JK atakiwa kuomba radhi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
JK atakiwa kuomba radhi
MZOZO MAHAKAMA YA KADHI

na Agnes Mlundachuma
Tanzania Daima

SUALA la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini linazidi kupanuka, na kwa mara ya kwanza tangu mjadala huo uanze, jina la Rais Jakaya Kikwete limeanza kuingizwa katika mzozo huo.
Rais Kikwete ametajwa katika sakata hilo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, wakidaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika mgogoro huo, ambao sasa unazidi kuchukua sura tofauti.

Kwa upande wake, Rais Kikwete ametajwa akitakiwa kuwaomba radhi Watanzania, kwa kile kinachodaiwa kuwa, dhamira yake ya kutaka kuigeuza Tanzania kikatiba kuwa nchi ya Kiislamu na hivyo kuirejesha katika mzozo wa miaka ya mwanzo ya 1990 uliohusisha juhudi za baadhi ya viongozi kuiingiza katika kundi la nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).

Aidha, IGP Mwema amepewa siku 21 kumuomba radhi Mchungaji Christopher Mtikila, kutokana na kitendo chake cha kuwatuma askari wamkamate (Mtikila), kumhoji na hatimaye kumfungulia mashtaka ya uchochezi wakati hana kosa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mchungaji Mtikila, ambaye ndiye aliyeibua mjadala unaoendelea kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, alitaka tamko la Rais Kikwete la kuomba radhi liambatane na hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wote wa umma, waliohusika kwa namna yoyote katika kitendo hicho cha kuingiza Uislamu katika ilani yake ya uchaguzi, serikali na Bunge.

Aliongeza kuwa sambamba na hilo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho alidai ni kikundi cha maslahi ya kibinafsi cha watu fulani, nacho kifutwe kama inavyoagiza katiba.

Mtikila alisema, Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Halmashauri ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), walikutana na walitaka kutoa tamko la kupinga mapinduzi hayo ili kulinda katiba ya nchi, lakini serikali iliwahadaa wasifanye hivyo bali wangojee tume yao ilifanyie kazi suala hilo.

Hata hivyo, Mtikila alisema, inashangaza kuwa tofauti na ahadi iliyotolewa na serikali kwa taasisi hizo nyeti za kidini nchini, harakati zilianzishwa ili muswada kuhusu Mahakama ya Kadhi upelekwe bungeni bila Wakristo kujua, mpaka Mungu alipowafunulia na kuwawezesha kuwahisha ulinzi wao wa katiba mahakamani.

Alisema yeye hapingi kuanzishwa kwa mahakama hiyo, bali anachopinga ni kuingizwa katika katiba ya nchi ambayo kimsingi inapingana na suala hilo.

“Tunachopinga vikali sisi ni kuingizwa kwa dini ya Kislamu au Mahakama ya Kadhi katika katiba ya nchi yetu,” alisema na kuongeza kuwa hata kama kutakuwa na harakati za kutaka kardinali, askofu au paroko wa Kanisa Katoliki kuingizwa katika katiba ya nchi, atapinga kama atakavyopinga kuingizwa mtandao wowote wa kidini katika katiba.

Aliwataka Waislamu wasidanganywe kwa kuwa Mahakama ya Kadhi ni mradi wa watu wachache, na kuongeza kuwa, kuna nchi kadhaa za Kiislamu zimekataa mahakama hiyo kwa sababu sharia zake ni kinyume cha haki za binadamu.

Alisema hoja ya kuwa mahakama hiyo itashughulikia mirathi, hija na ndoa tu, ni ulaghai ili iingizwe katika katiba, baadaye makadhi waue watu wasiokubali dini ya Kiislamu na kuangamiza Wakristo na Wayahudi na kuchinja Waislamu watakaoiacha dini yao.

Alisema hivi sasa nchi haina Mahakama ya Kadhi, lakini Waislamu wanaoa, wanaolewa, wanapata mirathi na kesi zao za mirathi zinashughulikiwa na pia wanakwenda hija na kuhoji mahakama hiyo italeta mabadiliko gani katika masuala hayo yanayodaiwa kuwa itayashughulikia.

