Pleeease kluna tatizo na korti ya kadhi toeni hoja zenu zikizungumzia korti hiyo na sio waislaam kuwa heading ya mada kwani wapo waislaam wasiokubaliana na korti hizo.
KUWAITA WAISLAAM MAGAIDI ni ushenzi, Upumbavu na Ufisadi mkubwa unaotokana na utumwa wa imani ya dini..