Aidha, Mtikila alisema kitendo cha baadhi ya Waislamu kupinga ziara ya Papa ni kutofahamu kwamba mbali ya Vatican kuwa makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, pia ni nchi huru ingawa ipo ndani ya nchi ya Italia.

Alifafanua kuwa Vatican ni sawa na Swaziland na Lesotho ambazo zimezingirwa na nchi ya Afrika Kusini.

Alisema Papa atatembelea Tanzania kiserikali sawa na kiongozi mwingine wa nchi na kwa kuwa kuongoza kanisa ni huduma ya kiroho, hawezi kuiweka roho pembeni anapokuwa katika ziara ya kiserikali.

Akifafanua kauli zake za awali kuhusu kupinga kwake utaratibu unaotaka kutumiwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi, Mtikila alikanusha kutamka kuwa Uislamu ni ugaidi na kusisitiza kuwa Mahakama ya Kadhi ndiyo chombo cha ugaidi ndiyo maana hata baadhi ya nchi za Kiislamu zinaikataa.

“Uislamu wa Watanzania usio na ukatili wa Mahakama ya Kadhi hauwezi kuitwa ugaidi kamwe,” alisisitiza.

Kwa upande mwingine, alisema mbinu ya kamati inayotetea mali za Waislamu iliyotangaza azma yake ya kumkata kichwa, ni hasira tu, kwa kuona pesa walizokuwa wanataka kupewa hazitakuwepo na suala hilo halitazungumziwa bungeni wala serikalini kwa kuwa lipo mahakamani.

Aliongeza kuwa, yeye hawakatalii Waislamu kuabudu, lakini si kuliiingiza suala hilo la kidini ndani ya katiba.

Kauli hiyo ya Mtikila inakuja wakati taifa likipita katika kipindi kigumu cha msigano wa hoja zinazokinzana kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi jambo lililogusa hisia za makundi mbalimbali ya Wakristo na Uislamu kiasi cha kutishia amani.

Baadhi ya kauli za waumini wa dini hizo mbili, ndizo ambazo kwa upande fulani zilisababisha taasisi za dola kuamua kuingilia kati na kuchukua hatua za kisheria.
 
What you see is not only that can be seen.

Anzisheni hiyo mahakma ya kadhi kwa namna yeyote muwezayo lakini kamwe! Mkome kutumia katiba yetu kwenye mambo ya kidini.
 
....udini wa aina yeyote ni wa kupingwa kwa nguvu zote na kama hatuna ukabila Tanzania tusipoangalia dini zitaanza kutufanya mambo mabaya na wote tutaumia,simzimii sana Mtikila lakini kwa hili namuunga mkono na hayo ya misamaha mimi sijui!
 
Ofcourse hapa hata mie namuunga si mkono tu bali hata mguu!

Jitihada zozote zile za kuingiza Kadhi ndani ya katiba utakuwa chanzo cha vurugu kubwa Tanzania. Hapo ndipo mwisho wa uvumilivu wa watanzania utakapo onekana!

Kuomba msamaha labda ni njia ya kistaarabu ya ya kumaliza uchafuzi huu!. Badala yake naona Wameamua kutumia mbinu ya kujifanya wana mfungua kesi kumnyamazisha mtikila kesi ambayo haitakaa isikilizwe bali itatumiwa kama chambo cha kusema kesi iko mahakamani mpaka mwisho wa dahari! kalaghabaho!
 
itafika mahali wakristo nao wataomba mahakama ya kikristo na nchi iendeshwe kwa sheria kumu za Mungu yatatokea mambo ya Lord resistance army ya Uganda. Naoana kama sheria na katiba ya nchi inamapungufu ni bora yenyewe ifanyiwe marekebisho. Tutaomba mahakama za kikabila (kimila) pia zianzishwe kama sisi wa Shinyanga tukimuona kikongwe mwenye macho mekundu tuweze kumwadhibu kwa sheria zetu.
 
Mtoto wa Mkulima unajua Wakatoliki wana mahakama yao wenyewe inayohusu mambo ya ndoa, uongozi wa kanisa, na Sakramenti (ibada(ambayo rufaa yake ya mwisho ni kwa Papa? Mahakama hiyo haijaundwa kikatiba, na haitumii fedha za serikali kuiendesha!!
 
....na sisi huku Wanyarukolo tupewe sheria zetu, tukimwona kijana amevuta mlungula na jicho jekundu kama nyanya iliyokwiva kipindi cha masika tunamwazibu kwa sheria zetu!!!!

SteveD.
 
Mtoto wa Mkulima unajua Wakatoliki wana mahakama yao wenyewe inayohusu mambo ya ndoa, uongozi wa kanisa, na Sakramenti (ibada(ambayo rufaa yake ya mwisho ni kwa Papa? Mahakama hiyo haijaundwa kikatiba, na haitumii fedha za serikali kuiendesha!!

Mkuu bado sijapata kuisoma makala yako ya mahakama ya Kadhi ila naomba unielewesha hapa kidogo. Inamaana hii mahakama ya kadhi ikiunwa itakuwa inaendeshwa na pesa za serikali?
 
Mkuu bado sijapata kuisoma makala yako ya mahakama ya Kadhi ila naomba unielewesha hapa kidogo. Inamaana hii mahakama ya kadhi ikiunwa itakuwa inaendeshwa na pesa za serikali?

ndiyo kwani kwa modeli waliyo nayo sasa, itakuwa ni sehemu ya Mahakama ya Tanzania, kama tulivyo na Mahakama ya Biashara, Mahakama ya Watoto n.k HIvyo, wafanyakazi wake watakuwa ni waajiriwa wa serikali hasa wale wanasheria na makadhi..
 
Nimeona makala ya mtikila,kwa kweli amejieleza vizuri sana.Ujumbe aliopeleka una mantiki kubwa sana.Huyu mwanaharakati ni muhimu sana katika jamii kutokana na msimamo wa kuiita spade ni spade na si vinginevyo.Bravo mtikila!!Inaonekana hii serikali ya muungwana ni ya kilaghai, wamejaribu kuwapiga bao kwa kuwadanganya hata viongozi wa kanisa.This is very bad indeed.Ndiyo maana huyu mwanaharakati alireact kama simba aliyejeruhiwa baada ya kugundua huo utapeli na kuwahi mahakamani.
 
katika makala yangu ya Jumatatu, nitajaribu kuonesha ni jinsi gani pande zote zinaweza kufikia hitimisho. Tatizo ni kuwa bado viongozi wetu hawajafikia mahali pa kuweza kuzungumza na kuhitimisha mijadala. Suala la Kadhi ni lazima lifikie kikomo
 
unaposema suala la kadhi lazima lifikie kikomo yaani nashindwa kuelewa wewe ni muamuzi au mtoa hoja ? why you seem so superior on the internet ??
 
........kikomo hicho ni kutupwa kapuni bila mjadala zaidi!!! huu ni upotezaji wa wakati, inakuwaje watu wanakubali kuburuzwa kwenye "not so comfort zones" na wanasiasa? hii issue inatumika for political gains na hicho ndicho kinachonikera zaidi.
 
unaposema suala la kadhi lazima lifikie kikomo yaani nashindwa kuelewa wewe ni muamuzi au mtoa hoja ? why you seem so superior on the internet ??

Hiyo ni hoja ambayo haijali nani anasema. Hata mtoto mdogo akija na kusema "malizeni mabishano" atakuwa anasema ukweli. Mjadala wa Mahakama ya Kadhi ni lazima ufikie kikomo, aidha kwa kukubaliwa, au kukataliwa, au kutojibiwa vyovyote vile. Kwanini unafikiri kusema hivyo ni kuwa superior? Nadhani anayesema kuwa "you seem so superior on the internet" ndiye anayejifikiria kuwa superior to the point of making such an arrogant assumption.
 
Kada,
Tatizo lake huyo anataka kupata kotekote.....flip flop kama ya John Kerry(sura ndefu). Ukimsoma vizuri utaona he is for Kadhi courts and at the same time he is NOT!!!? hapo sasa, ndio maana mie nasema kuna walakini.........anataka JK apewe talaka na waislamu kama punishment ya kuwaahidi na kuwanyima mahakama ya kadhi. Yeye anaangalia upande mmoja tu, bila kujali consequences in a bigger picture!. Watu wengine bwana............
 
YN, hujanisoma vizuri. Sina pande mbili katika hili. Waislamu wa haki kama watu wengine kuamini dini yao na kufanya kile ambacho imani ya dini yao wanaamini inawataka. Kama Mahakama ya Kadhi ni muhimu katika dini yao mimi na wewe ni nani wa kuwaambia hapana? Ninachoonesha hadi hivi sasa ni kuwa sababu zinazotolewa ni dhaifu na si za msingi. Hata hivyo zipo sababu za msingi wanazoweza kuzitoa na hizo ninazionesha. Sasa ukinisoma vizuri utaweza kuelewa hilo.
 
Hiyo ni hoja ambayo haijali nani anasema. Hata mtoto mdogo akija na kusema "malizeni mabishano" atakuwa anasema ukweli. Mjadala wa Mahakama ya Kadhi ni lazima ufikie kikomo, aidha kwa kukubaliwa, au kukataliwa, au kutojibiwa vyovyote vile. Kwanini unafikiri kusema hivyo ni kuwa superior? Nadhani anayesema kuwa "you seem so superior on the internet" ndiye anayejifikiria kuwa superior to the point of making such an arrogant assumption.

wewe ndio unadhani uko more superior hadi kiasi cha kuwafokea mapastors tz utadhani wanakufahamu bana, halafu unatakiwa uonyeshe heshima katika mambo unayotaka yatendeke !

kama mtoto wa kuja kusema mabishano yaishe, basi UNGEMUITA HUYO MTOTO KWANZA KATIKA ILE MADA KUHUSU PICHA ZA JK AMBAZO THEY NEVER EXIST !!

SHUKRANI !
 
Kada,
Tatizo lake huyo anataka kupata kotekote.....flip flop kama ya John Kerry(sura ndefu). Ukimsoma vizuri utaona he is for Kadhi courts and at the same time he is NOT!!!? hapo sasa, ndio maana mie nasema kuna walakini.........anataka JK apewe talaka na waislamu kama punishment ya kuwaahidi na kuwanyima mahakama ya kadhi. Yeye anaangalia upande mmoja tu, bila kujali consequences in a bigger picture!. Watu wengine bwana............

na nimeona kitu kibaya sana anataka kukidhi mahitaji yake kwa kufikia conclusion ya jambo muhimu na ambalo limepamba moto na linahitaji muda mwingi kulifikiria, lakini kilichonishangaza ni yeye kusema kwamba vyovyote itakavyokuwa lakini linatakiwa lifikie kikomo ! is he serious ??

mahakama ya kadhi ikiundwa je mtaanza kulalamika na kusema kikwete anapendelea uislam na ana mpango wa kuigeuza tz kuwa islamic state au ? je alipoangalia pande zote kwa hao wanaotaka kadhi na wasiotaka kadhi ILI MRADI TU ijulikane hatma ya uamuzi wake itakuwaje ?

Mwanakijiji stop pushing meeen, you are pushing tooooo hard kwa vitu muhimu, halafu wakikosea utapata upenyo wa kurusha madongo yako na kuanza kusema "tuliwaambia hawa viongozi wetu".

kama wewe unaona suala la kadhi lipo na linashuhulikiwa, huku mambo mengine yanaenda kama kawaida kuna tatizo gani ? au umeambiwa kuzungumzwa kwa kadhi ndio serikali nzima inasimamisha mishale ya saa ya kufanyia kazi na kuangalia suala la kadhi ??

Plz mwanakijiji dont just talk for the sake of talking, IF YOU REALLY WANT TO TALK THE TALK WITH OUR BELOVED LEADERS, DO SO, WITH WALKING THE WALK ALSO !
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom